Pendekezo: John Heche amrithi Zitto Kabwe

zitto amepandisha chati chama...yeye anafaaa uenyekiti ama ukatibu mkuu mbowe,hawezi shinda kwa urahisi kama akigombea urais, slaa ni jembe sana...ila ni mzee...abaki kama mshauri vijana waendeshe kazi....mtei asiingilie kabisa chama...hana hati miliki....chama ni cha wananchi...hazina ya kina mnyika,mdee,lissu,msigwa,nassari sugu, heche nk inatosha kusukuma chama na kupata wabunge wengi na hatimae kuchukua nchiii....
 
Ni maoni ya mtu binafsi lakini, je Wengi mnao changia humu mnaijua vizuri historia ya chadema Na nguvu kuu waliyokuwa Nayo chini ya Dr. Amani walid Kabourou miaka ya tisini, yupo wapi huyu jamaa now, karudi CCM ........ Siasa za bongo upuuzi mtupu
 
zitto amepandisha chati chama...yeye anafaaa uenyekiti ama ukatibu mkuu mbowe,hawezi shinda kwa urahisi kama akigombea urais, slaa ni jembe sana...ila ni mzee...abaki kama mshauri vijana waendeshe kazi....mtei asiingilie kabisa chama...hana hati miliki....chama ni cha wananchi...hazina ya kina mnyika,mdee,lissu,msigwa,nassari sugu, heche nk inatosha kusukuma chama na kupata wabunge wengi na hatimae kuchukua nchiii....

Naona kuna watu wanapata shida sana wanaposikia Mzee Mtei akitoa kauli kuhusu chama. Jamani tuwe wakweli hivi wakati Nyerere akiwa nje ya uongozi wa ccm na serikali mbona alikuwa akitoa matamko mazito yamkini yaliyowahusu hata viongozi walioko madarakani na hotuba zake tunazisikia hata hivi sasa. Kwa mtazamo wangu si makosa kwa Mtei aliye muasisi wa chama kufuatilia maendeleo ya chama hicho.
 
Mkuu wangu ukichunguza sana watu wanaompinga mzee Mtei Mwasisi wa chama utagundua ni watu wenye matatizo kumkichwa!
 
wanajf,

kiongozi wa bavicha taifa john heche ni kati ya wanamapinduzi waliojitolea na kufanya kazi kubwa sana ya kupigiwa mfano.

Kila tunaposoma vyombo vya habari john heche anaripotiwa yuko vijijini kufungua mashina, ofisi na kuingiza wanachama wapya. Ni mwezi uliopita tu alikuwa mikoa ya nyanda za juu kusini na kuingiza maelfu ya wanachama.

Wiki hii mwanzoni alikuwa morogoro na leo yuko vijijini kagera akifanya kazi kubwa ajabu. Hata anapokuwa mapumzikoni dar john heche hatulii ofisini bali anazunguka kila kona ya dar akifanya mikutano na kuzindua mashina.

Ni wazi kabisa kwamba kiongozi anayependwa na nyota wa chama hicho kwa sasa katibu mkuu dr willibrod slaa amekuwa na majukumu mengi kiasi kwamba pengo la naibu katibu mkuu bara linaonekana wazi.

Naibu katibu mkuu zitto kabwe amekuwa na majukumu mengi ya kibunge kiasi kwamba anashindwa kumsaidia katibu mkuu majukumu yake.zitto awe tu mjumbe wa kamati kuu ambaye atakuwa hana majukumu ya kila siku ndani ya sekretariati.

Ninatoa mapendekezo kwa viongozi wa chama kwamba ikiwezekana katika uchaguzi wa sekretariati mpya mwakani john heche akabidhiwe mikoba ya zitto kabwe kwa ufanisi zaidi.ikumbukwe kutokana na majukumu mengi ya kibunge ya zitto ameshindwa karibu mara 4 mfululizo kuhudhuria vikao muhimu vya chama hicho vilivyotoa maamuzi mazito.

John heche ni jasiri, mpambanaji, anayefanya kazi usiku na mchana na aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya chadema.

Hakika john heche ni jembe kwelikweli anayepaswa kupandishwa daraja zaidi.

Nawasilisha.

naunga hoja 100% mkuu
 
Hehehee mkuu mleta mada tafadhali peleka pendekezo lako mahala linapousika kwa utekelezaji, waambie JF wanaunga mkono hoja hahahaa
 
Sijaelewa watu wengine wanafikiria kwa kutumia nini?HECHE !!! hata kiswahili hajui vizuri,afadhali ungesema MNYIKA.
 
Mkuu wangu ukichunguza sana watu wanaompinga mzee Mtei Mwasisi wa chama utagundua ni watu wenye matatizo kumkichwa!
na watu wanaompinga zitto nao wana matatizo kumkichwa maana zitto amejenga chama sana tu mpaka kilipo fikia, mie ni mmoja wa wanachadema waliojiunga kwenye siasa na chama kwa sababu ya huyu kijana zitto, so nashangaa sana mnapo mblame zitto for no good reasons
 
Hehehee mkuu mleta mada tafadhali peleka pendekezo lako mahala linapousika kwa utekelezaji, waambie JF wanaunga mkono hoja hahahaa

Mkuu kwa taarifa wahusika wameshachukua hili pendekezo lakini halitakuwa haraka kama unavyodhani.Bali litatekelezwa wakati wa uchaguzi mkuu wa chama mwakani.
 
Acha kumdharirisha Mh. Zitto yan hapo ni sawa na Bajaj (Heche) na VX V8 (Zitto)
 
Back
Top Bottom