Paul Chizi wa ATCL asimamishwa kazi

Wote walikuwa wanakaimu sijui wenye vyeo vyao wako safarini au wamestaafu!!!
 
Duuuh kweli afadhali rais asingevunja baraza la mawaziri maana mawaziri wa sasa wana sifa balaa na hii itakifanya chama cha Mapindizi kung'ara na kufanya kazi 2015 kuwa pevu tena.

sasa mkuu unataka wafanyeje mkuu?
 
Too bad for them. Lakini kama kuwamwaga kutalinusuru shirika hili, ni sawa.
Swali la uzushi: Mwakyembe kamtoa Chizi kamweka Lusajo, je ni ukabila unafanya kazi?

Lusajo ni jina la Kinyakyusa lakini je tuna uhakika jamaa ni Mnyakyusa?...jaribu kukumbuka jina la yule comedian wa Orijino Komedi "Mpoki Mujuni", ana jina la Kinyakyusa lakini yeye ni Mhaya
 
Duuuh kweli afadhali rais asingevunja baraza la mawaziri maana mawaziri wa sasa wana sifa balaa na hii itakifanya chama cha Mapindizi kung'ara na kufanya kazi 2015 kuwa pevu tena.

Mchadema nini tena mmeanza kuchanganyikiwa na utendaji wa serikali sikivu ya CCM.
 
Mmh! isije ikawa hizi speed zote ni povu la ndovu baridi ktk glass baada ya muda linaisha...
 
Lusajo majini ya kule anakotoka Mwakyembe. Naona ndiyo undugu unaanza vile. Kama kawaida ya CCM!
 
Kinachonishangaza ni jinsi wakurugenzi karibia wote walikuwa wanakaimu kwa karibia mwaka mzima. Lazima kuna kitu mheshimiwa waziri amegundua kulikuwa na walakini katika uteuzi wao.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nice move Dr. Mwakyembe, tunasuburia TRL/TRC pale nao waondoke otherwise itakuwa shida treni zetu.
 
Nimemfurahia sana Kagasheki.. he is very serious hata kwenye maongezi unaona kabisa anajua nini kinatakiwa kufanyika katika wizara yake. Sisi kazi yetu ni kutuo tadhmini tu baada ya muda. Nguvu ya soda tutawaambia na watendaji tutawapongeza!!
 
Jamani hawa mawaziri hawa wezi kushikamana na kumsimamisha kazi kikwete?
Inaonekana lazima kuna kifungu flani cha sheria kinacho weza kutumika.
 
Haya watu wa Mbeya kaeni mkao wa kupewa vyeo,mambo ndio yameanza hivyo,sitoshangaa huko mbeleni hiyo wizara ikawa na Wanyakyusa tu,kama ilivyokuwa wizara ya fedha ya Mramba na Meghi.
 
Kwa nini serikali isianze sasa utaratibu wa kutangaza nafasi za kazi kama hii na kushindanisha watu kwa competency yao badala ya hizi siasa? Watu wafanyiwe interview na wafanye kazi kwa contract tena based on perfomance. Ukishindwa kufukia malengo, you are out.

Baada ya hapo ningetaka Mwakyembe afukuze mtu/watu TAZARA na TRL. Kuna watu hawatakiwi. Then aende bandarini, nako kuna watu wa kutoa hasa TPA. Yule aliyesema CCCC wanafaa aondoke. CCCC ni corruption pure.
 
Jamani hawa mawaziri hawa wezi kushikamana na kumsimamisha kazi kikwete?
Inaonekana lazima kuna kifungu flani cha sheria kinacho weza kutumika.

hahaha mkuu sidhani kama kuna kifungu chochote kama hicho....tatizo CCM wote wanafiki na ni moja ya dhambi inayowatafuna, wapo radhi kulindana na huku nchi ikienda mrama. Unafiki huu unaanzia chini kabisa kwenye ngazi za mashina, mara nyingi utawaona wakati wa kampeni na mashati yao ya kijani kumbe hakuna lolote...sijui imerogwa hii mijitu mweeh!
 
Back
Top Bottom