Pendekezo: Tanzania iweke Balozi Uholanzi!

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti leo kuwa Tanzania imeamua kufunga ubalozi wake nchini Uholanzi sio tuu kutokana na hali ya uchumi bali pia "conflict of interests" kati ya Uholanzi na Tanzania huku Uholanzi ikijikita zaidi kwenye uwekezaji na biashara. Nimesoma taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje lakini haijazungumizia kama ubalozi wetu nchini Uholanzi haujafungwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen: "It is obvious that there was a deterioration of the diplomatic relationship between Tanzania and Holland," said Mr Haule. "We decided to close our office after our colleagues concentrated on protecting their investors and businessmen in the country. Tanzania did not get what it wanted."

All is not lost, though, as the government still owns a house in Holland, which is in the care of the honorary consul. "Our house in Holland brings at least 8,040 Euros to the government every year and, at the moment, we have a honorary consul officer who reports to our embassy office in Brussels," he explained.

Source: Cash crisis hits Foreign ministry

Bit by bit we loose friends who were keeping us busy with visits to the extent that we forgot our own voters. Happy valentine anyway!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Tanzania hatukuwahi kuwa na balozi uholanzi ila tuna balozi wa heshima mr Henkbeg ambae 2010 alikutwa na kashfa ya kuingiza wazungu mbuga ya serengeti bila ya kulipia ila alikuwa anatumia kibali chake ubalozi wa heshima, mpaka alipoondoka DG wa Tanapa Mr bigurube ndipo waliokaibu ofisi wakambaini huyu bwana na utapeli wake na kama skosei yupo serengeti hivi tunavyo jadili.Hivyo yote hayo ni kutokana nahaliu halisi ya nchi tu wazembe kiasi fulani.
 
waambie mkuu,

Nafikiri hiyo hali si kwa sababu ya viongozi kuna ugonjwa fulani, ndiyo maana mie kwa miono yangu naona wtz wengi tunaugonjwa fulani.

Mfano
Mie nikienda pale kariakoo na mke wangu , pesa na toa mimi na pesa mie ndiyo nampa mwanamke, lakini wote huwa wana ni bypass wanakilimbilia kwa mwanamke wakiniona sifai kujadili nao kuhusu tunachotaka kununua, kwa sababu tu mwanamke ana rangi nyeupe na pua yake nyembemba ndefu sio pana kama yangu.
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti leo kuwa Tanzania imeamua kufunga ubalozi wake nchini Uholanzi sio tuu kutokana na hali ya uchumi bali pia "conflict of interests" kati ya Uholanzi na Tanzania huku Uholanzi ikijikita zaidi kwenye uwekezaji na biashara. Nimesoma taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje lakini haijazungumizia kama ubalozi wetu nchini Uholanzi

All is not lost, though, as the government still owns a house in Holland, which is in the care of the honorary consul. "Our house in Holland brings at least 8,040 Euros to the government every year and, at the moment, we have a honorary consul officer who reports to our embassy office in Brussels," he explained.

Source: Cash crisis hits Foreign ministry

Huu wizi yaani jengo letu holand tunaingizaa euro 8'000 kwa mwaka au kwa mwezi? Inaonekana kuna watu wanafanya ufisadi na nyumba za serikali nje ya nchi
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti leo kuwa Tanzania imeamua kufunga ubalozi wake nchini Uholanzi sio tuu kutokana na hali ya uchumi bali pia "conflict of interests" kati ya Uholanzi na Tanzania huku Uholanzi ikijikita zaidi kwenye uwekezaji na biashara. Nimesoma taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje lakini haijazungumizia kama ubalozi wetu nchini Uholanzi haujafungwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen: "It is obvious that there was a deterioration of the diplomatic relationship between Tanzania and Holland," said Mr Haule. "We decided to close our office after our colleagues concentrated on protecting their investors and businessmen in the country. Tanzania did not get what it wanted."

All is not lost, though, as the government still owns a house in Holland, which is in the care of the honorary consul. "Our house in Holland brings at least 8,040 Euros to the government every year and, at the moment, we have a honorary consul officer who reports to our embassy office in Brussels," he explained.

Source: Cash crisis hits Foreign ministry

Mimi sielewi kidogo hapa kwamba amebaki consular wetu hapo halafu nyumba inaingiza mapato, je ni kwamba consul wetu ana kichumba kimoja tu - ukute stoo - na vingine wamepangisha? Haya ndio mambo ya Bw. Mwembe au Mende?
 
Barua ya kwazi kwako Ndugu JK rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Nchi tajiri sana Duniani ina mbunga kibaoo, maziwa yenye kutoa samaki hadi Sauper akaja kupatia jina huko,Nchi yenye watu wavumilivu sana na wanaopenda lakini Serikali muda wote ina waangusha lakini hawakati tamaa.

Nchi yenye kuongozwa na watemi na wenye kauli jeuri kama Kalamagi lakini ndugu rais yuko kimya , Nchi inayo sadikiwa kuwa na makaa ya mawe, gesi, mafuta, urenium,madini ya kutengeneza meli, madini kibao , maua nk .

Pamoja na mambo hayo hapo juu bado tunasoma na kusikia toka kwa wakuu walioko chini yako nikiwa na maana ya mawaziri nk kwamba bajeti yetu 50% inagharamiwa na wazungu .Mali tunazao , akili tunazo na uwezo wa kuzifanya mali zetu ziwe msingi imara wa kulambwa na kubembelezwa Duniani hakuna .

Serikalio ya Uholanzi iko kwenye Umoja wa EU lakini kama serikali imekuwa kati ya Nchi marafiki wakubwa sana wa Tanzania kwa hila hali . Wanamwaga mapesa , yao kwa mikopo na hata misaada sawa , wamekuja kuwekeza kwa wingi sana Tanzania na sasa wako watu wao ambao wanafanya biashara na hasa utalii bila ya vibali na hawalipi kodi .

Hili nitaliacha kwa sasa ila nitalisemea pengine .Waholanzi kwa siku za karibuni wamekuwa marafiki wa karibu kuanzia kutoa mafasi za masomo kwa Watanzania kwa ngazi za Masitatz(Masters) na diploma na hata PhD na mengine mengi lakini ndugu Rais hujawahin kufika kwao kujitambulisha .Sijui labda wewe mkuu una sababu yako lakini bado najiuliza sana .

Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na ukaribu wote bado hakuna Ubalozi wa Tanzania Uholanzi.Balozi wetu wa Ubeligiji sina uhakika kama kapata kibali sasa kuja hata kuwatembelea Watanzania wa Uholanzi maana nakumbuka kwaba hata ndugu Mkapa anaenda mwaka jana kuaga Uholanzi balozi alienda kwa special permit .Uone mambo haya na kwa miaka kama 2 sasa tangia awe balozi pale Ubeligiji.

Tuna mtu anaitwa Hakkenburg ni mdachi huyu ambaye kwa kweli ni business minded .Hana habari na watanzania na mambo yake hayaeleweki . Ndugu Mkapa alisema siku ile ya kuagana na Watanzania wa Uholanzi kwamba kwenye handouts zake atakueleza juu ya umuhimu wa kuwa na Ubalozi Uholanzi je umepata ujumbe ule ? Ama bado kuna kubana matumizi hata mahala pale ambapo tunapata faida ?

Ubalozi wa Tanzania ama ofisi ya Konshula Uholanzi iko ofisini kwa huu mwakilishi wa watanzania Mzungu.Hatumbagui lakini pia kwenye habari zake wapi pa kumpata mara ya mwisho niliona kwamba anapatikana The Hague lakini ukweli ni kwamba anapatikana kwenye kijipori fulani ukipita kwenye highway utaona bendera ya TZ imepauka haishuki wala kupanda ilisha panda basi , hakufikiki bila ya taxi ama personal vehicle . Ndugu rais tafadhali fikiria hili ili ulipatie jibu ka Nchi hapa kama kana kuwa msaada mkubwa namna hii kwa Tanzania kwa nini basi tusipate Ubalozi na kuhudumiwa na Mtanzania badala ya sasa ilivyo shida kubwa hata ya kumpata mwakilishi wetu ?

Naomba chonde chonde ulikuwa mkuu wa mambo ya nje unajua vyema kuliko mimi sasa litupie macho hili .

Mimi Mtanzania mwenzio

Mugishagwe Mwana wa Majimoto
JF enzi hizo
 
Back
Top Bottom