Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Naomba msaada kama kuna mtu ana idea ya ufugaji bata kibiashara. Ninashukuru kwa mawazo chanya

MORIA... upo wapi .... I have the same idea ya kufuga in large scale kwa matunzo ya kisasa zaidi .... nimejaribu kuwatunza watoto 11 wa bata walioanguliwa mwezi wa 7 kwa kuwapa broiler starter in first three weeks na baade kuwapa growers mash ikichanganywa na portion ya pumba za mahindi na matokeo ni mazuri sana ... watoto hawa sasa ni wakubwa sana with a high yield in growth

ninachotaka kufanya sasa hivi ni kununua mayai ya bata kwa wafugaji mbalimbali na kuyapeleka kuanguliwa kwa incubator machine .... naanza na mayai 50 ... then from there I can propel the project well

kumbuka bata wanakuwa vizuri kwa malisho ya majani (grazing) na maji kwa ajili ya preening
 
Soko lake likoje? Usije ukajikuta unafuga wengi halafu unaishia kula mwenyewe,umeshafanya tafiti ya soko?
 
bata yupi mnaemuongelea?

Huyu hapa

thumbnail.aspx
 
Facilitator kama ni huyu maji hamna shida, ni rahisi sana kuwafuga kwasababu hawahitaji utaalamu wowoteni zaidi ya kuwafungia kwenye uzio na kuwawekea madimbwi ya kuogelea na vyakula vyenye mchanganyiko wa maji kama uji, wanakula kila aina ya chakula kama kiti na huwa hawaumwi hata siku moja ila sema vifaranga wake siku za mwanzo huwa wabovu sana na rahisi sana kufa.. Uzuri mwingine huwa wanatotoa kwa njia za asili na wanatoa watoto kama 8+.
soko lake linasumbua
 
Last edited by a moderator:
MORIA... upo wapi .... I have the same idea ya kufuga in large scale kwa matunzo ya kisasa zaidi .... nimejaribu kuwatunza watoto 11 wa bata walioanguliwa mwezi wa 7 kwa kuwapa broiler starter in first three weeks na baade kuwapa growers mash ikichanganywa na portion ya pumba za mahindi na matokeo ni mazuri sana ... watoto hawa sasa ni wakubwa sana with a high yield in growth

ninachotaka kufanya sasa hivi ni kununua mayai ya bata kwa wafugaji mbalimbali na kuyapeleka kuanguliwa kwa incubator machine .... naanza na mayai 50 ... then from there I can propel the project well

kumbuka bata wanakuwa vizuri kwa malisho ya majani (grazing) na maji kwa ajili ya preening

Nipo mtu wangu..nilijaribu kutafuta mayai ya bata ilikuwa ngumu...nashukuru kwa dondoo, ila mdizi nahitaji niwe mfugaji kwa maana ya kujua wanalalia mara? kwa mwaka,wanavunwa baada ya muda upi etc.
 
Facilitator kama ni huyu maji hamna shida, ni rahisi sana kuwafuga kwasababu hawahitaji utaalamu wowoteni zaidi ya kuwafungia kwenye uzio na kuwawekea madimbwi ya kuogelea na vyakula vyenye mchanganyiko wa maji kama uji, wanakula kila aina ya chakula kama kiti na huwa hawaumwi hata siku moja ila sema vifaranga wake siku za mwanzo huwa wabovu sana na rahisi sana kufa.. Uzuri mwingine huwa wanatotoa kwa njia za asili na wanatoa watoto kama 8+.
soko lake linasumbua

Umemaliza mkuu.
 
Soko lake likoje? Usije ukajikuta unafuga wengi halafu unaishia kula mwenyewe,umeshafanya tafiti ya soko?

Soko halina mjadala bata anapendwa sasa..hawatumii madawa na nyama tamu tena ya kutosha.
 
mkuu...asante sana...nyama ya bata ni tamu sana especially ikitengenezwa in dry form... i love this stuff ...ukitengeneza mamichuzi imekula kwako
aende tanga akapikiwe pilau akitafuna huyo ndege.... lazima ajing'ate vidole... mkuu hatuonani...!!
 
Wanajamii ,
Kama kuna mtu anautaalamu wowote wa ufugaji wa bata kibiashara naomba anijuze.Hii ikiwa ni pamoja na soko lake na management yake kwa ujumla.Mimi ni mwajiriwa na nipo hapa Dare salaaam nipo interested sana na ufugaji.Nawasilisha.

Bata ni kama walivyo jamii nyingine ya ndege yaani poultry mfano kuku,kanga,Bata mzinga,njiwa,kwereakwerea, nk,.Mahihitaji yao yanafanana kabisa na yale ya jamii nyingine ya ndege.Chakula ambacho kuku anakula hata bata anakula. Bata wakilishwa vyakula vya kuku wa kisasa wanakua haraka na uzito wao huu mkubwa kwa muda mfupi .

Ufagaji wa bata utakuwa mzuri kama utakuwa aidha na bwawa au mto uliopitishwa shambani kwani Bata anahitaji maji kwa asilimia 90.

Magonjwa yote anayopata kuku au jamii nyingine ya ndege pia bata hupata.Lakini ugonjwa unaowasumbua zaidi ni Mafua na kipindupindu.Bata ni wastahimilivu wa kupata magonjwa lakini wakipata ugonjwa uwezo wa kustahimili kwao huwa ni mdogo sana ,mara nyingi huwa wanakufa hovyo hivyo umakini unahitajika.
Masoko ya Bata yako ya kutosha hasa kwenye mahoteli makubwa ya mijini.Wageni wengi sana wanahitaji nyama ya bata,na kutokana uzalishaji wake kuwa mdogo ndio maana unakuta bei ya bata haikamatiki.

Ukijuhusisha na ufugaji wa bata,ndani ya muda mfupi,uwezekano wa kuwa tajiri ni mkubwa sana.Hebu tazama Tanzania sijasikia kampuni yoyote inayojihusisha na utotoreshaji na uuzaji wa vifaranga wa bata.Asikudanganye mtu nyama ya bata ni tamu sana.Tatizo letu watanzania ni mazoea mazoea.Tumezoea zaidi nyama ya Ng'ombe,mbuzi na kuku.Lakini nyama ya Kondoo,bata na kanga si maarufu sana.Kama mtu ukaaanzisha miradi ya ufugaji wa wnyama kama kondoo,bata na kanga wakapewa promo nadhani biashara itafanyika.Ebu fikiria hoteli zinaagiza bata kutoka magereza bwawani,na unakuta mahitaji yanakuwa makubwa kuliko uzalishaji.
 
Sipendi kufuga bata kwa sababu heshima yao sifuri, na akuna bata ambae amebalehe au kuvunja ungo atauona ufalme wa mbingu. Kila wakati wao ni kunanii tuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom