Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

hivi what if kesho polisi wakija kusema ni kweli tulipewa jina la Pengo
na tulipochunguza tukaona hana hatia.....
hapo atasemaje????

halafu si ndo huyu Pengo aliesema mwisho wa dunia ni mwaka 2000?????
au hiyo nayo namsingizia?????
 
Suala sio kanisa kuhusika na madawa bali aliyetajwa ni yeye bwana Pengo,kwanini analiingiza kanisa?kama kuigonga serikali mbona viongozi wengi tu wadini akiwamemo kakobe,mzee wa upako,Rev,Mtikila n.k.mbona hawajatwa katajwa yeye,au huko katoliki kwanini wasimtaje kilaini na wengine katajwa yeye kama anavyodai maana sisi hiyo list hatujaiona so far zaidi ya kumsikia yeye akiweweseka!

Siko zote mimi huwa nasema PENGO is a disaster kwenye hii nchi,mbona akina mzee Rugambwa enzi zile hawakuipenda dunia kama yeye?halafu watanzania tusipende kutetea tetea tu hata pasipo kuwa na uhakika,pengo ni binadamu,kwani yule askofu aliyeshiriki mauaji ya kimbari rwanda ilikuwaje?si nae alikua anaheshimika kama huyu PENGO before na kila muumini alimpenda na kumuamini?lakini kilichokuja kutokea kila mtu alishangaa,lakini hatukuklihusisha kanisa lote kwa ujinga wa yule askofu,na hili la PENGO kamaa kweli katajwa kwenye madawa tuwaachie polisi wafanye kazi yao ya kuyathibitisha madai hayo kwani kutajwa tu hakumtii mtu hatiani,pengo amefanya pupa ya bure ambayo inamfanye aonekane anakosa usingizi baada y kujulikana kwa taarifa zake sasa anazitoa kabla hazijatolewa ili zikitolewa aseme mi nilisema kuna njama,huo ni ujanja wa kitoto!

Kumbe na wewe ni mtoto wa mama mdogo?
 
kweli akili ni nywele...lol
eti serikali ilazimishwe impeleke mahakamani...
wapi serikali imesema Pengo anachunguzwa?
si ni yeye mwenyewe anabwabwaja????

The Boss sikujua nawe ni muumini wa serikali yenye kutoa ultimatum kwa wavunja sheria (wezi bandarini, TRA, EPA, wauza unga).
Joka la kibisa??.....
 
Inawezekana Pengo kakumbuka maneno ya JM kikwete kuwa uwongo ukisemwa sana hugeuka uwa ukweli. So yeye kama kiongozi kama kasikia jina lake Pengo linatajwa tajwa lazima na muhimu atoe tamko.

Lisemwalo lipo ...kama halipo ...
 
The Boss sikujua nawe ni muumini wa serikali yenye kutoa ultimatum kwa wavunja sheria (wezi bandarini, TRA, EPA, wauza unga).
Joka la kibisa??.....

mkuu mimi hii serikali siipendi na naipinga kwa mengi mno....
na hapa utaona sitetei serikali bali napinga kiongozi wa dini
kutumia taasisi yake kuchochea vurugu....

siku zote tunapaswa kutetea sheria
ni bora siku zote sheria iheshimiwe..
hata kama ina mapungufu...
 
Inawezekana Pengo kakumbuka maneno ya JM kikwete kuwa uwongo ukisemwa sana hugeuka uwa ukweli. So yeye kama kiongozi kama kasikia jina lake Pengo linatajwa tajwa lazima na muhimu atoe tamko.

amesikia kwa nani?na kwanini kwa pengo tu ndio iwe issue lakini wale viongozi wa makanisa mengine tulikua kimya walipotatjwa rasmi,sio hizi he said she said za pengo?jamani hawa viongozi wadini ni binadamu hivyo yote yanaweza kuwa majibu,tusubiri,kwani tumesahau wale wa kupanda mbegu?na wao si walikua viongozi wa dini pia mbona waliburuzwa mahakamani japo kuna watu walijitokeza mwanzoni kuwatete kama nyie mnaojitokeza kumtetea pengo tena kwa jambo alilozua tu mwenyewe hata polisi hawajawahi kumwita kumhoji!
 
Suala sio kanisa kuhusika na madawa bali aliyetajwa ni yeye bwana Pengo,kwanini analiingiza kanisa?kama kuigonga serikali mbona viongozi wengi tu wadini akiwamemo kakobe,mzee wa upako,Rev,Mtikila n.k.mbona hawajatwa katajwa yeye,au huko katoliki kwanini wasimtaje kilaini na wengine katajwa yeye kama anavyodai maana sisi hiyo list hatujaiona so far zaidi ya kumsikia yeye akiweweseka!

Siko zote mimi huwa nasema PENGO is a disaster kwenye hii nchi,mbona akina mzee Rugambwa enzi zile hawakuipenda dunia kama yeye?halafu watanzania tusipende kutetea tetea tu hata pasipo kuwa na uhakika,pengo ni binadamu,kwani yule askofu aliyeshiriki mauaji ya kimbari rwanda ilikuwaje?si nae alikua anaheshimika kama huyu PENGO before na kila muumini alimpenda na kumuamini?lakini kilichokuja kutokea kila mtu alishangaa,lakini hatukuklihusisha kanisa lote kwa ujinga wa yule askofu,na hili la PENGO kamaa kweli katajwa kwenye madawa tuwaachie polisi wafanye kazi yao ya kuyathibitisha madai hayo kwani kutajwa tu hakumtii mtu hatiani,pengo amefanya pupa ya bure ambayo inamfanye aonekane anakosa usingizi baada y kujulikana kwa taarifa zake sasa anazitoa kabla hazijatolewa ili zikitolewa aseme mi nilisema kuna njama,huo ni ujanja wa kitoto!

toka hapa na pumba zako hapa

Kikwete na siasa zako za maji taka, nani hakujui ulivyo wapaka matope akina sumaye, mwandosya, salim ahmed salim who was the best president na fitina zako mpaka kesho zinakusuta

my president was salim ahmed salim sio ww muuza sura

pili unafiki wako tumeuchoka ulianza kusema kwenye baraza la maaskofu kuwa baadhi ya viongozi wa dini wana fanya biashara ya madawa! alafu ukaja kwenye baraza la idd dodoma ukasema mashekh na watoto wao wanafanya biashara ya madawa unajifanya msanii kwa kutufanyia michezo ya kuigiza

unavyombo vyote vya dola na wawajua wote kwa nini usiwakamate au ndio ya akina amina chifupa alivyotaka kuwataja ww na wenzio mkamuua binti wa watu kwa masumu yenu mliyowapa mwandosya na mwakyembe.

tumechoka na siasa za maji taka
 
kama hawana ushahidi wafanyaje?
waache kuchunguza?
hawawezi kwenda mahakama hawana ushahidi
hiyo haifanyi kuweka list ya watu wa kuchunguzwa kuwa ni kuonewa
tena na mtu anaejitangaza mwenyewe kuwa yupo kwenye orodha....

assume pengo kweli anafanya huu mchezo mchafu. Je anaweza kuwa anaufanya kwa maslahi yake binafsi au anaufanya kama mradi wa Kanisa?

Kama ni mradi wa Kanisa nataka nikuhakikishie Kanisa la RC kwa structure yake haliwezi kumtumia Pengo kuna watu na watumishi wengine wangetumika. Laini hili kama mkatoliki ningepnda kusikia japo kaitwa kuhojiwa. Kwanza Ziara anzofanya Pengo nje ya nchi ni chache sana. wa hiyo hata sisi wakatoliki tunapenda kujua Ni kanisa letu la tanzania linafanya hii biashara au ni "watu" ndani ya kanisa au ni vita ya wanasiasa fulani na kanisa la RC limeoneana ndio uwanja bora

Kama ni biashara yake binafsi na ni nje ya system ya Kanisa basi tungesikia wamenesawa wengine wengi amabao wangemtaja na vile vile vyombo husika vilitakiwa Kulifanyia kazi.
 
mkuu Fahari....
uliyoyaongea yoote ni point na ya maana
lakini yanakuwa hayana maana kwa sababu moja kubwa tu...
hakuna polisi wala serikali iliyosema Pengo anachunguzwa...
sasa uhalali wa wewe kusema yoote hayo hakuna
umeona hapo????
yeye kasema anapakaziwa...na serikali inaweza kesho kukanusha..likaishia hapo..
 
Watanzania tuko ndani ya mwaka mwingine ki-kalenda hivyo ni vema basi mambo yalokuwa ya kipuuzi tukayaacha kwa kalenda iliyopita,fikra na akili za kuku tuziache ingali mapema tarehe moja.
Ninachotaka kusema kama kweli nchi hii inawaogopa baadhi ya watu,haiwezi kuwachukulia hatua za kisheria tu eti nchi haitatulia basi ni kithibitisho tosha kwamba serikali ya CCM-Magamba ni legelege na wala haitufai jana,leo na kesho.kama kweli Kikwete anawajua wauza unga na kama kweli na Askofu Pengo yumo kwa nini hakutajwa na kukamatwa sawia?kwani kama kuna uthibitisho wa kutosha na kama mnavyosema Kikwete hakukurupuka kusema viongozi wa dini waache kuuza unga ina maana anayo list ya wauza unga akiwemo na Pengo kama inavyotaka tusadiki,kwanini asikamatwe,mnamuogopa wa nini?au ndo kuziba midomo wasiendelee kukemea maovu hasa ufisadi uliojenga mizizi ndani ya CCM na serikali yake?nasema hivi kama kweli polisi wana taarifa sahihi za Pengo na kama kweli JK alishapewa list hiyo na Pengo alitajwa basi naomba akamatwe na hii itasaidia sana kurudisha nyuma harakati za wakubwa na watu maarufu kujihusisha na biashara hii,vinginevyo tafakari yangu mimi ni kwamba kama wataogopa kumkamata Kadianali Pengo basi napata picha ya kwamba serikali nayo inauza madawa ya kulevya hivyo basi inaogopa kumkamata vile atawataja anaoshirikiana nao wakiwemo vigogo wa serikali hata hao kina JK na wenzake,siamini kama serkali itakuwa inatawala huku ikiwaogopa raia tena wachache eti kwa kuwa ni drug dealears au ni viongozi wetu wa dini,hii itakuwa serikali gani kama inamuogopa Pengo tena anafanya biashara haramu ambapo kuna nchi adhabu yake ni kunyongwa?vinginevyo nitaonisha na sakata la Richmond,EPA na mengineyo serikali imeshindwa kuwachukulia hatua wahusika maana hata yenyewe ilihusika kupitia mgongo wa chama tawala,na ndio maana hata EL hawawezi kumvua gamba kwa vile sakata la Richmond hata mkuu wa kaya yumo.basi na hili kama wana ushahidi Pengo ni dealer wamkamate vinginvyo na wao wanahusika wanahofu ya kutajwa
 
kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, sasa kama mtu anasimama kutetea drug dealers wanaotumia jina la kanisa kwa nini na yeye asiwemo kwenye list? wewe wadhani alihamishiwa kagera kwa mazuri? ni mengi yangelipuka kama angeendelea kaa hapa dsm. all in all, pengo aache unafiki, urafiki wake wa karibu na drug dealers watia mashaka. may be wote wanachonga michongo pamoja....who knows....? watu hawawezi just list him without knowing his involvement.

Kama sikosei umekosea wewe, unauhakika unayemuongelea ndiyo huyo unayemaanisha? Pls tafakari zaidi!
 
toka hapa na pumba zako hapa

f..k you kikwete na siasa zako za maji taka, nani hakujui ulivyo wapaka matope akina sumaye, mwandosya, salim ahmed salim who was the best president na fitina zako mpaka kesho zinakusuta

my president was salim ahmed salim sio ww muuza sura

pili unafiki wako tumeuchoka ulianza kusema kwenye baraza la maaskofu kuwa baadhi ya viongozi wa dini wana fanya biashara ya madawa! alafu ukaja kwenye baraza la idd dodoma ukasema mashekh na watoto wao wanafanya biashara ya madawa unajifanya msanii kwa kutufanyia michezo ya kuigiza

unavyombo vyote vya dola na wawajua wote kwa nini usiwakamate au ndio ya akina amina chifupa alivyotaka kuwataja ww na wenzio mkamuua binti wa watu kwa masumu yenu mliyowapa mwandosya na mwakyembe.

tumechoka na siasa za maji taka

Bwana masaburi unanitukana bure mi siko upande wowote ila sipendi kuona mtu akijaribu kutaka kuwauzuia polisi kufanya kazi zao ambazo sisi tax payer tunawalipa kuzifanya...tungependa kuona kodi zetu zinatumika vizuri,polisi wakikamilisha kazi zao huwa hawatoi hukumu,mzee pengo ikithibitika ataburuzwa mahakamani,na huko kuna haki,si uliona bwana zombe,wengi tulipenda afungwe au anyongwe akiwemo rais lakini kwa kuwa mahakama zetu ziko huru akapata haki yake...na hakuna aliye juu ya sheria hata pengo au mufti simba.
 
Michango ni mingi sana ila take this also. JK naye yupo kwenye list hiyo ya madawa ya KULEVYA. NAOMBA MICHANGO HAPA PIA.
 
hata sijakusoma mwanagu mwenyewe labda utoe ufafanuzi zaidi una maana gani

Dini zetu kuu ni uzao wa Ibrahim, kupitia watoto wake Isaka na ishmael, ishmael alikuwa mtoto wa mama mdogo, na kwa desturi watoto wa mama mdogo haweshi kulalamika, hata wapewe vyote.
 
Nani kakurupuka? Mimi au wewe? Soma uelewe nini kimendikwa siyo kukurupuka tu. Mimi wala gari analotumia Mhashamu Policarp Kadinali Pengo silijui. Mantiki ya post yangu ilikuwa kumdhihaki jamaa aliyejibu post yangu kuwa Vague. Mimi nikasema gari la kifahari? Nikiwa na maana hiyo vague alikuwa akimaanisha Vogue? Najue vague ni kwamba haieleweki nami nikajifanya sielewi! Wapi nimesema anatumia gari la kifahari? Acha kukurupuka na kujifanya wewe ndio mkatoliki namba one. Mimi mwenzio ni mwenyekiti wa baraza la walei parokiani kwangu.

Binafsi nilikuelewa sana..na nimeshangaa kuona gari ya kifahari ya pengo..jamani Polycarp Pengo anatumia escudo na anaendeshwa na dada yangu mimi sista wa wadada wadogo...nimekua puzzled kusikia sijui gari ya kifahari..anyways..happy new year

.......halafu si ndo huyu Pengo aliesema mwisho wa dunia ni mwaka 2000?????
au hiyo nayo namsingizia?????
Huyo nina hakika 99.999% sio Pengo. Kanisa la RC haliendi kwa mafundisho ya UTABIRI TABIRI tena ya mauda specific
 
Huyo nina hakika 99.999% sio Pengo. Kanisa la RC haliendi kwa mafundisho ya UTABIRI TABIRI tena ya mauda specific

tuliache hili tusiharibu thread hii
nikishapata ushahidi nitalifungulia thread na kuku notify
sawa?
 
Bila kujali ni kweli au si kweli pia ikumbukwe kwamba Pengo nae hajakurupuka kusema hivyo na kanisa katoliki lilivyo anataarifa zote kuhusu kinachoendelea na hata kama ni kweli ni dealer lakini kutajwa kwake kumetokana na washirika wa biashara hiyo wakiwemo wanavitengo wenyewe na ndio maana binafsi nataka nione kitendo ndipo nitaamini,tena kitendo cha kumkamata na kumhoji na kwa kutumia ushahidi waliokwisha ukusanya apelekwe mahakamani,wakishindwa basi mjue ya kwamba anapakaziwa ili kumziba mdomo asiendelee kukemea ufisadi na uroho wa madaraka hasa mbio za urais za 2015
 
Michango ni mingi sana ila take this also. JK naye yupo kwenye list hiyo ya madawa ya KULEVYA. NAOMBA MICHANGO HAPA PIA.

Na yeye jk kasema "Mimi mwenyewe nimewekwa katika orodha ya dawa za kulevya"?
 
Back
Top Bottom