Paul Chagonja atimuliwe Polisi

Mtu mzima kutoa maamuzi yaliotawaliwa na jazba na ushabiki wa kisiasa hata haipendezi..kwa akili yake alichoweka kichwani ni maandamano ya CDM..taka taka kabisa!!
 
inawezekana akapatikana juha alie afadhali mkuu.. Imagine ametumwa kwenda kuchunguza.. lkn ameanza kutetea kabla ya kutoa nyayo zake hapa kwenda huko..! ati polisi wamefundishwa na kwa hiyo hawawezi kuua raia.. damn wanakera sana hawa..

huyo bora arudi tu Dar,sioni anachoenda kufanya wakati tayari jibu anayo kwamba wale wananchi walioandamana walikuwa wahuni.yaani tayari amesha side upande mmoja.hopeless cop.
 
Mbona alianza kuongea pumba kabla hata hajafika eneo la tukio? Kwani hata kama lilikuwa kundi la wahuni polisi bado wanayo nguvu ya kuua wahuni bila ya sababu za msingi? Sioni kama tuna viongozi tena ila limebaki kundi la wazee wanajitengenezea pensheni.

humo ikulu alikuemo ****** au mamake na huyu changoja, hao wahuni anaowasema walikuwa na silaha za moto? Hv jeshi letu la police huwa awana rubber bullets.useless cop.
 
Ametumwa kwenda kuchunguza nini wakati tayari ana majibu ya kazi anayotakiwa kufanya. Hawa wanatafuna fedha za walipa kodi bure na hakuna chochote cha maana watakachofanya ama kushauri
 
Toka lini mtu asiyekuwa na uelewa wenyewe wa uchunguzi akafanya uchunguzi hapo mnategemea nini?
Kesi ya ngedere unamplekea kima
 
huyu polis anafikira wananchi wote hawajakwenda shule kama yeye unatoa taarifa kabla hujafika eneo latukio hata huko ccp moshi am not sure kamaamewahi kufika kwenye mafunzo cheo chakununua haya ndio matokeo yake wewe sacp unaongea utumbo hatahujafika kwenye tukio ulijuwaje kama
Niwahuni? Na wahuni sio watanzania wezetu jee katiba inasema wahuni wauliwe?
 
Inasikitisha kama kweli yeye ndio katumwa kuongoza jopo,IGP Mwema afanye maamuzi ya kuteua mwingine yeye arudi DAR na pia achukuliwe hatua za Kinidhamu[/QUOTE

Hawezi fanya hivo,,hatuna utamaduni huu,japo kwa wenzetu huko kauli hiyo ilishakuwa kubwa mno ya kumwajibisha mtu! lkn Mwema nae bingwa wa magumashi,, iko wapi report ya tume iliyochunguza uhalali wa Jerry Muro kumiliki Pingu, ile ya vigogo(charlesmkumbo) waliotuhumiwa kupanga njama za kumbambikia drugs mtoto wa mebgi? nk?




I always wonder what for are these committees, i say this because i have never seen a successful committee in Tanzania. Natamani katiba mpya ianishe kuwa hakutakuwa na kamati.
 
hii nchi ilipofikia hakuna mtu anaweza kufukuzwa kazi hata afanye uzembe wa aina gani aibe, afanye ufisadi wa ajabu wala hakuna kitu!! watu walipiga kelelel Jairo, luhanjo, Mponda, ngeleja, malima, nkya, wameguswa?? serikali ya kishikaji na kujuana ndugu!!!
 
Polisi gani lina mashavu makubwa, tumbo na wowowo mpaka akili zote zimehamia kwenye masaburi. Bonge la Dog likiambiwa shika linakimbiza tu, akili imehamia miguuni........
 
raia mwema ni yule anayetii sheria kwa ustawi wake na wawatanzania wote hata kama rais angekuwa Slaa lazima kuwe na rule of law na police ndiyo law enforcers msilete siasa kwenye sheria za nchi mtakwisha.
 
raia mwema ni yule anayetii sheria kwa ustawi wake na wawatanzania wote hata kama rais angekuwa Slaa lazima kuwe na rule of law na police ndiyo law enforcers msilete siasa kwenye sheria za nchi mtakwisha.

mkuu.. rule of law iwe pande zote.. kosa la kuandamana haliadhibiwi kwa kuwaua raia bali ni kuwakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.. unapoua unakuwa umevunja sheria na unapaswa na ww uadhibiwe.. ielezee kauli ya kiongozi wa kikosi cha kwenda kufanya uchunguzi wa mauaji kuanza kutamka maneno ya kuwashutumu raia.. haki itatendeka hapo..? hakuna siasa hapo..
 
Uchunguzi wa kutuliza hasira za wananchi ili wasahau. Nchi hii wote tulishaonekana wajinga.
 
Namkumbuka yule mzee marehemu wa Libya aliyewaita wananchi waliokuwa wanaandamana kupinga utawala wake kuwa ni mende na mapanya siku yake ilipofika mnafahamu alifanyiwa nini! Sasa siku ya Chagonja ikifika sijui wananchi watamfanyaje!!
 
Amelewa madaraka huyo anastahili astahafishwe kwa manufaa ya umma, kama kiongozi wa umma anakwenda kwenye uchunguzi alishakuwa na conclusion kwamba walioandamana ni wahuni ni bora asiende[/QUOTE]

Ni lazima aende akaangalie vijana wake wanavyojua kutumia risasi za moto kuua raia halafu atawapandisha vyeo kwa kazi nzuri ya kuua raia wasiyokuwa na hatia wala silaha!!!
 
Soma habari hii halafu utaelewa kwa nini chagonja anapaswa kufukuzwa kazi polisi..

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta saidi mwema ametuma kikosi cha maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hiko, kikiongozwa na Mkurugenzi wa operesheni na mafunzo kamishna Paul Chagonja kwenda mjini songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo.
Chagonja akiongea na mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwamo ikulu ndogo na ofisi ya mkuu wa mkoa.
Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze ednapo haoni kkama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.
"maandamano yamani watu wanavamia ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"
"sijafika huko ndio naelekea lakini yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka waachiwe? Kuweni wazalendo , miswe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka uingereza, hii ni nchi yenu"
Alifafanua kwamba maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano. "lakini siyo maandamano yale, hayakuwa na kibali chochote wahuni tu wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi"
Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema; "ucifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue ovyo risasi za motokwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia, lakini watu wanavamia ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa magari ya polisi, hapo kuna amani kweli?"
Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki na badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza: "kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu"

Source: Mwananchi
Ni kweli kabisa tuwaache POLISI wafanye kazi yao! WaTZ hawapendi kuambiwa ukweli!!!!!!
 
Back
Top Bottom