Paul mabuga- Tuongee asubuhi.

Huyu ni moja ya Makanjanja, yeye anawakilisha mwajiri wake zaidi ambaye ni CCM damudamu na anasahau kuwa ukiwa mtangazi hutakiwi kuonyesha itikadi yako ya kisiasa kwani unaowatangazia wengine siyo wafuasi wa chama chako.
 
Paul Mabuga,
I always respect your presentations on star tv's live programs, kuwa na utayari wa kurekebishika punde unapoteleza...kumbuka upo kwenye kioo cha jamii. Hali hii iliwatokea pia akina Yahya Mohamed & Baruan Muhuza kipindi cha 2010 national elections, lakini kwa sasa WAMEBADILIKA na kurejea kwenye ubora.
Hivyo Mabuga ipokee changamoto na ifanyie kazi, hopefully utafaulu na audience kukurejeshea heshima. UUNGWANA NI VITENDO, usichukie changamoto mkuu.

SHIME.
 
Huyu jamaa naamini jinsi alivyi hangaika n a maisha ndicho kinachomsumbua, ametuka mbaali sana hadi hapo alipo lazima ajikombe kwa wakubwa, hiyo ndiyo tabia yake toka alipokuwa mwalimu wa shule ya msingi shinyanga then sekondari ya buluba......
Hatumii sana kichwa kwa kuendekeza kujikomba......
Ugonjwa unaomsumbua ni kudhani anajua kila kitu.............DK Slaa alishawahi kumfokea kama mtoto kwa ujinga wake.....
 
Paul Mabuga,
I always respect your presentations on star tv's live programs, kuwa na utayari wa kurekebishika punde unapoteleza...kumbuka upo kwenye kioo cha jamii. Hali hii iliwatokea pia akina Yahya Mohamed & Baruan Muhuza kipindi cha 2010 national elections, lakini kwa sasa WAMEBADILIKA na kurejea kwenye ubora.
Hivyo Mabuga ipokee changamoto na ifanyie kazi, hopefully utafaulu na audience kukurejeshea heshima. UUNGWANA NI VITENDO, usichukie changamoto mkuu.

SHIME.
Hapo kwenye RED. Kumbuka Jenerali Ulimwengu katika makala zake wakati wa uchaguzi alisema waandishi wengi unapofika wakati wa uchaguzi huwa wanachukua akili zao za kawaida wanaziweka kando, na kuvaa akili za kiuendawazimu hadi uchaguzi unapoisha. Kisha uchaguzi ukiisha wanazivua akili za kiuendawazimu na kuzirejesha akili zao za kawaida. Hao jamaa ndivyo walivyokuwa wakati wa uchaguzi kama unabii wa Jenerali Ulimwengu unavyoeleza
 
Kipindi kilikuwa kizuri nilisikitika sana umeme ulikatika kabla ya Kipindi kuisha mimi nilipenda Paul Mabuga alivyooanza kwa kupata tafsiri za kisheria kuhusu maandamano kufanyika, na kama maandamano kufanyika ni uvunjwaji wa sheria kwa kweli wale vijana waliokuwa naye Mwanza walinifurahisha jinsi walivyokuwa wanaenda na muongoza mjadala
Lakini wasikilizaji tutambue kuwa kila mtangazaji anastyle yake kwa hiyo hawawezi wote kuwa na mtindo mmoja mtindo wa Paul Mabuga ni wa kuprovoke,au kudadidisi kwa undani na kumfanya mgeni wake aweze kuibua mambo mengi zaidi
Tatu mimi napenda jinsi anvyoingia kwenye mazungumzo Paul Mabuga anakuwa na mgeni wake kwa karibu ni mcheshi na anakumbukumbu ya vitu vingi anajitahidi kwa kweli
Kiujumla waandishi na watangazaji wa Star TV wanajitahidi sana kila mara nasema tangu uchaguzi mimi nimekuwa teja lao
Paul chukua hii mipasho kama challenge lakini pia ufurahie kwamba kumbe wengi walisikiliza kipindi chako
 
Nachoamini ni kuwa changamoto ni jambo la kawaida kwa binadamu! Kwangu mimi hakuna hoja ya kipuuzi. Lakini pia binadamu kutofautiana katika fikra ni jambo la kawaida, fikra zinajengwa na misingi minigi, baadhi ni pamoja na Imani, utashi na uelewa. Siwezi kuhukumu kipi kinawasukuma baadhi kutoa hoja na maoni waliyonayo, lakini ni mara chache misingi hii ikafanya katika hali ya usawa na kwa pamoja,lazima msingi mmoja utakuwa juu zaidi ya mingine. Kama binadamu pia kuna hatua za kujifunza katika jambo, kwanza naona, Napata uzoefu, maarifa mapya kama yapo na kisha napambanua, na hii ni lazima.
Kuibuka na fikra na kushtumu ama kulalamikia jambo ambalo una uewlewa nalo ama huna pia siyo dhambi, lakini uendeshaji na utayarishaji wa vipindi vya majadiliano una misingi na maadili yake. Unaweza kufanya kama wengine wanavyotaka uwafurahishe, nap engine fikiria ukifanya kuegemea upande mwingie kuwauzi hali itakuwaje. Lakini fikiria ukaendesha mjadala ambao wageni wako wengi wa upande mmoja, lakini unatakiwa kuwa na muungwana akilalamika kwa sababu umeuliza jambo ambalo yeye linamkirihisha.
Najua kwa nini zinakuwepo hoja kama zinazotolewa, lakini naziheshimu na nachukua kama changamoto.
Pengine ni nadra kwa mtu kujibu wazi malalamiko kama hivi, lakini nawapeni hongera mnaotoa malalamiko, wengine nawafahamu na wengine siwajui lakini Shukurani na Kwaresma njema.

umejibu vyema Paul Mabuga, yafanyie kazi hayo mambo yao.
 
Hivi kwa nini malalamiko haya yanatokea pale tu huyu jamaa anapoendesha kipindi ambacho kinaihusu CHADEMA sijasikia akilalamikiwa katika mada nyingine! Aanauwauzi nini Wana Nzengo na hasa wale ambao wanatarajia kugombe ubunge kwa tiketi ya CDM 2015?

Lazima malalamiko yaje pale uendeshaji wake wa kipindi unapoanza kuegemea ule upande usiopendwa na wengi. mada zingine hazina tija ndiyo maana watu hawahangaiki nazo na pengine hata mtangazaji mwenyewe hafanyi kama anavyofanya a anapokuwa katika masuala ya siasa.

Ujue vile vile watu sasa hivi maisha yao yanaguswa zaidi kuliko katika kipindi chochote katika historia ya Tz, hivyo hakuna anayependa mambo yaende hovyo hovyo
 
Nimekiona kipindi, lakini , je usalama wa mtangazaji unakuwa wapi ikiwa mgeni anakaribia kuzunguza jambo ambalo linaweza kuwa kashfa ama tusi kwa namna fulani, lakini mbona nimeona wageni walikuwa wanapewa kauhoja za kuchokozwa ili waongee ... lakini bado licha ya kipindi kuegemea upande mmoja lakini bado tumepata hoja za upande mwingine... maanake vingine kingekuwa kipindi cha kwa ajili ya Cdm kama baadhi ya watu wanavyotaka.

Ufafanuzi ulikuwa mrefu, nafikiri kama hatujui kazi za watu tusijisemee kama vile tunabishana kwenye matapu tapu

Wewe mtu wa ajabu sana, kama hukuweza kuona kasoro kwenye kipindi cha leo basi una matatizo, usalama wa host unahatarishwa vipi kwa mgeni kusema matusi, halafu nyie bwana watu wakiongea ukweli ndio wanatukana? Huyo mabuga ni uozo tu nashangaa kwa nn hawamtoi hapo, yani uwezo wako wa kufikiri ni hafifu sana, sikutukani nakwambia kweli. Kwahiyo kwa kuwa wewe unakunywa mataputapu unadhani wote tunakunywa?
 
Mimi ningekuwa ndiyo huyu mtangazaji na hizi baadhi think tank za mataputapu ambazo zinababia mambo na hata kiswahili cha kubabia kweli ningenyoosha mikono na kuvaa khaki kisha vidole viwili juu na kutoa heshima ya peoples for power kipindi chote angalau wenye uozo wa mawazo waridhike.
 
Nimeongea na mtoto wake na hata baadhi wanaomfahanu wewe uliyejidai kumfahamu naona umetokota! Huku Buluba wala primary hakupita! Na wewe ni great thinker! Nimo humu kwa miaka mitatu ni mara kwanza nashuhudia mazuzu na wazushi kupindukia! Hivi sifa ya forum hii kweli italindwa kweli kupitia fikra 'pevu za watu hawa! Au tuanzishe kuhamia kwa real great thinkers!
 
Hata mimi mabuga nashindwa kumuelewa anaita watu studio halafu hataki wajieleze kwa kina kuhusu masuala wanayoyajua yeye anawakatishakatisha tu,naomba mwache mtu azungumze kwa sababu sisi watazamaji tunapata elimu pale kupitia hawa watu unao waita studio sasa wewe ndio unakuwa muongeaji kuliko wao sasa umewaita wa nini ?na ili tuwaelewe lazima umpe nafasi azungumze mpaka amalize anachotaka kusema hawa wengine ni wahadhiri chuo kikuu wanajua wanachotaka kusema la sivyo siku nyingine hawatakuja mkiwaita,hasara itakuwa ya kwetu sisi watazamaji ambao tunaangalia kipindi hicho na hawa watu mnaowaita studio wametufungua sana sana macho na masikio na tumeelewa vitu vingi kupitia vipindi vyenu.nampongeza angello moleka ,samadu na anayeongoza kipindi cha jumamosi asubuhi.
 
ndugu yangu mabuga mi nakusihi achana na kina mgoyangi,chuki naona wao wanaleta mapambano. mtoa thread amerefer hata matukio ya nyuma acha kipindi ulichoendesha na kina greyson ambacho sasa ndicho kimeibua thread. nakusihi ujitizame na kujirudi si vibaya ukaonana pia na hao wanaotajwa, yahaya,baruan,samadu,mwaleko, binadamu hatujakamilika na mtu huishi kujifunza,kuhusu ushabiki wa vyama lazima una chako ila unapokuwa kazini uwe neutral. binafsi c mtazamaji wa star tv wala hata cjui habari zake,lkn kwa thread na watu wanavyochangia inaonekana una kajitatizo kidogo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom