Stevemike
Senior Member
- Mar 12, 2011
- 117
- 15
Kuna jambo nimelishuhudia jana jioni nikashangaa. Mchungaji mmoja na waombaji wenzake walikuwa wanamuombea binti aliyepagawa mapepo nikasikia pepo linasema hivi, 'JAMANI KARIBUNI LOLIONDO KWA BABU MPATE KIKOMBE, HALAFU WEWE MCH. UNAMPINGA SANA BABU, WENZAKO WANAKUJA. KWA NINI? UNAJIFANYA UNA IMANI SANA?" baadaye yule pepo akashindwa na kumuacha binti huyo akawa mzima. Hii imekaaje? Pepo anahusikaje kuwakaribisha watu kwa babu? Au ana ushirika gani na babu? Au ni uongo wa shetani tu?