Pesa na Penzi kipi kinaendesha Dunia?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kuna watu wanadai kama kusingekuwa na hali ya watu kupendana kusingekuwa na haja ya kutafuta PESA kwa nguvu hizi zinazotumika sasa. Wengine wanadai PESA ndizo zinazofanya watu wapendane au wachukiane, bila PESA hakuna PENZI au CHUKI. wewe unaonaje kati ya PESA na MAPENZI nini kinaindesha jamii ya dunia?
 
Kwani mapenzi ndio yanajenga nyumba? Si mtalala nje? Me nachagua Pesa bwana mapenzi hayana issue sana kama hakuna mapenzi si nakwea bomba tu?
 
Ndiyo ni watu lakini wakiwa na nini. Wakiwa na PESA mifukoni mwao au wakiwa na mapenzi mioyoni mwao?

Sijataja kimojawapo maana ukiwa na kimoja bila kingine maisha hayawezi kukamilika. Vinategemeana..na anaeiendesha dunia ni yule mwenye uwezo wa kutoa/pata vyote.
 
Sijataja kimojawapo maana ukiwa na kimoja bila kingine maisha hayawezi kukamilika. Vinategemeana..na anaeiendesha dunia ni yule mwenye uwezo wa kutoa/pata vyote.

Kwa hiyo haiwezekani kumpenda asiye na PESA?
 
siamini kama umeliogopa hili swali!

jG bana...you know me..woga nilishamtaliki zamani!!

Ishu ni kwamba Hamna anaeweza kuendesha maisha kwa mapenzi pekee wala anaeweza kuishi kwa furaha akiwa na pesa pekee bila mapenzi (yoyote yale..ndugu/marafiki/mwenzi/watoto n.k) kwahiyo siwezi kuchagua kimoja. Unless tuko kinadharia zaidi na sio kiuhalisia!!
 
ndio mi najua na naelewa, nadhani hapa inabidi twende tu kinadharia tu ili kushibisha uzi, naamini Kigarama nae anaelewa yote haya ila anataka tu kujua akili/moyo wa mtu hapa umezingirwa na nini hasa!
Mi nshasema PENZI, na wewe si utaje kimoja tu kati hvyo jamani hahahaha
 
Pesa,money,hela,ndalama,................ndio mpango mzima bhana.....mengine urembo tu.
 
Pesa na penzi havina mahusiano yoyote!!!!!bali tumejifisha ulimbukeni na umbumbu kwamba pesa ndio kibali cha kupata mapenzi,wakati ALLAH anaiumba dunia na kuwaumba ADAM na HAWA hakuweka pesa kwenye bustan ya EDEN,bali aliweka vyakula pekee,SHETANI aliyelaaniwa kwa kukataa kum-sujudia ADAM ndiye aliyeleta mambo ya pesa,SASA kama unamfuata SHETANI basi penzi litakuendesha kwa pesa,bali kama unamfuata ALLAH pesa yako utaitumia ktk jihadi ya haki na siyo anasa!!!!!
Nadhani darasa limeeleweka inshaallah!
 
ndio mi najua na naelewa, nadhani hapa inabidi twende tu kinadharia tu ili kushibisha uzi, naamini Kigarama nae anaelewa yote haya ila anataka tu kujua akili/moyo wa mtu hapa umezingirwa na nini hasa!
Mi nshasema PENZI, na wewe si utaje kimoja tu kati hvyo jamani hahahaha
Ukiiweka namna hiyo basi MAPENZI....kama ni pesa hata mimi naweza kutafuta!!
 
Back
Top Bottom