Akiwa mwanaume mwelewa atazidisha bidii kutafuta sources nyengine za pesa ... mwanaume hasa ... rijali kabisa hawezi kupokea hela ya mwanamke ..... mwanamke kumpa hela yake ya mshahara .. mhh! sidhani kama ni kuwa thabit ama kumpa uhalisi wake ... mwengine ni mharibifu ... na hela usioifanyia kazi waweza kuzitumia utakavyo maana hujui uchungu wake ... mimi nadhani mugawane majukumu halafu umsaidie tu pale ambapo anaupungufu ... heshima ibaki palepale
Mwanaume kuwa rijali 100% ni ngumu kama ilivyo mwanamke kuwa mtii 100%
tukubali kukosa kidogo kila upande.
manake hapa mimi napata picha ya mwanaume rijali kiafrika ni yule ambaye maamuzi yote ya nyumbani anafanya yeye. mimi kama mwanamke sitamuweza.
Kwa ajira za sasa, kupanda na kushuka kwa kipato si kitu cha muda mrefu sana.
sisi tumeshawahi kusimamia nyumba kwa zamu mara kibao, ila tofauti ni kuwa yeye akiwa nazo anatoa kiasi fulani anaweka mahali/account naweza kuchuka bila kuombaomba kila saa, na mimi pia hivyo hivyo, ila uwazi katika jumla kuu ni muhimu.
Pia kwamba balance uliobaki nayo ni kwaajili ya personal use tu.
inahitaji kujitoa zaidi na TOTAL TRUST IN EACH OTHER. Ambayo nadhani kwa muelekeo wa hapa ni ndogo.
tution ya bure kwa kina dada (ambao bado bado) ukiua self confidence ya mumeo utamchukia mara moja. Jitahidi aweze kutembea kifua mbele humu duniani, hasa kwa rafiki zake na ndugu.