Huu mjadala ni mfu, Pengo kaisha sema sasa mijadala ni ya nini?
you are right .... sio kila kitu lazima kijadiliwe!!Sioni mantiki ya kujadili statement yake
Huu mjadala ni mfu, Pengo kaisha sema sasa mijadala ni ya nini?
Sasa hii inamaanisha kwamba ni amri ya kupiga vita maovu?
Hiyo ilishabadilishwa na mengi yameandikwa kwamba sheria does not count anymore.
Romans 10:4 Christ is the end of the law so that there may be righteousness for everyone who believes.
Kama unaaamini tafsiri yangu sio sahihi nijulishe nilete ushahidi wa tafsiri niliyoitaja kwa mujibu wa wahubiri wenyewe.
Asante kwa changamoto.
Labda kwanza nianze kwa kukuomba ulete quote ya hapo niliposema waraka unatishia amani.
Nirudie tena msingi wa hoja yangu.
Mtu anaweza kuzungumza katika capacity tofauti. Angekuwa amezungumza kama Raia wa kawaida hapo angekuwa Raia kasema kama vile wewe, mimi, mwanasiasa na kadhalika.
lakini hapo kazungumza kama Kiongozi wa kanisa. Ninahoji, je aliyoyasema anaweza kuya support na maandishi?Nimeuliza wapi ameamriwa kupiga vita yale anayoyaona ni maovu.
Kama hana ulazima wa kuamriwa ili apige vita maovu kama walivyoashiria wengine pia haina tatizo, ili mradi 'isemwe wazi' kwamba maelekezo na mafundisho ya anayoyasema kama Kiongozi wa kanisa hayana ulazima wa kuwa supported na maandishi yake matakatifu. Kwa maana nyingine imani zake zinampa mamlaka ya kusema lolote hata kama anachosema hakina mwongozo huo ndani ya vitabu vyake.
Sina tatizo na content za waraka, nina question process and scope of what he can say and cannot say in his offcial capacity.
Angekuwa Rais tungesema katiba inamdhibiti. Kama Kiongozi wa Kanisa ni kipi kinachodhibiti matamshi yake?
Ona miafrika. Badala ya kujadili "uozo wa nchi" yenyewe inamjadili aliyeanzisha mada, haki zake na dini yake.
Halafu tunashangaa kwanini hatuendelei?
- Asema Katoliki haliandai mgombea Urais mwaka 2010.
- Adai anayeogopa waraka wa Kanisa ni Fisadi.
Nadhani watu wengi wasichokielewa ni kwamba hauwezi kuwaongoza nakuwajenga watu wawe imara kiroho hili khali kimwili wamedhoofika. Miminadhani kutenganisha dini na siasa ni kutoruhusu masuara ya kisiasa kuamuliwa na kuongozwa kwa misingi ya dini.Mkuu ni kweli kuna separation ya politics na religious matters. Sina hakika kama maana yako ya Church and State, ina maana Mosque yenyewe haiwi separated na state matters, which in many cases it may seems so.
Lakini where do you draw that line. Mambo ya dini yanaishia wapi na ya siasa yanaingia wapi, ukiangalia kwa undani utaona kuwa ni mstari ambao umechorwa hewani tu. Sioni ubaya kwa kiongozi wa msikiti au kanisa kusema hatutaki viongozi wabovu, mtu akiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa, diwani, mbunge,waziri au rais anaongoza watu wote bila kujali yeye ni mwanadini au la. Kwa hiyo kama uongozi wake haufai unamwathiri moja kwa moja hata mtu wa dini. Kama serikali inalinda na kupalilia maovu, misikiti na makanisa yatakuwa yanafanya kazi bure, yaani kufinidhs amorals wengine wanafanya tofauti. Wakati wao misikitini na makanisani wanapreach honesty, itakuwa ni upuuzi kama watachekelea ufisadi.
Makamba most of the time amekuwa akiquote Qoran na Biblia anapokuwa kwenye kazi za siasa. Alipokuwa RC hata alikuwa anakwenda misikitini kama RC, kumbuka mwembechai au pale kwa mtoro wakati wanachapana bakora ndani. Mbona yeye hakuwahi kukosolewa kuwa anachanganya siasa na dini?
Are we being hypocritical, or is our system hypocritical? Why should politicians mix politics and religion and why shouldn't clergymen mix religion and politics. Inawezekana Pengo hajui kama dini na siasa haviwezi kuchanganywa?
Muadhama Cardinal Polycarp Pengo ... tuna separation of church and state ... remember?
Waumini wanaruhusiwa kisheria kuwa kwenye chama chochote cha siasa kikatiba...sasa pengo kama anataka siasa aanzishe "christian party" asajili halafu aombe kura kwamba chma chake hakita vumilia mafisadi tutampa na kumpima..Kwa sababu hiyo, waumini wake waachane na siasa na wasishiriki uchaguzi any more?? OK
.Nafikiri sasa serekali imefika wakati wa kumshuhulikia huyu Polycarp Kardinali Pengo,ni lazima achunge sana hii sio serekali ya kuchezea ipo kihalali na imechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi kwa ushindi mkubwa.
Acha kubwabwaja wewe....serikali ipo kwa ridhaa ipi ya wananchi?,,tatizo hamtaki kuambiwa ukweli....utashughlikiwa wewe na siyo PengoNafikiri sasa serekali imefika wakati wa kumshuhulikia huyu Polycarp Kardinali Pengo,ni lazima achunge sana hii sio serekali ya kuchezea ipo kihalali na imechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi kwa ushindi mkubwa.