Kardinali Pengo: Wanasiasa waacheni Maaskofu wafanye kazi zao, msiwafundishe kazi

Cardinal Pengo told the Government not to meddle in religious affairs by censoring evangelical circulars.
Cardinal Pengo was apparently responding to the recent criticism by some CCM and government officials of the Roman Catholic Church circular, which guides its followers on how to choose good leaders in the civic poll later in the year, and in next year's General Election.

Wakuu hayo maneno meusi hapo ni dhahir kuwa Waraka huu ni Ibada ya kanisa Katoliki. Yaani Pengo anazungumzia IBADA ya dhehebu la katoliki la haki za kanisa hilo ktk ibada zake..
yale yale.. nilokuwa nikisema toka mwanzo sasa hivi bila shaka mtanielewa vizuri sana...

Ni vigumu sana kwa mtu asiyekuwa Mkatoliki akajaribu ku reason out kwa kutumia elimu nje ya elimu ya katoliki, ile ilofundisha ibada hizo ukapata jibu la ibada hii..Ni ujinga mkubwa kujaribu kutumia tamaduni, fikra, elimu dunia ktk mambo ya dini ya wahusika wakati fikra hizo ndizo zilikuzuia toka mwanzo usiamini au kuabudu mafundisho ya dini au dhehebu hilo..

Yanayo wezekana ktk Ukiristu au Ukatoliki sii lazima yawezekane na yatumike katika ibada za Waslaam. Haramu ya waislaam sio lazima iwe ya Wakristu au Katoliki na Uhuru wa madhehebu haya kufanya ibada zao ni jambo ambalo halina mjadala nje ya vyombo vya dini..kwani kufanya hivyo ni kuzua Matatizo mengine makubwa zaidi ambayo tutayalamizisha tu pasipo kubaliana.

Leo hii katika mazishi ya Askofu tumeona maswala ya Siasa yakizungumzwa wakati kama ingekuwa ktk dini ya Kiiislaam hasa dhehebu la Sunni la ukawakuta hao kina Ansar Sunni wamesimama mbele ya kaburi au kusimamia mazishi ukaleta hizi habari za Siasa mazikoni wangekugeuza volleyball....
Sii Pengo au Sheikh Simba ndio wangesema maneno yanayohusu Uchaguzi ktk msiba na hasa mazishi ya kiongozi wa dini, bila shaka angepigwa kibao cha Kereb kama alivyofanyiwa Mwinyi ktk Maulid.

Hivyo ni kawaida ya waumini wa kanisa Katoliki kuzungumza vitu hivi ktk mazishi, au hata kunywa pombe matangani, lakini hairuhusiwi kabisa kwa Waislaam..Hivyo ni huwezi kunambia nani mwenye haki zaidi ya mwingine kwa kutumia mijadala nje ya kutambua haki ya wahusika kwanza..

Yaani haya maswala ya Waraka na Mahakama ya kadhi ni ndoto mbaya sana niliyoiona miaka miwili iliyopita nwa kwamba ndiyo itakuwa angamizo la UMOJA na Mshikamano wa Watanzania..
Bila shaka wakati wake umewadia na sasa hivi kilichobakia ni kila msafiri kuchunga mzigo wake.. nauona mwisho wa Uhuru wa Mtanzania na kwamba uchaguzi wa mwaka 2010 ndio kilele cha amani na Utulivu nchini.. yote itatokana na UDINI...

UDINI ni kushindwa kwa muumini au Waumini wa dini au dhehebu moja kukubali na pokea ibada za waumini wengine kama ni haki ya waumini hao na wanaweza kufanya ibada hizo mahala popote wakati wowote maadam haitaweza kuathiri waumini wa madhehebu mengine..
 
Last edited:
Kikwete ana kwa ana na Maaskofu Katoliki
lC.gif
Mwandishi wa Raia Mwema​
Agosti 26, 2009
rC.jpg
bul2.gif
Atarajiwa kupoza mtafaruku wa Waraka
bul2.gif
Kanisa lasita kumwalika kuwa mgeni rasmi wa hafla
WAKATI mjadala kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki ukipamba moto, Rais Jakaya Kikwete, leo Jumatano, anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Anthony Petro Mayala (69) atakapokutana uso kwa uso na Maaskofu wote wa Kanisa hilo ambao ndio waliobariki waraka huo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, mbali ya Rais Kikwete, viongozi wastaafu akiwamo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa wanatarajiwa kushiriki mazishi hayo.
Askofu Anthony Petro Mayala ambaye alifariki dunia ghafla Jumatano wiki iliyopita atazikwa leo ndani ya Kanisa Kuu la Epifania-Bugando jijini Mwanza.
Taarifa zilizopatikana wiki hii, Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili Mwanza leo asubuhi na anatarajiwa pia kutumia fursa hiyo ambayo inaelezwa amekuwa akiitafuta “kuweka mambo sawa”, baada ya kuwapo sintofahamu kati ya Serikali yake na Chama cha Mapinduzi (CCM) anachokiongoza upande mmoja na Kanisa hilo lenye nguvu kubwa duniani upande mwingine.
Habari za ndani ya Kanisa Katoliki zinasema tangu baada ya Waraka wao kutoka, limekuwa halifurahishwi na mashambulizi yaliyotoka serikalini na katika CCM na kwamba kwa sababu hiyo kumekuwako na hali ya kutaka kumgomea ama kumsusa Rais Kikwete.
Dalili za mwanzo za hali hiyo ni kwamba Kanisa hilo, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limesita kumwita Rais Kikwete kuwa mgeni rasmi katika shughuli za uchangiaji wa shule moja ya jimboni humo.
Habari za ndani zinaeleza kwamba Rais Kikwete alikuwa awe mgeni rasmi katika shughuli ya uchangiaji wa shule moja inayomilikiwa na Kanisa Katoliki lakini kutokana na kile kilichoelezwa ya kuwa ni “uzito mkubwa” ratiba ikabadilishwa na badala yake akaombwa kiongozi mmoja, mstaafu ndiye awe mgeni rasmi.
“Awali walimwalika kiongozi wa juu serikalini lakini wenzake wakasema si vyema kumtumia kiongozi huyo ambaye ni Mkatoliki na badala yake aende Rais Kikwete ambaye ni Mwislamu. Lakini kukatokea uzito mkubwa kutoka ndani ya uongozi wa Kanisa Katoliki na sasa inaelezwa bado haijaamuliwa ni nani awe mgeni rasmi japokuwa anatajwa sasa Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi,” anaeleza ofisa mmoja wa Kanisa ambaye yuko karibu na Kanisa Katoliki Dar es Salaam.
Uzito huo wa kumwalika Kikwete kuwa mgeni rasmi unaelezwa ndani ya Kanisa Katoliki kuwa unatokana na tamko la CCM kupinga matamko ya Kanisa hilo, tamko lililotanguliwa na kauli tata zilizotolewa na mwanasiasa mkongwe anayetajwa kuwa karibu na Kikwete, Kingunge Ngombale-Mwiru.
Pamoja na ukweli kwamba CCM haijaukemea rasmi Waraka huo wa Wakatoliki, matamshi ya baadhi ya vigogo kama Mzee Kingunge yamekuwa hayapokelewi vizuri ndani ya Kanisa Katoliki nchini.
Kikikariri maamuzi ya wiki iliyopita ya Halmashauri Kuu yake, CCM, katika taarifa yake, kilionyesha wazi kutoridhishwa na Waraka huo lakini kikakwepa kuukemea, na badala yake kikaelekeza viongozi wakuu wa nchi kukutana na viongozi wa dini kurekebisha hali hiyo, huku viongozi wa Kanisa Katoliki wakionyesha wazi kutotaka kurudi nyuma.
Tamko la NEC lililotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, John Chiligati lilisema: “Baada ya NEC kuzingatia Waraka wa Maaskofu, na hasa malumbano na hisia tofauti zilizojitokeza kuhusu Waraka huo, imeelekeza kwamba viongozi wakuu wa nchi wafanye mazungumzo na viongozi wa dini zote ili kutafuta njia tulivu ya kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii yetu.”
Habari zinasema kwamba huenda zikatolewa kauli za kujaribu kujibu mapigo kutoka kwa wanasiasa wakati wa mazishi ya leo.
Kanisa Katoliki ni moja ya makanisa yenye mtandao mkubwa wa kisayansi duniani kote na nchini Tanzania limejikita kwa kiwango kikubwa kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa.
Pamoja na kutotaja chama, Waraka wa Kanisa Katoliki ambao sasa umekuwa ukienea kwa kasi nchi nzima umekosoa kwa kiasi kikubwa utendaji wa Serikali iliyoko chini ya Chama cha Mapinduzi na kutoa ushauri mbadala unaoelezwa kukera wakubwa.
Mbali ya kuandaa Waraka huo, Kanisa hilo tayari limeanza utekelezaji wa programu yake tokea Januari mwaka huu inayoishia mwaka 2011, ikiwa na lengo la kuwaandaa waumini wake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na baadaye tathmini yake baada ya uchaguzi huo.
Sehemu ya programu ya Kanisa hilo inasema: “Watu wengi wanadhani kwamba mambo ya umma si sehemu ya majukumu yetu ya kidini na kiimani, na hivyo Kanisa halipaswi kujishughulisha na mambo hayo.
“Kinyume chake Kristo anatualika kuleta mafundisho ya Mungu, maadili ya asili yetu ya kibinadamu kama tulivyoumbwa na Mungu. Tunaalikwa kuyafanya hayo yawe ndio msingi na mwanga unaoongoza maamuzi na sera zetu.”
Katika programu hiyo ya kichungaji kumeandaliwa hatua madhubuti za ufuatiliaji ambao utaanzia kwa kufanyika mikutano ya makleri na viongozi wa halmashuri walei kujadiliwa katika ngazi ya Jimbo na kupewa umuhimu unaostahili.
“Katika kazi ya kuongoza mkutano wajumbe wa CPT (Wanataaluma Wakristo) na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi. Inapendekezwa paundwe timu ya Jimbo kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hii. Katika ngazi ya Parokia programu ilenge kufundisha wanavijiji/watu mitaani na katika jumuiya ndogo ndogo ili waweze kujadili masuala yaliyomo katika programu,” inaeleza sehemu ya waraka huo wa kichungaji.
Pamoja na uongozi wa juu wa Kanisa kueleza kwamba hii si mara ya kwanza kwa Kanisa Katoliki kuandaa waraka wa kuongoza waumini wake na wananchi kuhusiana na mambo muhimu, hatua ya mwaka huu imeelezwa si ya kawaida na inaashiria kuwapo kwa ombwe kubwa katika mfumo wa kiuongozi na kijamii.
Tangu Waraka huo kutolewa na kuibua mjadala mkubwa, hiyo itakuwa mara ya kwanza Rais Kikwete kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki akiwemo Polycarp Kardinali Pengo. Watakutana ana kwa ana mjini Mwanza mjini Mwanza wakati wa mazishi ya Askofu Mayala.
hs3.gif

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1643
 
Ama kweli ulevi wa madaraka una vituko vingi. NEC ya CCM sio serikali. Haina nguvu, kisheria, ya kuelekeza Maaskofu wakutane na viongozi wa serikali. Haina hata nguvu ya kumwelekeza Machinga aondoke barabarani.

Ni kukosa umakini kwa hali ya juu kwa CCM kukubali ionekana inapambana na Maaskofu. Kwa kisa gani? Kwa kuwafundisha Watanzania wachague viongozi wazuri?

Maaskofu huteuliwa na Baba Mtakatifu. Maoni wala baraka ya CCM haitakiwi kwenye huo uteuzi. CCM imeshamwona Askofu aliyetaka kuwa na nguvu za kichama?

Ni jukumu la Maaskofu, hata mbele ya macho ya Mungu, kukemea na kupigana ili kuondoa uovu nchini. Ikibidi Askofu anakubali kufungwa au hata kuuawa kuliko aache kukemea uovu. Na waraka walioupa baraka zao ni wa kufundisha watu namna ya kuondokana na uovu (kwa kuchagua viongozi bora).

Zamani, wakati Kingunge hajachanganyikiwa bado, angeishauri CCM isizungumzie kabisa waraka uliotolewa.
 
Ukweli ni kwamba kosa kubwa la CCM ni kupungukiwa na vision yao ya tangu enzi za enzi. Hii inatokana na ushawishi wa hatari wa Lowassa na Rostam.

EL na RA wako tayari kufanya lolote ili kufanikisha maslahi yao binafsi na sio ya chama chao wala ya taifa. Kama CCM wangeachwa kufikiri kwa vichwa vyao wenyewe wasingejishushia hadhi kiasi hicho hadi kuwafananisha wabunge na walevi na kuliita bunge letu ze comedy, au kujijengea uadui na kanisa katoliki.

Lakini huu ndio mwanzo wa mwisho wao! Ni vizuri kwamba mabadiliko yanakuja kwa kasi kuliko wengine tulivyotarajia. CCM watakapokuja kugundua wanatumiwa na watu wawili tu it will be too late! Watakuwa tayari wameshaonyeshwa mlango wa kutokea!
 
Maneno ya Pengo hayakumtisha Mkapa, JK na kundi lake pekee bali hata akina Barubaru wenye uwezo mdogo wa kujua mambo na kubeba udini na chuki binafsi n akuacha haki za watanzania zife kwa jina la imani ama dini.

Pengo hata Rome wanamjua vyema alivyo. Pengo atakuwa kachukia sana , kwa kawaida Pengo ni mfuasi mzuri wa Mwalimu, kama kafikia hapa ina maana kachoka na tabia za JK na kundi lake.

Moto chini kwa sasa kuuzima si rahisi .

Rejea msimamo wake kuhusu Wakalizmatiki baada ya kuruhusiwa na papa katika kanisa la Tanzania...............
 
Wakuu hayo maneno meusi hapo ni dhahir kuwa Waraka huu ni Ibada ya kanisa Katoliki. Yaani Pengo anazungumzia IBADA ya dhehebu la katoliki la haki za kanisa hilo ktk ibada zake..
yale yale.. nilokuwa nikisema toka mwanzo sasa hivi bila shaka mtanielewa vizuri sana...

Ni vigumu sana kwa mtu asiyekuwa Mkatoliki akajaribu ku reason out kwa kutumia elimu nje ya elimu ya katoliki, ile ilofundisha ibada hizo ukapata jibu la ibada hii..Ni ujinga mkubwa kujaribu kutumia tamaduni, fikra, elimu dunia ktk mambo ya dini ya wahusika wakati fikra hizo ndizo zilikuzuia toka mwanzo usiamini au kuabudu mafundisho ya dini au dhehebu hilo..

Yanayo wezekana ktk Ukiristu au Ukatoliki sii lazima yawezekane na yatumike katika ibada za Waslaam. Haramu ya waislaam sio lazima iwe ya Wakristu au Katoliki na Uhuru wa madhehebu haya kufanya ibada zao ni jambo ambalo halina mjadala nje ya vyombo vya dini..kwani kufanya hivyo ni kuzua Matatizo mengine makubwa zaidi ambayo tutayalamizisha tu pasipo kubaliana.

Leo hii katika mazishi ya Askofu tumeona maswala ya Siasa yakizungumzwa wakati kama ingekuwa ktk dini ya Kiiislaam hasa dhehebu la Sunni la ukawakuta hao kina Ansar Sunni wamesimama mbele ya kaburi au kusimamia mazishi ukaleta hizi habari za Siasa mazikoni wangekugeuza volleyball....
Sii Pengo au Sheikh Simba ndio wangesema maneno yanayohusu Uchaguzi ktk msiba na hasa mazishi ya kiongozi wa dini, bila shaka angepigwa kibao cha Kereb kama alivyofanyiwa Mwinyi ktk Maulid.

Hivyo ni kawaida ya waumini wa kanisa Katoliki kuzungumza vitu hivi ktk mazishi, au hata kunywa pombe matangani, lakini hairuhusiwi kabisa kwa Waislaam..Hivyo ni huwezi kunambia nani mwenye haki zaidi ya mwingine kwa kutumia mijadala nje ya kutambua haki ya wahusika kwanza..

Yaani haya maswala ya Waraka na Mahakama ya kadhi ni ndoto mbaya sana niliyoiona miaka miwili iliyopita nwa kwamba ndiyo itakuwa angamizo la UMOJA na Mshikamano wa Watanzania..
Bila shaka wakati wake umewadia na sasa hivi kilichobakia ni kila msafiri kuchunga mzigo wake.. nauona mwisho wa Uhuru wa Mtanzania na kwamba uchaguzi wa mwaka 2010 ndio kilele cha amani na Utulivu nchini.. yote itatokana na UDINI...

UDINI ni kushindwa kwa muumini au Waumini wa dini au dhehebu moja kukubali na pokea ibada za waumini wengine kama ni haki ya waumini hao na wanaweza kufanya ibada hizo mahala popote wakati wowote maadam haitaweza kuathiri waumini wa madhehebu mengine..

Mkandara udini umekuzidi sana nawe.OK bada ya Pengo na maandiko yako meusi unataka nini kifanyike ?
 
Mtasema sana na CCM hawatishiki na maneno ya Pengo wala Jino na kila ukijifanya wewe ndio unaevaa msalaba mkubwa basi kwa CCM wanakuwa hata hawakuelewi upo upande gani.Maana mwisho watakwambia vua msalaba ili upambane kwenye siyasa .
Unajua Msalaba hauwezi kufua dafu kwenye Chama Cha Madracula (CCM) ,ukiangalia filamu za siku hizi utaona msalaba hauna nguvu mbele ya dracula.
 
Kwa hiyo akina Pengo wameamua kumuonyesha JK kuwa nguvu zake ziko serikalini na CCM tu huko kanisani inabidi anegotiate. Alifikiri wao ni wajinga wampe jukwaa lao kupiga propaganda za CCM. Kanisa lina wasomi na watu makini kuliko CCM. Alitakiwa ajue hilo siku nyingi!!!!
 
Mvutakamba,
Mkuu nimesema kitu gani hapo zaidi ya ku nukuu maneno ya Pengo mwenyewe. Au anapozungumza Pengo, sisi wengine haturuhusiwi kunukuu maandiko yake itakuwa Udini..wewe kama mtu uliyenisoma inakuaje uniulize mimi tena nini kifanyike! hata nikisema kifanyike kitu fulani, wee umesha nihukumu kuwa ni mdini, vinginevyo itakubalika vipi ktk akili yako.

Ama kweli NDIVYO TULIVYO, kazi kubwa sana kuwaelimishana na bila shaka kutokana na watu kama wewe ni dhahiri huu Waraka unakubaliika kwa imani ya kiroho badala ya kuwa ni Elimu ya Uraia, That is a Fact. na ndio maana tulitawaliwa na wakoloni hadi leo Ukoloni Mamboleo tukitawaliwa na wakoloni Weusi kina CCM.. kwa sababu unashindwa kuona pini hizi za kuamba ngozi.. ambazo ni muhimu ktk utawlaa wowote na zinatumika toka enzi ya Nuhu na kina Constatine..Imani ya dini ikitumika ktk utawala wowote husababisha maradha makubwa kuliko itikadi yoyote ile. Historia inatufundisha kwamba dini imekuwa itikadi ya kwanza iloleta madhara makuwba ya vita ya mauaji ktk historia ya vita na mauaji duniani..

Hizi dini hazikuona Ubaya wa mtu mweusi kutawaliwa, tena ndio kwanza kwa kutumia watawala waliowapitisha wao kwetu ndio waliweza kujijenga zaidi na zaidi ndani ya nchi maskini na changa kama Tanzania, Afrika na Third world kote..For years tulikuwa Utumwani hawakuona ubaya wa tawala zile hadi dunia nzima walipo laani Utumwa.. It is estimated kuwa Over 10 million ya watu weusi (Wabantu) walikuwa traded from Afrika each Year...
Mtu mweusi Mbantu aliikuwa dhahabu kuliko hiyo ya Bulyanhulu.. Ndio kwanza makanisa na miskiti ilitumika kukusanya Watumwa! -Acheni jamani achweni kuita watu wadini wakati hamjui Facts ni zipi! Hawa Masheikh, Maaskofu na sijui Makardinal ni binadamu kama sisi wana tamaa na wanaweza kabisa kutumia dini kukandamizia haki za wanyonge..Wengine tunagongana vichochoni mitaani usiku wa kiza ktk nyendo zisizokubalika kidni. Acheni nyie hu ushabiki..Ikraaa!

Augustine Moshi,
Mwalimu nakubaliana sana na wewe ktk upana wa hoja yako lakini mkuu imani yangu kubwa itaendelea kuamini kwamba hiizi Warakaz ni mafundisho ya dini iwe ya kiislaam au Kikristu na zinatanguliwa na Imani kubwa ya dini au dhehebu lolote kwamba SIN au DHAMBI ni matokeo ya mtu asokuwa na Imani ya dini..
UFISADI ni matokeo ya mhusika kutomkubali Mungu ktk mafundisho ya dhehebu husika.iwe Uislaam , Ukiristu, Ukatoliki au Sunii. Ufisadi ni dhambi kubwa na mara nyingi hufanywa na watu wasiokuwa na imani ya kitabu.. yaani hawafuati mafundisho ya dini..Hii ndio Principal tangulizi ktk circular ya dini yoyote ile, leo unambie tunaweza kuchambua Pumba toka ktk Mchele pasippo kutumia Principal hiyo..

Principal ya kwanza ya mafundisho ya dini zote ktk kuchagua viongozi hutanguliwa na shahada au niseme Ubatizo. Ikiwa mtu hajamkubali Yesu (Katoliki) au Hajashuhudia (Waislaam) aukwa lugha tunayoijua ya Kusilimu..Huyu mtu hawezi kuongoka wala kuwa msafi!..
Ni Principal ya kwanza kabisa ktk circular za dini zote duniani kwamba mtu yeyote asiyekubali mafundisho ya dini au dhehebu hilo HAFAI ktk Uongozi wa kiroho na UFISADI ni matunda ya mtu aliyepoteza imani ya kiroho na kutokubali mafundisho.

Itakuwa ni kinyume cha mafundisho ya dini au dhehebu lolote kumpendekeza KIONGOZI wa serikali ambaye hakubali mafundisho ya dhehebu husika. Nikiwa na maana Kardinal Pengo atakuwa anakiuka misingi ya Ukatoliki ikiwa atawafundisha waumini wa dhehebu la Katoliki kwamba kiongozi bora sii lazima awe amempokea bwana kwa jina la Yesu Kristu!..sidhani! na hata kama haikatazwi ktk Ukatoliki basi inakatazwa ktk madhehebu mengine na Inakatazwa ktk Uislaam...Kwa hiyo tunapotumia neno tuwachague viongozi wetu Kulingana na mafundisho ya dini... Hapa tuwe makini sana, yawezekana aya au sura hiyo inazungumzia zaidi viongozi wa dini kwani ktk uandishi wa Biblia karne ya Tatu< Ulaya na karibu dunia nzima ilikuwa ikitawaliwa na dini... yaani viongozi wa nchi walikuwa pia ni viongozi wa dini na madhehebu yalitawala milki hizo.

Hivyo sababu zinazotokana na Circular za kidini ndizo tunazopinga sisi wengine kuona DINI kuingilia Siasa kwa sababu Imani ya roho inatanguliwa na ikmani ya kuabudu, kile ulichobatizwa kuwa ndio njia pekee ya Usafi wa binadamu.
Nitaendelea kusema sikubaliani na waraka wa kanisa, waraka wa Msikiti, Sheikh, Kardinal, Ayatollah, Papa, Mullah, Dalai, Monk au mjumbe yeyote anaye represent imani ya dini ktk kuchagua viongozi wetu.
NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kushindwa kuona mbele (vision) kwamba uchaguzi wa 2010 utakuwa na ubaguzi mkubwa sana ikiwa imani za dini zitahusika ktk kuchagua viongozi wa nchi.
 
Last edited:
Afadhali Pengo amewaka maana muda mrefu toka tusikie sauti za busara na ukali kama hizi hasa baada ya baba wa taifa, pongezi pengo
 
Ndugu yangu Mkandara asante kwa shule kubwa sana ambayo umeitoa hapa .Sasa kwa kuwa mwongozo according to you umeuona ni ibada ya kanisa katoliki na si Wakristo , sasa tufanyeje na waraka ndiyo unashika kasi kama moto wa Greece ? ushauri ni upi ili kuondoa watu wachache kulalamika maana ujue wanao lalamikia ngoma hii wako wachache na wana hesabika.Tufanyeje ili kuweka umoja wa Kitaifa kwa mujibu wako ?
 
Mkandara unazungumzia hewani? Ni sehemu gani ya waraka inasema tuchague Mkatoliki? Waraka umewekwa hapa JF. Usome.

Baraza la Maaskofu la Tanzania halipingi kuchagua Rais asiye Mkatoliki. Lilikaribisha, kwa furaha, uchaguzi wa Kikwete na ule wa Mwinyi.

Sio tu kwamba waraka hausemi tusichague mtu wa dini gani, bali hausemi vile vile tusichague mtu wa chama kipi. Ila mimi nasema tusichague mtu wa CCM. Kwangu mimi, mpenzi wa fisadi ni fisadi.
 
Augustine,

Mbona Mbowe naye ni fisadi? Kwahiyo watu wasichague CHADEMA yote kwasababu ya makosa ya Mbowe?

Kwa vyama vya Tanzania kila ukichambua viongozi utakuta tu viongozi ambao kwa njia moja ama nyingine wameiba. Muhimu kwasasa ni kuhamasisha wananchi ili wachague watu wenye uwezo na wasio wezi bila kuangalia ni chama gani.

Ukianza kufuata ya samaki mmoja akioza basi wote wameoza, kwa Tanzania hutapata hata chama kimoja cha kukichagua.
 
Engineer una madai mazito na hapa si mahala pa matusi na uongo.Wenzako walianza a Mbowe na ufisadi wake wakashindwa .Sasa wewe tueleze ufisadi wa MBowe vinginevyo itetee CCM kwa hoja na si zaidi ya hapo .Pendo kesha wapa ukweli mbele ya Mwenyekiti wenu .
 
Lunyungu,

Si wewe ndiye unasema huna chama? Unaona Mbowe sio fisadi kwasababu na wewe ni fisadi kama yeye ha haaa!

Mkimpatia Uenyekiti Zitto basi nitahamia CHADEMA!

Pengo alikuwa anamsema pia Mengi ambaye ni mfadhili namba moja wa CHADEMA.

CCM wanafadhiliwa na mafisadi papa, CHADEMA wanafadhiliwa na mafisadi Nyangumi.

Sisi maskini tufadhiliwe na nani? Bado nina kadi ya TLP.
 
Ndugu yangu Mkandara asante kwa shule kubwa sana ambayo umeitoa hapa .Sasa kwa kuwa mwongozo according to you umeuona ni ibada ya kanisa katoliki na si Wakristo , sasa tufanyeje na waraka ndiyo unashika kasi kama moto wa Greece ? ushauri ni upi ili kuondoa watu wachache kulalamika maana ujue wanao lalamikia ngoma hii wako wachache na wana hesabika.Tufanyeje ili kuweka umoja wa Kitaifa kwa mujibu wako ?

Kama wanaolalamika ni wachache mfano 2% basi tayari umoja wa kitaifa umekamilika maana tuna 98% wanaokubali. Asilimia hiyo haipatkiani popote duniani hata Nyerere alikuwa anakubalika lakini si kwa silimia hiyo.
 
Muwadhama Polycarp Kardinali Pengo anazungumza katika mazishi ya Askofu Mayala Mwanza ambako anazungumzia ufisadi na maovu mengine, lakini anaonekana kukemea ufisadi huku akionekana kuwabeza wanaopambana na ufisadi. Iko live Star TV.

Yuko JK na Mkapa

Wanahabari acheni kuandika hizi habari za kidini. Kama TZ haiongozwi kidini kwanini bado tunaandika hizi habari?
 
Kwa hulka na silika ya mwanadamu huwa ni mtu wa kujisahau sana.

Nakumbuka kwenye msiba wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanda ya ziwa baba askofu mayala baba asikofu pengo alitamka maneno yafuatayo.

Nanukuu:
Serekali haiwezi kuingilia mambo ya dini,serekali haipaswi kuwafundisha viongozi wa dini namna ya kuubiri neno la yesu,akimanisha injili,injili ni neno la mungu halitakiwi kuongezwa kitu wala kupunguzwa,tena alienda mbali zaidi na akatolea mifano nchi za kipepari na nchi za kikomnist.

Nanukuu mapepari japo wana dhambi lkn wanaamini kuwa kuna aliyeko juu yao ambaye ni mungu baba,wakomunisti hawamini dini na kutokuamini kwao hamna dini pia wanaamini kuna mungu,sasa juzi baba askofu amekubali serekali iwafundishe viongozi wa dini namna ya kuhubiri neno la mungu (injili) ndio maana nimesema binaadamu ni watu wa kujisahau sana na ndio maana huwa wanatenda dhambi kila wakati.

Baba askofu aliyasema hayo kwenye msiba wa baba askofu mkuu kanda ya ziwa,tena raia kikweke alikuwepo na viongozi wengine wengi tu,akiwemo na sita membe wasira na wengine wengi tu,baba askofu alitamka hayo akiwa anajibu kauli ya mh:rais kikweke kwenye kampeni za mwaka 2010 baada ya baraza la maskofu tanzania kutoa waraka wa kinabii unahusu uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Kwa wali wasikumbuka waraka ule ulileta mgongano mkubwa sana kati ya mzee kingunge na kanisa katoliki.

Sasa cha kushangaza mtu yule yule amebadilika,amewajeka wenzake,kwa kifupi amelijeuka baraza la maskofu tec kwa kisingizio cha kutoa maoni yake binafsi lkn tufanyeje ndio kiongozi wetu na ni mtu mzima hawezi kuomba msamaha hadharani,kiafika huwa baba haombi msamaha kwa na ss tunamsamehe
 
Back
Top Bottom