Pendekezeni jina la kampeni ijayo ya CHADEMA

Tanzania mpya

Tanzania mpya, Uongozi mpya, Maisha mapya

Jambo muhimu ni kuelimisha watu mpaka ngazi ya kijijini ambako watu wengi ndipo walipo na ndiko mahala ambapo hakuna usimamizi mzuri wa kura kama ambavyo tumejionea jinsi kura za mijini zilivyoweza kulindwa vizuri na vijana wa "Peoples Power" jambo muhimu ni zile percent alizoongelea JK kuwa 70% hufuata upepo basi hapo ndipo pakujikita hasa katika kundi la vijana ambao makali ya maisha wanayapata kwa kilele kikubwa, na mwisho CDM anzisheni mfuko maalumu wa kuchangia gharama za kampeni kuanzia hivi sasa na sio kusubiri dakika za majeruhi au kuwasubiri wasamaria wema kama mzee Sabodo kwani kazi hii ni kubwa kuliko uwezo wa watu wachache wenye upendo na mabadiliko
 
Vijana Lazima tuungane na viongozi wa CDM kuhakikisha tunarudi vijijini kwetu ili wakati wa
harakati za Operation Mapanki kama nilivyopendekeza tushiriki kuamsha watunzania

Peoples Power

Hakuna kulala mpaka 2015
 
Mimi nadhani operation ukombozi ni safi. Kwanza ni neno moja, rahisi kutamkika. Au kama vipi turudie operation sangara. Ni nzuri pia
 
wadau . Naomba tujadili jina linalofata baada ya operation sangara na namna ya kuindesha kwani sasa hivi ni mtu kwa mtu, mh mbowe alisema jaja hakuna kijiji ambacho wabunge wa chadema hatakikanyaga.:-*
"operation kimbunga"
 
WADAU . naomba tujadili jina linalofata baada ya operation sangara na namna ya kuindesha kwani sasa hivi ni mtu kwa mtu, mh mbowe alisema jaja hakuna kijiji ambacho wabunge wa chadema hatakikanyaga.:-*
operation CRUSADE
operation ONDOA UISLAMU
operation CHAGANISE THE NATION
operation MWAGA DAMU
operation LETA MACHAFUKO
 
Nakubali kwamba "Operesheni Sangara" ilikuwa nzuri sana na matunda yake yameonekana ila si vizuri kuendelea na jina hilo hilo - opesheni ni kitu kina kuja kwa kusudio na wakati maalumu na kupita. Sangara imekamilisha malengo yake, ije nyingine. Pia unaweza kushangaa ni kwanini opesheni hii imeleta mwamko mkubwa maeneo ambako "Sangara" wanapatikana, yawezekena ukanda wa kati na kusini wa nchi yetu hakukuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na jina lililotumika - SANGARA - ambako wakazi wengi hawamfahamu vizuri? Sijui.

Mimi nashauri litafutwe jina na kauli mbiu ambayo hata mtoto mdogo akiisikia itamtoa machozi na kuamsha moyo mpya wa kizalendo - Afrika Kusini walitumia sana mbinu hii dhidi ya makaburi - muulize Jacob Zuma anajua vizuri sana hili. Tanzania hapa ilipo sasa hivi ina matatizo nadhani yanayokaribia ya Afrika Kusini ya enzi zile. Unahitajika ushawishi mpya, mwamko mpya, hamasa mpya - vijini na mijini hata kwa wa-Tz waishio ng'ambo. Watu wajue thamani ya kujiandikisha na kupiga kura; kutokuuza shahada, kufikia maamuzi sahihi, kutokughilibiwa na hadaa za wanasiasa wanaotumia mbinu mbali mbali zikiwemo chafu za UDINI, amabao kimsingi haupo ila unajaribu kupandikizwa na kuchochewa.

Na wakati wa kuanza hayo si kusubiri hadi wakati wa kampeni, vyama vya upinzani anzeni haya mambo sasa. Ni haki yenu kisheria kufanya siasa na si kudanganyana eti kampeni zimeisha!!!
 
Operation no more Mtanzania kuishi kwenye nyumba za TEMBE/Elimu bure kwakila Mtanzania inawezekana/Maisha bora kwa kila mtanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom