Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.


Nakusahihisha kama ifuatavyo, Prof. Lipumba awe mgombea wa CUF na si wa Upinzani.

Ili CUF ichukue jimbo.
 
Wakuu tukiacha itikadi, CUF wana nguvu Igunga Kuliko CDM

Matokeo ya Mwaka Jana

Igunga

Msimamizi wa jimbo hilo Protas Magayane alimtangaza Rostam Aziz wa CCM kuwa mshindi wa kiti cha ubunge baada ya kupata kura 35,674 dhidi ya mpinzani wake, Leopord Lucas Mahma wa CUF ambaye amepata kura 11,321. kwa maana hiyo CDM walikwa wa 3

Ni kweli mkuu, si kwa jimbo la Igunga tu hata katika majimbo mengine kama Sikonge, Tabora Mjini, Kaliua, Urambo, Nzega - CDM inakuwa ya 3 baada ya CCM na CUF. ni kweli kutakuwa na challenge kubwa hasa ukizingatia kambi za CCM katika jimbo la igunga bado ipo thabiti unless RA aamue kutojihusisha na kampeni, maana karibia kila kaya katoa bima ya afya kwa maana hiyo anawajua wapiga kura wake wote wa igunga na kadi zao za kupigia kura zipo kwenye mafaili yake.

Anyway, Pamoja Tutashinda - Sababu Chadema ni mtetezi wa wanyonge, kimbilio la wenye shida na sera zake zinauzika.
 
Tatizo lawatanzania ni uvyama, tutachagua mtu muadilifu jamani,, CDM, UDP, CCM, NCCR, CUP vyote sawa, we need watu wa adilifu na watiifu kwa watu wao,
 
Wote mnaounga mkono wazo hili ni CCM.

Sihitaji kwenda Chuo kujua uhusiano wa CUF na CCM!!!

Endapo CUF wangekua wapinzani wa CCM wazo lako ni zuri, Ila kwasasa CUF ni wapinzani wa CDM. kwahiyo unalolisema halitawezekana kamwe.

Kaka umeona CCM wanataka kurudisha jimbo lao kupitia CUF wajanja sana hawa jamaa. Igunga lazima atashinda CCM kwasababu RA atalazimwa na CCM kumpigia kampeni mgombea atakayepishwa na CCM na hatoweza kukataa maana hajui hatima yake kabla hajavaa pingu unategemea nini lazima awe kibaraka wa CCM hadi kufa hli kuepuka pingu na gereza na 2015 nadhani atakimbia nchni kama ataona wapinzani wanashika dola.

Kama tungekuwa na Usalama wa Taifa strong wangelinda mali zote kubwa zisitoroshwe kwenda nje ya nchni.
 
Ni wazo zuri Prof kugombea akiungwa mkono na vyama vingine vyote vya upinzani, lakini kwanza aende mjukwaani na kuwaomba radhi wananchi kwa kauli zote chafu alizozitoa dhidi ya CDM, bila hivyo asahau tu hatapata support ya CDM. Alisema CDM ni wakuogopwa, akasema anayedhani CDM itaongoza nchi aende Loliondo akapate kikombe cha Babu.

Hatutamsamehe mpaka ameomba radhi. CDM MSIDANGANYIKE LIPUNDA HANA LOLOTE TOFAUTI ATAKALOPELEKA BUNGENI. TUNAO VIJANA WA KUTOSHA KUTETEMESHA WANA MAGAMBA.
 
Wakuu tukiacha itikadi, CUF wana nguvu Igunga Kuliko CDM

Matokeo ya Mwaka Jana

Igunga

Msimamizi wa jimbo hilo Protas Magayane alimtangaza Rostam Aziz wa CCM kuwa mshindi wa kiti cha ubunge baada ya kupata kura 35,674 dhidi ya mpinzani wake, Leopord Lucas Mahma wa CUF ambaye amepata kura 11,321. kwa maana hiyo CDM walikwa wa 3

Pamoja na tahmini yako ukumbuke kuwa kata ya Igunga mjini inashikiliwa na CDM. Na mjini ndipo mambo yote yanapoanzia, la muhimu tu ni kuwa CDM wasimamishe mtu makini anayechagulika. PROF. LIPUMBA ATUSUBIRI KWANZA.
 
Mkuu,

Tukiweka mbali ushabiki wa Chama tunahitaji mtu kama Lipumba bungeni. Hali ya uchumi wa nchi unaenda kombo na walioko bungeni sio wajuzi wa uchumi waliobobea Lipumba anaweza kuongeza nguvu bungeni kuzidi kuikosoa serikali iliyo madarakani.

ni lini tukaitaji economic consultant kwenye siasa? Kama anafaa basi mwambie jk amteue lipumba awe katibu mkuu wizara ya fedha na uchumi. Kisiasa lipumba hafai kukaa bungeni hana uthubutu wa kumpinga ccm.

Kiuchumi namkubali uyu babu. Onyo: milele cdm simameni kama cdm,kafu na sisiemu walishakuwa wamoja! Msingizie ukabila ktk siasa,eti mpaka awe mnyamwezi,mdini au vp ndo apate,je uyu rose_tamu alikuwa mnyamwez?
 
Acheni mambo yenu bwana
Hatuwezi kuendesha nchi wala vyama kwa misingi ya ajabu namna hii.
na wote ni mashahidi kwamba katika nchi yetu maamuzi yote ambayo
hufanyika kwa misingi hii hayajawahi kuwa na faida kwa upande wowote
ule, hayajawahi kuwa na faida kwa vyama husika vya siasa wala kwa wananchi.

Swala la kumshinikiza Lipumba kugombea halina uhusiano wowote na Chadema
kutogombea, Nchi hii haitoongozwa na vyama vya siasa Imara bali itaongozwa na
Chama cha Siasa Imara. Acheni wote watatu wapambane, CUF, CCM na CHADEMA.

Kama Lipumba hakuona umuhimu wa kumuachia DR amuondoe Jakaya Ikulu kirahisi
hakuna sababu yoyote ya CHADEMA kumuachia Lipumba wala CUF kupata ushindi
bwerere katika nafasi yoyote ya uongozi.

Sitaki kusikia Siasa za Hovyo Hovyo namna hii, tena nimechukizwa sana kuona
kwamba bado kuna watu wanaujasiri wa kutoa hoja za namna hii, nimeichukia
hoja hii sana na nimemchukia mtoa hoja pia.

Wote ni Mashahidi kwamba, kabla, na baada ya Uchaguzi CUF na Lipumba in
person, wametumia nguvu kubwa sana katika kuhakikisha inakichafua CHADEMA
kwa kila namna.

Baada ya Uchaguzi, Wakati Chadema wanaandamana kupiginia mambo ya msingi
kwa watanzania, CUF na Lipumba walianza kuzunguka kote wanakojua wanasikilizika
na kutangaza kwamba Chadema ni Chama cha Udini.

Achana na Patrinership yao na CCM Zanzibar, sababu sijawahi kuona ubaya wake,
as long as Wazinzabar waliona unawafaa wao kama jamii, CUF waliendeleza informal
partinership na CCM Bungeni, ili kufisha vyote viwili, nguvu ya Upinzani Bungeni na
Nguvu ya Chadema pia.

Waoh, where do you get the guts to recommend Chadema not to go for
Igunda for the sake of CUF. come on.

Let them all go for it. Igunda will decide for their own interests.
 
Mkuu,

Tukiweka mbali ushabiki wa Chama tunahitaji mtu kama Lipumba bungeni. Hali ya uchumi wa nchi unaenda kombo na walioko bungeni sio wajuzi wa uchumi waliobobea Lipumba anaweza kuongeza nguvu bungeni kuzidi kuikosoa serikali iliyo madarakani.

Unachosema ni sawa lakini Lipumba kisha poteza sifa hata kua katibu wa mbunge wachadema hafai...( sorry kama unamtazamo tofaut) .
 
Busara ni pamoja na kuendeleza msingi iliyoaanzisha taasisi/chama. Na kwa chama cha siasa ni hatimaye kushika madaraka ya nchi, hii ikiwa ni mchakato kuanzia ngazi za vijiji/serikali za mitaa na hatimaye serikali kuu.

Unaweza kuonekana kama ubinafsi, lakini ukweli ni kuwa chama cha siasa chenye nguvu, hiyo nguvu inatakiwa ipimwe kwenye kushinda uchaguzi na pia inavyojipambanua kwa wera zake. Kwa maana hiyo, haiwezi kuingia akilini kusema eti, CDM iwaachie CUF kama wagombea pekee katika nyakati hizi kinapojitahidi kujipanua na kujianisha kama chama chenye nguzu Tanzania.

Hii ni sawa na kuwaambia CCM wasishiriki uchaguzi pemba kwa kuwa tu CUF wamekubaliana na ccm kuwa naserikali ya umoja wa kitaifa na kuwa CUF ndio inayokubalika huko Pemba. Ingefaa basi pia kuvishawishi vyama vyote visishiriki kabisa chaguzi!

Hivyo, mtizamo wangu ni CDM washiriki kama CDM na CUF washiriki kama CUF, kadhalika CCM na wengineo. Hiki ndicho kipimo pekee cha nani anafanya nini na anaelekea wapi!
 
Ni wazo zuri Prof kugombea akiungwa mkono na vyama vingine vyote vya upinzani, lakini kwanza aende mjukwaani na kuwaomba radhi wananchi kwa kauli zote chafu alizozitoa dhidi ya CDM, bila hivyo asahau tu hatapata support ya CDM. Alisema CDM ni wakuogopwa, akasema anayedhani CDM itaongoza nchi aende Loliondo akapate kikombe cha Babu. Hatutamsamehe mpaka ameomba radhi. CDM MSIDANGANYIKE LIPUNDA HANA LOLOTE TOFAUTI ATAKALOPELEKA BUNGENI. TUNAO VIJANA WA KUTOSHA KUTETEMESHA WANA MAGAMBA.

Mkuu huyu hatuna haja ya kumsamehe kwa sababu hajatutusi ila alidhihirisha ilivyo brainwash so we h've nothing to him ....Ombi langu kwa CHADEMA kipendekeze kichwa makini kitakachouzika kwa wana IGUNGA ...kitu mpera mperaaaaa......P'poooz powerrrrrrrr
 
It wiil be a tough fight. CCM wana marriage of convinience na CUF haitamuuga mkono mgombea wa CUF.CDM asitumie nguvu nyingi,itakuwa ni vigumu kushinda uchaguzi mdogo kwani CCM na serikali yake watatumia nguvu na fedha nyingi.CUF vile vile hana lake pale is a junior parterner wa CCM.
 
Ingekuwa igunga ipo mtwara au lindi, ningeshauri asimame lipumba lkn si vngnevyo.
 
Hatasiku moja upinzani bungeni hauwezi kuletwa na cuf (ccm-b) isipokuwa utaletwa na chdema ambayo ni nguvu ya watz......utajadili vipi upinzani halafu ukawa-include cuf........................cuf ni taasisi ta kidini zaidi

cdm ilimshinikiza dk slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza mh lipumba ili agombee ubunge jimbo la igunga:
  • ni mzaliwa wa tabora
  • ni mwenyekiti wa chama cha cuf ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina mbowe, lissu na wengine
  • itaijenga cuf kisiasa na kujenga upinzani wenye nguvu bungeni
  • cdm haina nguvu sana kulinganisha na cuf kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
 
..compromise ni Prof.Lipumba kuhamia CDM halafu asimamishwe kugombea ubunge Igunga.

..tatizo la Prof.Lipumba ni kwamba anapenda kujipendekeza na kumchekea-chekea JK. hana tofauti na Zitto linapokuja suala linalomhusu JK, they just cant help themself. They would rather go against their parties.

..naomba mrejee concession speech ya Prof.Nguyuru Lipumba. yaani ukimlinganisha na JK siku ule utaona kabisa kwamba Prof.Lipumba would have made a better president.
 
Back
Top Bottom