PENDO MAGALUDA Ametutoka

Status
Not open for further replies.
Ndugu wa-Tanzania wenzangu wote, hasa wa mji wa New York ninapenda kutoa shukrani zangu nzito sana kwa wananchi wote tuliokusanyika juzi Jumatano jioni kwa ndugu yetu William Malecela na kutoa heshima zetu za mwisho na kumfariji na kumuaga Ndugu yetu Abel Magaluda na watoto wake, aliyefiwa na mkewe Pendo Magaluda, wiki iliyopita huko Rochester Upstate New York, pamoja na kwamba ilikuwa ni notice ya masaaa 12 tu, lakini heshima mbele kwa wananchi wote mliojitokeza kwa wingi.

- Kama mshiriki wa shughuli hiyo, ninapneda kutoa shukrani nzito sana kwa Mheshimiwa Dr. Asha-Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa UN kwa kujitokeza kwake kuja kujiunga nasi wananchi wenziwe kumfariji ndugu yetu na watoto wake. Wananchi tuliokuwepo tumefarijika sana na ushirikiano na upendo wake aliounyesha katika kipindi kizima cha mauguzi ya marehemu Mpendwa Pendo, mpaka dakika ya mwisho ya kuuga mwili wa marehemu na kuwafariji wafiwa.

- Naomba pia kutoa shukrani za dhati kwa Balozi wetu wa Tanzania katika Umoja wa Taifa, DR. Augustine Mahiga pia kwa ushirkiano mkubwa sana yeye na ofisi yake waliouonyesha katika kipindi hiki kizima kigumu cha mauguzi ya marehemu. Naomba kumshukuru pia kwa kujitokeza kujumuika nasi wananchi wenzake katika kuwafariji na kuwaaga ndugu zetu Abel na familia yake.

- Naomba niwape heshima kubwa sana maofisa wote waUbalozi wetu New York, kwa kutoka nje ya mstari wa shughuli zao nzito za kutuwakilisha taifa kwenye Umoja wa mataifa na kushirikiana nasi wananchi wenzao na kumsaidia kwa hali na mali katika kipindi chote cha mauguzi ya marehemu, mpaka dakika ya mwisho ya kugana na ndugu zetu hawa wafiwa.

(a). Dada Rose Mkapa, naomba nikutaje kwa jina, maana ulioyafanya ni makubwa sana na utalipiwa na Mungu tu, Dada Joyce Kafanabo Mungu akuzidishie kwa mchango wako mzito sana, Ndugu Mello (HOC) tafadhali pokea heshima zangu na za wananchi wanzangu kwa ushirkiano wako, Dada Tully Malecela utalipwa na Mungu tu uliyofanya, Dada Hellen Maduhu ubarikiwe tu,

(b). Again maofisa wote wa Ubalozi huu na wafanayakazi wengine wote mbarikiwe sana na Mungu wa Mbinguni.

- Ndugu Amos Shindika na Mkulu William Malecela, pia mbarikiwe kwa kazi na msaaada mzito mlioutoa kwa familia ya marehemu mpaka kuweza kumuingiza kwenye ndege ili aweze kuufikisha mwili wa marehemu nyumbani kwao Mwanza, mtalipwa na Mungu wa miujiza tu.

- Ndugu wa-Tanzania wote mliohudhuria kwa faraja na mali, wote mbarikiwe 1. Bwana Fundi Ramadhani, ahsante sana kwa kuweza kutangaza kwa wananchi na kwa muda mfupi lakini uliweza kuwafikia wananchi wengi sana, kupitia kwa mtandao wake wa fundirkombo.blogpost.com ubarikiwe mkuu.

- Ndugu zangu wa-Tanzania wote mliojitokeza kwa wingi naomba mbarikiwe sana na muendelee na moyo huu huu wa kusaidiana wakati wa shida na wakati wa raha, sisi wote ni ndugu wamoja na tuko pamoja katika kujaribu kuishi kwa amani na uelewano na mshikamano, tabia tuliyofundishwa na Mwalimu baba wa taifa letu na wazazi wetu pia. Michango yenu ilikuwa mizito sana na iliweza kusaidia kufanikisha mambo mengi sana katika safari ya ndugu zetu.

- Ndugu zangu wana-JF mliojitolea kwa hali na mali kutikia wito, pia mbarikiwe sana. Ndugu yetu Abel na familia yake na mwili wa marehemu, walifika hapa nyumbani Tanzania, yaani Dar-es salaaam leo mchana kueleka nyumbani kwao Mbezi, wakijitayarisha na safari ya kuelekea Mwanza kuupumzihsa mwili wa marehemu.

Respect - Wenu

Field Marshall Es.
 
mkuu Fmes,
Mie naomba nikushukuru na wewe binafsi,kwa kuweza kusaidia ukusanyaji wa michango..hasa jitihada zako za kuandika suala hili hapa..
Mchana huu ndio mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda mwanza..

Asubuhi ya leo watu wamekuwa wakitoa heshima za mwisho maeneo ya Tegeta ununio.Mjomba kaniambia kuna simanzi ya khali ya juu..

Tuendelee kuombea familia hii
 
mkuu Fmes,
Mie naomba nikushukuru na wewe binafsi,kwa kuweza kusaidia ukusanyaji wa michango..hasa jitihada zako za kuandika suala hili hapa..
Mchana huu ndio mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda mwanza..

Asubuhi ya leo watu wamekuwa wakitoa heshima za mwisho maeneo ya Tegeta ununio.Mjomba kaniambia kuna simanzi ya khali ya juu..

Tuendelee kuombea familia hii
It pains kwa kweli dada Pendo nilimfahamu huyu dada ingawa mimi nilikuwa mdogo sana wakati baba yao akiwa Dr pale KO hospital then wakahamia mkula then mwanza mjini !inauma sana kwa kweli!Tangulia Dada Pendo naamini umetutoka katika bwana naamini ulikuwa mcha MUNGU nilikuwa nakuona pale AIC MAGOMENI!
it pains a lot
 
mkuu Fmes,
Mie naomba nikushukuru na wewe binafsi,kwa kuweza kusaidia ukusanyaji wa michango..hasa jitihada zako za kuandika suala hili hapa..
Mchana huu ndio mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda mwanza..

Asubuhi ya leo watu wamekuwa wakitoa heshima za mwisho maeneo ya Tegeta ununio.Mjomba kaniambia kuna simanzi ya khali ya juu..

Tuendelee kuombea familia hii

- Mkulu Gembe, tupo pamoja na pia naomba kuwashukuru kuna niliowasahau yaani tulioshirikiana nao majuzi usiku kwa kuwataja majina yao,

- Nao ni Balozi Manongi na Dada Maura Mwingira, naomba pia kuwashukuru sana kwa juhudi zao nzito sana katika kushiriki kumuuguza marehemu na hata kufikia majuzi kwenye kuwafariji na kuwaaga ndugu zaetu na mwili wa marehemu.

- Mkulu Gembe, ni wananchi kunazia hapa JF, mpaka huko mitaani ndio waliofanikisha sana hii shughuli ya kusaidiana kwa hali na mali, unajua hakuna wakati nina proud to be Tanzanian kama nyakati kama hizi za matatizo, ninakushukuru kwa taarifa za kwanza za kifo, na ubarikiwe pia mkuu, tupo pamoja katika taifa.

Respect!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom