Pesa chafu kuelekea uchaguzi wa 2015

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Ni vita: Lowassa, Sumaye, Mwandosya
Waandishi Wetu

Toleo la 258
12 Sep 2012


258_lowassa.jpg



  • Madai ya matumizi ya fedha chafu yaibuka
  • Udini na ukabila nao watajwa


    YANATAJWA majina makubwa: Edward Lowassa, Frederick Sumaye, Hamisi Mgeja, Anthony Diallo, James Lembeli, Clement Mabina, kwa uchache katika mchakato wa kutafuta kupitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama tawala CCM katika chaguzi za chama hicho zinazoendelea.

    Taarifa zinasema kwamba pengine mpambano wa safari hii utakuwa mkali zaidi kwa kuwa ndio utakaoamua ni nani hasa wanasimamishwa na chama hicho katika kuelekea kumpata mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati huko Arusha anatajwa Lowassa kupambana na hasimu wake wa muda mrefu Dk. Salash Toure, mkoani Manyara uwezekano mkubwa mpambano huo utawakutanisha Sumaye na Mary Nagu; Diallo na Mabina (Mwanza) na Mgeja na Lembeli (Shinyanga) huku taarifa zikisema pia kwamba mchakato wenyewe umegubikwa na malalamiko ya matumizi ya fedha, uhasama wa kisiasa na hoja za kikabila

    Raia Mwema - Ni vita: Lowassa, Sumaye, Mwandosya
 
Back
Top Bottom