Pawassa,, Lunyamila,Manofu, Mahadh walipotonesha ‘donda’ la Watanzania

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,971
3,827
Manofu, Pawassa, Mahadh, Lunyamila walipotonesha ‘donda’ la Watanzania





.Ni katika mechi ya Veterans wa Simba, Yanga U/Taifa
.Wapeleka ‘uhondo’ Dodoma Machi 27

NA MICHAEL MAURUS
MASHABIKI wa soka waliokosa kuuona mchezo wa hisani wa kuchangia waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Gongolamboto, baina ya wachezaji waliowahi kutamba katika timu za Simba na Yanga, uliofanyika Machi 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bila shaka watakuwa wamezidhulumu nafsi zao.
Katika mchezo huo, Simba Veterans walishinda bao 1-0, bao hilo likiwekwa kimiani na Shekhan Rashid kutokana na mpira wa adhabu ambapo mashabiki waliofika uwanjani siku ile, walipata fursa ya kushuhudia nyota waliowahi kutamba na timu za Simba na Yanga miaka ya nyuma kidogo wakionyesha vitu adimu ambavyo kwa sasa ni nadra mno kuviona katika viwanja vyetu.
Pia, mbali ya soka, mashabiki waliokuwapo uwanjani siku ile, walipata nafasi ya kukutana kama si kuwaona wachezaji wenye majina makubwa katika soka ya Tanzania, waliowahi kutamba enzi zao kutokana na kandanda walilokuwa wakilionyesha.
Wachezaji walioonekana uwanjani siku hiyo, ambao enzi zao walikuwa ni moto wa kuotea mbali, ni Issa Manofu, Abubakar Kombo, Bakari Idd, Tom Kipese ‘Uncle Tom’, Ramazani Wasso, Said Kokoo, Boniface Pawasa, Said Sued, Shekhan Rashid, Madaraka Selemani ‘Mzee wa Kiminyio’, Kamba Lufo, Bita John, Yussuf Macho ‘Musso’ na Mrisho Moshi.
Wengine ni Peter Manyika, Omar Kapilima, Mwanamtwa Kihwelo, Chibe Chibindu, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Shaaban Ramadhani, Waziri Mahadhi, Idd Moshi, Steven Nyenge, Deo Lucas, Sekilojo Chambua, Ephraim Makoye, Salvatory Edward ‘Doctor’, Akida Makunda, Ally Yussuf ‘Tigana’, Ally Mayai ‘Tembele’, Kudra Omar, Edibily Lunyamila na Omar Changa.
Mbali na hao, pia walikuwapo Wakenya Edwin Mukenya na Ben Mwalala ambao wataonekana katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao wakiwa na Coast Union iliyopanda daraja msimu huu, akiwamo nyota Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye kwa sasa yupo benchi kutokana na kukosa timu ya kuichezea.
Pamoja na kuacha soka kutokana na sababu mbalimbali, zaidi ikiwa ni umri kuwatupa mkono, baadhi ya nyota hao wa zamani, walionyesha kuwa bado wamo, wakitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki.
Nikianza na kipa wa Simba Veterans, Issa Manofu, kipa huyo nadhani siku ile aliwaonyesha Watanzania nini wanakosa kwa sasa. Manofu alionyesha umahiri mkubwa wa kudaka mipira, akiokoa hatari kadhaa langoni mwake, zilizoelekea kuwa mabao.
Kwa kiasi kikubwa, Manofu ndiye aliyeamua matokeo ya mchezo ule kwa kuinyima Yanga Veterans mabao kutokana na mikwaju ya akina Ben Mwalala, Edibily Lunyamila na wengineo. Ama kwa hakika, Manofu alionyesha utofauti mkubwa na baadhi ya makipa wa sasa.
Mchezaji mwingine aliyefanya mambo siku ile, alikuwa ni beki wa kati wa Simba Veterans, Boniface Pawasa ambaye alionyesha umahiri mkubwa wa kukaba, kuokoa hatari na hata kuwapanga wenzake kuhakikisha Manofu anakuwa salama muda wote wa mchezo huo.
Kikubwa zaidi, uwezo wake wa kutumia nguvu na akili pale ilipohitajika, uliwakumbusha mashabiki enzi zake alipokuwa aking’ara na Simba, uwezo ambao pia walikuwa nao mabeki waliowahi kutamba hapa nchini kama George Masatu, Said Mwamba ‘Kizota’ na wengineo.
Tangu Pawasa alipopotea katika soka ya Tanzania, hakuna beki aliyewahi kutokea mwenye sifa kama zake. Kwa mfano, ukimwangalia ebki tegemeo wa Tanzania kwa sasa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yeye ni hodari wa kukaba, kutumia nguvu inapohitajika na kuondosha hatari katika eneo la hatari.
Tatizo laek na wengineo kama Juma Nyoso na Kelvin Yondani, ni uwezo wa kuwapanga wenzake, kwa maana ya kuwakumbusha majukumu yao, ili aweze kuwa ‘mtu wa mwisho’.
Kama ilivyokuwa kwa Pawasa, kiungo wa Yanga Veterans, Waziri Mahadh, naye aliwaonyesha mashabiki wa soka nchini nini wanapungukiwa kutoka kwa viungo wao wa sasa.
Mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa vivutio katika mchezo huo, zaidi ikiwa ni kutokana na uwezo wake wa kubadili uelekeo wa mchezo na kutoa pasi za ‘ukweli’, kitu kilichokosekana kwa idadi kubwa ya viungo wa siku hizi.
Ukitoa viungo kama Mohamed Banka, Godfrey Bonny, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Mwinyi Kazimoto, viungo wengi wamekuwa wakishindwa kuwapa burudani mashabiki, kama iliyotolewa na Mahadh au kiungo mwingine aliyechezea Yanga Veterans, Salvatory Edward.
Na hilo ndilo tatizo linalowafanya washambuliaji wa sasa kushindwa kufunga mabao, kutokana na kukosa ‘wapishi’, kwa maana ya viungo wa kuwapa pasi maridadi za mwisho, tena za kwenye njia.
Wachezaji wengine waliowatia kiwewe mashabiki katika mchezo ule wa Machi 19, ni Mukenya, Shekhan Rashid, Madaraka Selemani ‘Mzee wa Kiminyio’, Haruna Moshi ‘Boban, Yussuf Macho ‘Musso’, Peter Manyika, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Shabani Ramadhani, Sekilojo Chambua, Ephraim Makoye, Ally Mayai ‘Tembele’, Ben Mwalala na Edibily Lunyamila.
Katika mchezo huo, timu zilipangwa kama ifuatavyo:
Simba: Issa Manofu, Abubakar Kombo/Bakari Idd/Tom Kipese ‘Uncle Tom’, Ramazani Wasso, Said Kokoo, Boniface Pawasa, Edwin Mukenya, Said Sued, Shekhan Rashid, Madaraka Selemani ‘Mzee wa Kiminyio’/Kamba Lufo, Bita John/Haruna Moshi ‘Boban na Yussuf Macho ‘Musso’/Mrisho Moshi.
Kocha: Madaraka Seleman
Yanga: Peter Manyika, Omar Kapilima, Mwanamtwa Kihwelo/ Chibe Chibindu, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Shabani Ramadhani, Waziri Mahadhi/Idd Moshi, Steven Nyenge/Deo Lucas, Sekilojo Chambua/Oscar Makoye, Salvatory Edward ‘Doctor’/Akida Makunda, Ally Yussuf ‘Tigana’/Ally Mayai ‘Tembele’, Ben Mwalala/Kudra Omar na Edibily Lunyamila/Omar Changa.
Kocha: Ken Mwaisabula ‘Mzazi’.
Na kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa mchezo ule, Seleman Mathew, uhondo ulioonyeshwa na wakongwe hao, utahamia Dodoma Machi 27, mwaka huu ili kutoa fursa kwa wakazi wa huko kushuhudia nini wanakikosa kutoka kwa wachezaji wao wa sasa.
“Tumeamua kuwapelekea wakazi wa Dodoma mchezo huo ili waweze kuona vitu anadimu vilivyokuwa vikionyeshwa na wachezaji wao wa zamani,” alisema Mathew.
 
Imenikumbusha mbali sana mkuu
kila nikikumbuka wachezaji wa zamani naumia sana
serikali haikuwa na mwamko wakati ule bana
 
Mkuu mbona Kipindi kina Powasa wanacheza tulikua tunasikia Mpira ulikua zamani. Leo tunaambiwa Mpira ulikua Enzi za akina Powasa, Naona kama mnatuchanganya kidogo
 
ukilinganisha vipindi viwili....hiki na cha akina pawasa cha akina pawsa kilikuwa bora...na pia ukilinganisha cha akina pawasa na cha akina CHUMILA/MKAPA/PAZI/MKANDAWILE/MAMBOSASA et al cha akina pawasa si lolote kwa kile ....! tupo pamoja hapo?
 
Ally Mayai bado kijana, mara hii kaingia kundi la veterans? amecheza muda mfupi sana huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom