PCT Yaibua Upya Hoja ya Kadhi!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Baraza Kuu la Makanisa ya Pentekoste nchini limeibua upya hoja ya Kadhi kwa kuitaka Serikali kutopeleka muswada Bungeni kuhusu masuala ya dini moja kwa kuwa huo ni uvunjaji wa Ibara ya 19 ya Katiba ambayo inasema kuwa Serikali haina dini ila watu wake wana dini. Badala yake wawaachie Waislamu wenyewe kushughulikia suala hilo kivyao na kimsingi hawana tatizo na uanzishwaji wa mahakama hizo isipokuwa hawaafiki Serikali kujishughulisha na suala hilo kama ilivyoanza kujionyesha wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipounda kamati kushirikiana na waislamu kuanzisha mchakato wa kuunda mahakama ya Kadhi. (Source: Majira, tr 02/11/2009).
 
Tunapelekwa kwenye mdomo wa simba mkali hivi hivi! Mungu tunusuru na huyu mnyama aitwaye Kadhi!
 
Mahakama ya Kadhi yazidi kuwachanganya maaskofu

na Betty Kangonga

BARAZA la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT), limeitaka serikali kuacha suala la Mahakama ya Kadhi liendeshwe na kuratibiwa na Waislamu wenyewe badala ya kuingilia.

Wito huo waliutoa jana jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya baraza hilo Kurasini walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato ambao wamesema unaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Mwenyekiti baraza hilo, David Batenzi alisema serikali haipaswi kuhusika kwa kuwa katiba inaeleza wazi kuwa haina dini, lakini wanashangazwa na kujiingiza katika mambo ya dini.

“Baraza la Maaskofu linakubaliana na uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, lakini tunashauri suala hili lisipelekwe bungeni kwa sababu ni uvunjaji wa katiba ya nchi kifungu cha 9 kanuni ndogo ya 6,” alieleza Batenzi.

Aidha, alisema ingawa serikali iliamua kuwaachia Waislamu kufanya matengenezo ya kanuni, bado inatia shaka kwa kuwa suala hili lipo chini ya Kamati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

“Wao wamewaachia Waislamu suala lao, lakini kwanini Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na kamati yake iamue kuwasaidia katika kutengeneza kanuni?” alihoji Batenzi.

Alisema kujihusisha kwa Ofisi ya Waziri Mkuu katika matengenezo ya Katiba ya Waislamu, ni lazima kutakuwepo na matumizi ya fedha zinazotoka kwa walipa kodi ambao ni wafuasi wa dini mbalimbali.

Hata hivyo, Batenzi alishauri kuwa iwapo kuanzishwa kwa katiba hiyo ya Mahakama ya Kadhi kwa waislamu kutafika ukingoni, kuna dalili kuwa kanuni hiyo inaweza kutinga bungeni ili kufanyiwa majadiliano. Alisisitiza kwamba, kutokana na serikali isiyo na dini kulipeleka bungeni suala hili, linaweza kuwagawa wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wenye itikadi za dini tofauti na hakuna mbunge atakayekubali kuona dini yake ikishindwa. Aidha, waliwataka viongozi wa serikali kufuata nyayo za hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo katika uongozi wake, aliongoza taifa kwa kutotaka ubaguzi katika dini au kuifanya dini moja kuwa bora kuliko nyingine.
 
Kwanini wanataka kuifundisha serikali kazi who are they? kama siyo wivu na fujo zisizo na maana nafikiri maaskofu wamechoka na amani ...wanataka wakajifiche vatican kule wafichapo waouvu lol.
 
Kwanini wanataka kuifundisha serikali kazi who are they? kama siyo wivu na fujo zisizo na maana nafikiri maaskofu wamechoka na amani ...wanataka wakajifiche vatican kule wafichapo waouvu lol.

I think you just have issues with the Vatican and the Catholic church because the Vatican has nothing to do with PCT or Pentecost priests.

Anyway I think PCT's move in this case was unnecessary because this issue has already been discussed by different parties in the past. If I'm not mistaken islam leaders and the government are still working on a compromise. I think we all should wait to discuss what they came up with. PCT is a tad late in giving it's standings on this issue.
 
Kwanini wanataka kuifundisha serikali kazi who are they? kama siyo wivu na fujo zisizo na maana nafikiri maaskofu wamechoka na amani ...wanataka wakajifiche vatican kule wafichapo waouvu lol.

Ndugu kwanini usitafiti kwanza kabla ya kuchangia?Vatican siyo makao makuu ya kila kanisa duniani.Vatican ni makao makuu ya kanisa katoliki na hao waliozungumza siyo maaskofu wa kanisa katoliki.Ni maaskofu wa kipentekoste.
 
Buchanan,
Mkuu naheshimu sana michango yako lakini unapokuja na hoja kisha wewe mwenyewe unakianzisha sijui unalotaka.. Mbona serikali iliweka mkataba MoU na kanisa na hatusemi kitu au hilo kanisa sio dini mbona haikufanyika kwa dini zote.
Unapinga Kadhi endelea kupinga kivyako, lakini usitake kuuza sura hapa..mijiutu mingine bana aaaah!
 
Hakuna similarity baina ya MoU ya Taasisi fulani ya Kikristu na Mahakama ya Kadhi. Mahakama ya Kadhi inawahusu wasilamu tu na ni sehemu ya usilamu wakti ishu ya MoU ya kanisa ilihusu kutoa huduma za kijamii kwa watanzania wote kwa ujumla wao bila ubaguzi. Sasa wewe ndiye usiturejeshe nyuma na ububu wa akili.
 
Mikristu bada, akili zao kama picha za sura zao!
 
Buchanan,
Mkuu naheshimu sana michango yako lakini unapokuja na hoja kisha wewe mwenyewe unakianzisha sijui unalotaka.. Mbona serikali iliweka mkataba MoU na kanisa na hatusemi kitu au hilo kanisa sio dini mbona haikufanyika kwa dini zote.
Unapinga Kadhi endelea kupinga kivyako, lakini usitake kuuza sura hapa..mijiutu mingine bana aaaah!
Huyu mr Kadhia awepo na aeneshwe na wahusika, otherwise whether we like or not the our future will be worse than Nigeria's!
 
Sikiliza wee mpuuzi,
Ibara ya 19 inakataza serikali kujihusisha na swala lolote la dini moja linalohusu nchi nzima (nchi haina dini) isipokuwa tu kama swala hilo linahusu waumini (WATU) wa dini hiyo.
MoU ni mpango wa Katoliki enforced kwa NCHI nzima hata wale wasiokuwa waumini.
Mahakama ya Kadhi ni kwa WATU wa dini hiyo..
 
Wewe kweli ni kilaza, na ndio maana posts zako nyingi ni NDEEEFU kujaribu kuficha ukilaza wako.

Kwa kifupi ibara ya 19 ipo ktk sehemu ya III;

The Right to Freedom of Conscience
...
19. Right to freedom of religion.
...

Ibara yote ya 19 ni hii :)(kwa ukamilifu wake)

19.-(1) Every person has the right to the freedom to have conscience, or faith, and choice in matters of religion, including the freedom to change his religion or faith.

(2) Protection of rights referred to in this Article shall be in accordance
with the provisions prescribed by the laws which are of importance to a
democratic society for security and peace in the society, integrity of the society and the national coercion.

(3) In this Article reference to the term "religion" shall be construed as
including reference to religious denominations, and cognate expressions shall be construed accordingly.
Sasa wewe ambaye si mpuuzi unioneshe hoja yako inaingia wapi hapa, maana sioni hata neno 'serikali' hapa. MoU inapingwa wapi na kivipi, Mahakama ya Kadhi inaidhinishwa wapi hapa.etc etc

Fingers crossed, maana I'm about kupindua meli. teh teh teh
 
Mkuu soma habari iliyotangulizwa na Buchanan..Kisha nitafsirie ibara ya 19(2) unaielewa vipi...Na kwa kumalizia tu inaposemwa - Serikali haina dini ila watu wake, sii maneno ya PTC wala KKKT ila ni katika kuielewa katiba..
 
Back
Top Bottom