Pendekezo: Katibu wa Bunge ajiuzulu kwa kupotosha taifa

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
6,146
6,999
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano
 
Naunga mkono hoja, bi mkora unapaswa kumjairo huyu mtendaji wake aliyetoa taarifa ya udanganyifu kwa umma
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

Hawezi kujiuzulu kwa maana ya watanzania wengi ni waoga wa kueleza hisia zetu!!!!
Hebu jiulize Ngeleja, Adamu Malima wako wapi licha ya kunangwa na ripoti waziwazi!!! Bado wapo ofisi za umma mpaka Lowassa leo anawananga waige mfano wake wa kujiuzulu.
Ama kweli ibilisi akizeeka anakuwa malaika, Lowassa leo amekuwa malaikaz.
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

Naunga mikono. Upime mwenyewe na aamue
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

leo ukisema uongo, kesho itakugharimu kuusema ukweli.
 
Mbona raisi wenu anapotesha watu kila siku na haja jiuzulu?
 
resign! In tz ole wako, ukifanya hivyo tuu makosa yote ya idara uliyokuwa unaongoza unapewa wewe badala ya kukusifu watakupakazia mpaka ujute kwa nini ulichukua maamuzi hayo, hata ukiuchuna hakuna wa kukufatilia! Welcome to tz the land of waongeaji wasio na matendo.
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

Hii ni Tanzania, kama ni kweli ameongopa hatafanywa kitu, tena anaweza kupandishwa hata cheo. Hii ni Tanzania.
 
Nakuunga mkono 100% kwa sababu;
  • awali wakati anaulizwa alikana kwamba yeye si msemaji wa bunge ila spika ndiye ajuaye na mwenye majibu
  • akakurupuka kujibu mambo yasiyo mhusu kama alivyo kiri awali kuwa posho hizo hazijapanda hata cent ila huu ni uzushi wa vyombo vya habari na kuwashangaa wabunge wanao kiri kupanda huko
  • Spika (mwenye dhamana) kadhihilisha kuwa ni mwongo yaani si mkweli hata kidogo
  • tuta mwamini vipi kwa yaliyo pita na mambo yajayo haweze kuuaminika tena kwa sababu ana ajenda ya siri
kweli alipaswa kujiuzuru ila tatizo huu msamiati hapa Tz hautumiki sana hivyo si rahisi kihivyo
MUNGU LABDA AINGILIE KATI
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

Mkuu hoja ya ni yamsingi lakini tanzania hakuna hiyo desturi ya viongozi kuchukua maamuzi kama hayo we chukua mfano Wa Jairo kulikuwa na haja gani yeye kutochukua hatua ya kujiuzulu mpaka kuunda kamati ya kumchunguza ikitumia pesa za walipa kodi wakati matokeo yake alikuwa anayajua?

Mytake:Wapi Ngeleja,Jairo,Malima, Luhanjo na wengine wengi.......
 
Tatizo la kashilila ni kufanya kazi ya siasa badala ya ile aliyopewa. I doubt bis doctorate kwakweli. Nadhani huyo jamaa hamnazo kabisa, yaani hata wasaidizi wake wanabusara sana kumpita yeye
 
Leo nimesikia kwenye vyombo vya habari Spika Anna Makinda amekiri kuwa posho za wabunge zimeongezeka, hapo juzi kati katibu wa bunge Dr Kashilila alikanusha kwenye vyombo vya habari ya kwamba posho haijaongezeka, je mgongano huu wa viongozi wakubwa wa bunge kutofautiana katika kauri zao ndo kusema hakuna mawasiliano mazuri?
Na kama ni kweli Dr alikuwa akifahamu ukweli kwamba posho imeongezeka, alipata wapi ujasiri wa kukanusha?. Kwa suala hili ili Dr alinde heshima yake naomba abwage manyanga kwani ameuongpopea umma wa watanzania kwa kufahamu ukweli wa jambo hili.

Asipofanya hivyo hii ina prove kwamba uwajibikaji kwa viongozi wa nchi hii ni ndoto.

Wadau naomba kuwakilisha.
 
Nakuunga mkono 100% kwa sababu;
  • awali wakati anaulizwa alikana kwamba yeye si msemaji wa bunge ila spika ndiye ajuaye na mwenye majibu
  • akakurupuka kujibu mambo yasiyo mhusu kama alivyo kiri awali kuwa posho hizo hazijapanda hata cent ila huu ni uzushi wa vyombo vya habari na kuwashangaa wabunge wanao kiri kupanda huko
  • Spika (mwenye dhamana) kadhihilisha kuwa ni mwongo yaani si mkweli hata kidogo
  • tuta mwamini vipi kwa yaliyo pita na mambo yajayo haweze kuuaminika tena kwa sababu ana ajenda ya siri
kweli alipaswa kujiuzuru ila tatizo huu msamiati hapa Tz hautumiki sana hivyo si rahisi kihivyo
MUNGU LABDA AINGILIE KATI

Ndugu yangu unayoyasema ni kweli tena ni kweli tupu. Tatizo la Tanzania ni kuwa udanganyifu unaazia kwa rais wa nchi, waliopo chini wataachaje kudanganya? Tunakumbuka kuwa rais alisema hafahamu wamiliki wa Dowans baada ya siku chache akasimama waziri wa Nishati na Madini, mh. Ngeleja akawataja. Hivyo, haishangazi kama kaatibu wa bunge anaweza kusema yeye siyo msemaji na baadaye anasema posho haijapanda bila kujitambulisha kama yeye amepewa nafasi ya kuwa msemaji. Mwisho wa yote anakuja spika anasema kuwa posho imepanda, bila kukanusha kile kilechosemwa na katibu wa bunge. Hakika hiki kifo tunachokiendea ni kifo kibaya sana.

Tusishangae kama ile katiba mpya tunayotarajia ikawa kitu kingine. Kwa uwongo wa kiwango hiki na kutoka kwa watu wa kiwango cha spika kwa kweli tunatakiwa kufanya maombolezo ya kitaifa. Hivi siku tukiwambiwa kuwa kilichoazimiwa bungeni kuhusu katiba siyo katiba mpya bali ni kitu kingine ni nani atakayebisha?
 
Kwa kutuona sisi Watanzania nni Majuha na mazezeta natoa wito huyu Katibu wa Bunge ndg Kashilila ajiuzulu mana amedanganya umma huyu nae ni mwizi na fisadi tu...kama hataki tulianzishe maandamano

Mwizi akijiuzulu Mkuu wa waizi anamteua mwizi mwingine!
 
Kujiuzulu! sio Bongo hii labda ijayo, hapa ata mtu ateketeze kijiji kwa risasi kwa kisa cha mtoto kuiba mhogo tu hawezi jiuzulu, sembuse maandishi karatasin?
 
Back
Top Bottom