Waungwana,
Imekuwa ni ada sasa kwa wanasiasa na hasa katika Bunge letu tukufu kusisitiza aidha umuhimu wa kujipanga au kusema kuwa sasa wanajipanga au wamejipanga. Tatizo kubwa ni kuwa, toka msisitizo wa kujipanga umeanza hakuna anayezungumzia kujipangua.
Lakini, kwa tuliopitia JKT hata wale wachambuzi wa mpira tunafahamu kuwa wakati fulani kikosi kinalazimika kujipangua ikiwa ni mbinu ya kujipanga upya, hususan pale ambapo mpango wa kwanza umejikuta umekwama. Ni maoni yangu kuwa, dhana hii inaweza pia kuwa na mantiki katika siasa na utawala.
Ndani ya Jukwaa hili tumejipanga kila kukicha kulaumu, kudhihaki na kukosoa bila mafanikio, je si wakati wa Jukwaa hili kujipangua kwa kujitokeza na vipaumbele vya Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kuinadi kwa wagombea na vyama kuisimamia na kuiweka katika ilani zao? Hatutakuwa tumetenda haki zaidi sisi wasomi kwa taifa letu?
Kama hivyo ndivyo, uchaguzi mkuu na chaguzi za ndani ya vyama vinabisha hodi mbele yetu.................. ni maeneo gani kumi ya vipaumbele tunadhani yanatakiwa kupanguliwa au tunapaswa kama taifa kujipangua? Maeneo haya yanaweza kuandaliwa kama Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu 2010 na kushawishi wagombea na vyama kubeba agenda hizo katika ilani zao.
Tusipofanya hivyo, ipo hatari ya Jukwaa letu hili tukufu kutumika kujadili watu na kuchafuana badala ya 'issues' za msingi na haja za wananchi wetu.
Napendekeza Mwanakijiji na moderator waratibu mchakato huu kwa kuanzia.
Nawasilisha waungwana!