Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Inasadikika kuwa unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji. Vivyo hivyo katika mapenzi kuna wakati inafikia ambapo mpenzi hawezi kumlazimisha mwenza wake kitu fulani. Pamoja na kuwa kunyenyekeana na kuafikiana ni muhimu ni dhahiri kuwa kuna wakati hilo haliwezekani. Je, nani anakuwa na uamuzi wa mwisho hilo linapotokea? Na, je, uamuzi huo utatekelezekaje kama pande zote zimeshindwa kufikia muafaka?