Pendekezeni jina la kampeni ijayo ya CHADEMA

Operation JUBILEE
Huu ni mwaka wa 50 tangu tupate uhuru.
La sivyo operation ANGAZA ili kuleta mwanga unaofichua wizi na maonevu mengine.
 
Tutapiga kura kwa kuona "jina" lipi limependwa na watu wengi ili tutoe suggestion yetu kwa pamoja
 
Operesheni ondoa boriti kisha vibanzi!

Maana yake:
Kazi ianze na kudeal na challenges za ndani zinazowakabili wao mfano juu ya muundo wao, malamiko ya baadhi ya viongozi na wanachama wake, kujitangaza ipaswavyo ili chama kiaminiwe na makundi ya watu wote hata vijijini kote, kuwadhibiti wanaoonekana kuwa wanakaidi kutekeleza yale wanayokubaliana pamoja kupitia vikao vyao halalai (Wasaliti), kujijenga kiuchumi n.k ili wanapoanza kudeal na Wapinzani wao, basi wawe na uwezo wa kutosha na pia kukubalika kwa upana zaidi mbele za Wananchi wa makundi yote.
 
mimi nina wazo tofauti tusifikirie sana katika kutafuta jina ila tufanye kazi ili kuhakikisha watu wote wanakuwa na uelewa wa jinsi gani nchi inaliwa na pia kuwepo kwa vuguvugu mpya ya kudai mabadiliko.mimi mwenyewe naelewa ya kuwa kuwepo kwa katiba mpya hakutasaidia iwapo watu hawatakuwa makini kusimamia na kuitetea na kubali kuwa huru kifikra na kiakili pasipo kuwa na uoga. natamani sana siku moja watu wote wa tanzania wawe na uelewa na udhubutu wa kudai haki zao kama walivyofanya pale arusha.
 
Back
Top Bottom