Pengo amtolea uvivu Kikwete

Rais Kikwete alitumia jukwaa/mimbari ya Kanisa Katoliki kutamka maneno yake. Maaskofu wake hawakimjibu hadi mwezi huu. Kiimani hata kimaadili Kanisa limekwazika kama dhambi nyingine inayotafuna WTZ wote ya UFISADI hata kama hukushiriki.

Inaumiza, Mkuu wa Dini anachomwomba JK awe jasiri awataje wahusika ili washughilikiwe kama wale mapadre walawiti. Vinginevyo tamko lake la jumla litamgharimu kwa kutengeneza chuki isiyo ya lazima kama alidhani msg sent but at a wrong place space and time. Ukatoliki thabiti unatafuta kusimamia kwenye ukweli na haki.

Bravo Askofu Card Pengo.
 
Haya sasa tunasubiri tamko toka BAKWATA. Tuone upande wa pili nao wanasemaje kuhusu jambo hili.?
WALA USISUBIRI BAKWATA. FUNGULIA REDIO KHERI 104.20Mhz LEO JMAPILI SAA TATU NA NUSU USIKU YUKO SHEIKH BASSALLEH ATASEMA SANA KUWA MAASKOFU WANAINGILIA SIASA. PILI CHANNEL TEN LEO USIKU YUKO SHEIKH SAID NI MSEMAJI WA JK HATAKOSA KUMSEMEA JK.
 
Kuna MwanaJF mmoja aliwahikuwasema humu Jamvi kuwa Ni Bora Kikwete akiwa nje ya nchi kuliko akiwa ndani ya nchi anatoa maneno ya Kukejeli, Kuudhi na ya kijingajinga anaropoka hovyo kama vile hakuwahi kumaliza Shule. Nimeamini kuwa Kikwete akiwa nje ya Tanzania, Watanzania wanakuwa na uafadhali kuliko akiwa ndani.

Kwanini tusimtoeni kwa Nguvu ya Umma, ni kitu gani kinashindikana? Watanzania wenzangu muda wa kuchukuwa hatua umefika mambo mengine sio ya kuyafumbia Macho lazima tusimame na nchi yetu
umtoe nani? Rais Kikwete? Thubutu. you will see na uzezeta wako huo.
 
Hakuna chochote kinacho msumbua huyo mnafiki zaidi ya kununa, nchi hii imepitia mambo mangapi makubwa kabla kanisa lake halijaingia kwenye kampeni za Slaa lakini hakuwahi kuongea kitu lakini tokea huyo padri mwenzake ameshindwa uchaguzi basi ni nongwa tu kila kukicha. Narudia tena Pengo na wenzake wa TEC na wengine wooote waliokuwa wapiga kampeni wa Slaa wamenuna tu ndio kinacho wasumbua, na salamu zao wataendelea kunua hadi 2015 labda wakaze buti kwenye hizo mbinu zao za kupindua serikali halali.
.
Mtu yeyote ambaye ni dhaifu wa hoja utamgundua mapema sana, hata katika mambo yanayohitaji analysis utamuona anakuja na majumuisho ambayo hata collection yake haikufanyika....

Kama una hamu ya kulichafua kanisa, ni vizuri ukajipa muda wa kulitafiti na kulifahamu vizuri, vingenevyo kila unachoongea hapa kitakuwa kinakudunisha mbele ya wasomaji uwaandikiao.

Elewa kuwa kanisa halijanuna ndiyo maana hata sasa linaendelea kusaidiana na serikali katika kuwahudumia watanzania katika nyanja za kiroho, afya,elimu uchumi n.k Jiulize kuhusu hao unaodhani ndiyo wamefurahishwa na ushindi wamefanya nini katika kuisaidia serikali mpaka sasa zaidi ya kuomba upendeleo kweny nafasi mbalimbali (viti maalum- kwa vigezo vya dini)?.

Fungua akili, usifinye uwezo wako kutafakari na kuacha, kinywa, akili, na moyo wako vikiwa vimatawaliwa na mapenzi yanayokufanya ushindwe kuuona na kuutambua ukweli. Huko uendako, utaikana jinsia yako, sijui baada ya hapo kitafuata nini.

Yote uyaongeayo yanakufanikisha katika kuonekana kuwa wewe ni ant-society.
 
Huyu si ni member wa mafiaso wa Sicily Italy? Lazima atakuwa anahusika na biashara ya unga!
 
Hakuna chochote kinacho msumbua huyo mnafiki zaidi ya kununa, nchi hii imepitia mambo mangapi makubwa kabla kanisa lake halijaingia kwenye kampeni za Slaa lakini hakuwahi kuongea kitu lakini tokea huyo padri mwenzake ameshindwa uchaguzi basi ni nongwa tu kila kukicha. Narudia tena Pengo na wenzake wa TEC na wengine wooote waliokuwa wapiga kampeni wa Slaa wamenuna tu ndio kinacho wasumbua, na salamu zao wataendelea kunua hadi 2015 labda wakaze buti kwenye hizo mbinu zao za kupindua serikali halali.
mkuu kwenye highlight hapo nadhani umekosea. Hakuna kumtoa mtu hapa mpaka 2015. huo umma wanaouongelea ni upande mwingine. geuza pia upande wa pili wa shilingi, kuna bonge la umma. huo hauogopi chochote na hauna cha kupoteza. huo umma wanaouongelea si kwa wanao peke yako, Hata JK alishasema wanasema nguvu ya umma as if huo umma wanao peke yao. Wasifikiri nchi itatawalika. Thubutu. waendelee tu hukuhuku kwenye net tu na si kule uraiani. Full stop.
 
Huyu si ni member wa mafiaso wa Sicily Italy? Lazima atakuwa anahusika na biashara ya unga!
Safi sana......watu wa aina yako ndiyo wale ambao wakitua tu pale Hollywoodland inakuwa ni vituko tu, kwani kila mzungu mzee na mwanaume wanayekutana naye wandhani ni Chuck Norris....wanaanza kumsumbua eti wapige naye picha ya ukumbusho.
 
jamani mimi ni mwisilam safi ila kwa hili jambo la kitaifa nauweka uislam wangu pembeni na ninaungana na pengo, jk ni msaliti na anatumia uislam wetu kutujengea chuki akishirikiana na baadhi ya mashekhe uchwara kuandaa midahalo msikitini na kuwahadaa na kuwajengea chuki watoto wa sekondari na jamii kwa ujumla dhidi ya wakiristo jamani huku tuendako ni kubaya sana shauri yenu mimi yangu macho
 
Halafu kitu ambacho kimewaudhi sana wakristo ni kwamba jk alisema baadhi ya viongozi wa dini wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya. baadae wanasema alimaanisha makanisa madogo. maana yake viongozi wa dini alimaanisha wakristo ndio maana akawa specific kuwa ni makanisa madogo. waislamu na dini nyingine wao rais anasema ni watakatifu hawahusiki
 
Pengo unatakiwa useme hivi CCM nchi imewashinda basi!Kikwete hakiondoka ndio CCM itakuwa nzuri?
 
Naomba niongezee kwa DSN kuwa umefika wakati sasa viongozi wa dini hasa wa Kikristo wa makanisa yanayoeleweka sio yale yanu ayotumiwa nafikiri umma unshajua vikundi na watu waliojipachika uaskofu kumbe ni mamluki kuacha kumwalika Kikwete kwenye sherehe zao za kidini. Nalisema hili kwa sababu huyu ni mtu asiyekuwa na staha kwenye kwa kila anachokisema ndio maana anattumia masaa na masaa kuongea lakini anaishia kutoa lugha za taarabu.

Wanaomtetea kuhusu tamko la madawa ya kulenya kulitoa mbele ya waumini wa kanisa Katholiki na viongozi wao toka pande zote za nchi halikuwa sahii na hapakuewa mahali pake. Kama aliona ni vyema kutoa tahadhali kuhusu viongozi wa dini wanaoijhusisha na biashara haramu hiyo angewaalika wawakilishi wa viongozi wa dini zote na kutoa tamko au angesema wakati wa vipindi ambavyo anahutubia Taifa.

Halafu biasha hii ni haramu ikafanywa na mtu yeyote. Kama kuna viongozi wanafanya hivyo wahukumiwe kama wao na sio taasisi wanazoziongoza kupakwa matope. Kauli ya Kikwete ilikuwa inakera na sasa Maaskofu wetu, mapdri, wachungaji, masista na wengine wenye daraja katika Makanisa makini umefika wakati msimhusishe mtu katika sherehe zenu.

Inaonekana anapokuja anakuwa anawakoga tu maana hathathmini wala haeshimu mnachokuwa mnakifanya kuwa ni cha ibada. Kama angetambua hilo asingesema kama alivyiosema siku ya kuwekwa wakfu baba askofu. Sherehe nzima na dhana nzima aliitia doa, kanisa kalitia doa na ni wakati mwafaka kumwonyesha yeye na nchia nzima na dunia nzima kuwa makanisa hajajapenda kauli ile. Na ajue kuwa na sisi wananchi hatujapenda na ukimya wetu asiuone kama ujinga.

Nimpongeze Baba Askofu Cardinal Pengo kwa usahii na umakini wa kauli yake isiyokuwa na chembe ya unafiki. Nimwombe aendelee kukemea watu wenye undimilo kuwili kama wa JK. Nitoe rai kwa viongozi wengine wafuate nyayo za Baba Pengo na CCT
 
Hivi JK alitamka "Maaskofu" kwenye ile hotuba au alisema baadhi ya "Viongozi wa dini"?...
 
umtoe nani? Rais Kikwete? Thubutu. you will see na uzezeta wako huo.

Uzezeta wako ndio unaiofanya hii nchi iibiwe na wewe upo bila kuuliza umekuwa zezeta Subiria Kikwete tutkapo Muondoa Madarakani na Ufisadi wenu utakuwa ndio Mwisho
 
Halafu kitu ambacho kimewaudhi sana wakristo ni kwamba jk alisema baadhi ya viongozi wa dini wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya. baadae wanasema alimaanisha makanisa madogo. maana yake viongozi wa dini alimaanisha wakristo ndio maana akawa specific kuwa ni makanisa madogo. waislamu na dini nyingine wao rais anasema ni watakatifu hawahusiki
.
Mkuu labda nikukumbushe kidogo...Hukusema "baadhi ya viongozi wa dini", alisema "viongozi wa dini"
 
kwanza msamehe, pili mchukulie kama alivyo, tuseme alikosa cha kuongea hivyo akalopoka tu aonekane kasema chochote... mwisho tumwombee kwani amesahau kuongea ni vizuri lakini kukaa kimya ni vizuri zaidi...
 
Haya sasa tunasubiri tamko toka BAKWATA. Tuone upande wa pili nao wanasemaje kuhusu jambo hili.?
bakwata huku hakuna kauli kwa kuwa hatuhusiki na biashara ya madawa ya kulevya, wewe ukimuona mtu anajibu na anatoa kauli za kashfa kwa Rais juwa anahusika, Rais amegusa maslahi yao, na kama kutajwa wameishwa tajwa tunawajua, tunawafahamu.
 
mkuu kwenye highlight hapo nadhani umekosea. Hakuna kumtoa mtu hapa mpaka 2015. huo umma wanaouongelea ni upande mwingine. geuza pia upande wa pili wa shilingi, kuna bonge la umma. huo hauogopi chochote na hauna cha kupoteza. huo umma wanaouongelea si kwa wanao peke yako, Hata JK alishasema wanasema nguvu ya umma as if huo umma wanao peke yao. Wasifikiri nchi itatawalika. Thubutu. waendelee tu hukuhuku kwenye net tu na si kule uraiani. Full stop.
Hapo kwenye red I can imagine....! kama mtu kutwa nzima unacheza bao au unashinda kwenye nyumba ya ibada kweli hautakuwa na cha kupoteza!! Ila ipo siku itafika hata nyinyi mtasema basi..liwalo na liwe..kwa sababu kikwete anafikiri kwa kutumia masaburi!
 
bakwata huku hakuna kauli kwa kuwa hatuhusiki na biashara ya madawa ya kulevya, wewe ukimuona mtu anajibu na anatoa kauli za kashfa kwa Rais juwa anahusika, Rais amegusa maslahi yao, na kama kutajwa wameishwa tajwa tunawajua, tunawafahamu.

.............Anajibu na anatoa kauli za kashfa kwa rais? Kwa hiyo unamaanisha kuwa mheshimiwa rais aliongea kashfa tu. na si kitu halisi?
Pia huoni muda na misuri ambayo serikali inatumia ili kunyoosha mambo? Serikali imetambua kuwa ilifanya makosa ndiyo maana imetafuta maseremala wa kunyoosha nyoosha maneno ili yanyooke (rejea kauli ya pinda bungeni kuhusiana na sakata hili).
Tubishane katika misingi ya kujengana na wala si kwa misingi ya kuongeza ufa kati yetu.....
 
Back
Top Bottom