Patroli, dizeli, mafuta ya taa bei juu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
EWURA(44).jpg

Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)


Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za aina zote za mafuta za jumla na rejareja zitakazoanza kutumika kuanzia leo, ikiwa ni siku mbili tangu matumizi ya kanuni ya zamani ya ukokotoaji wa bei ya mafuta kuisha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ewura jana, kutokana na kanuni hiyo mpya, kuanzia leo jijini Dar es Salaam, bei ya rejareja ya petroli itakuwa Sh. 1,956 wakati bei ya dizeli itakuwa Sh. 1,977 na bei ya mafuta ya taa itakuwa Sh. 1,963 kwa lita.

Katika bei ya jumla, petroli itakuwa Sh. 1,881.92, dizeli (Sh. 1,903.04) na mafuta ya taa (Sh. 1,888.59).
Miongoni mwa mambo muhimu yaliyomo kwenye kanuni hiyo mpya, ni pamoja na tozo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Tozo hiyo imeongezeka kutoka dola za Marekani 8.30 hadi dola za Marekani 10 kwa ujazo wa tani moja, pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Pia Ewura itaendelea kuchapisha bei kikomo kwa wafanyabiashara wa jumla na rejareja na kwamba taasisi zote zinazotoza tozo kwenye kanuni hiyo, zitalazimika kutoza kwa mujibu wa maagizo ya kanuni hiyo.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom