Pepo la baba mwenye nyumba lagoma kutoka, ahama

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
HATIMAYE maombi yaliyofanywa na msichana mmoja akishirikiana na waumini wenzake kumuondoa pepo chafu baba m,wenye nyumba ili asihame kwenye nyumba hiyo lagoma kutoka na ahama
Msichana huyo juzi alionekana akihamsiha vitu vyake kwenye chumba alichokuwa amepanga baada ya mmiliki wa nyumba hiyo kumtaka ahame kwa kuwa alikuwa akikiuka maagizo aliyompa awali ya kutowasumbua wapangaji wenzake

Msichana huyo awali alimuomba mmiliki wa nyumba hiyo asimuhamishe kwa kuwa alivutiwa na nyumba hiyo na nyumba hiyo ilikuwa jirani na alipokuwa akisali bila kutumia gharama ya nauli ya mabasi ya kila siku

Hata hivyo ombi hilo liligonga mwamba na alichukua uamuzi wa kumfanyia maombi kuondoa pepo chafu lakini maombi hayo yalionekana kugonga mwamba na kuonekana pepo hilo kukataa kuondoka kwa mmiliki huyo na kuendelea kusimamia msimamao wake wa kumtaka aondoke

Hivyo juzi msichana huyo alionekana kuhamisha mali zake akisaidiwa na waumini wenzake na alihamia sehemu ambayo haijafahamika mara moja

Awali msichana huyo alikuwa akiendesha maombi katika moja ya chumba alichopanga katika nyumba hiyo na kusababisha upotevu wa amani ka kusababisha kelele endelevu katika nyumba hiyo na kuwasumbua wapangaji wengine waliokuwa wamepanga katika nyumba hiyo

Hata hivyo ilidaiwa mmilikiwa nyumba hiyo alimtaka msichana huyo akifanya maombi afanye tahadhari asisumbue wenzake lakini ilishindikana na kuendeleza maombi hayo na waumini wenzake hata usiku jambo ambalo lilishindwa kuvumuliwa na wapangaji wenzake
 
Back
Top Bottom