Wanajamii,
Kama kuna mtu ana utaalam wowote wa ufugaji wa bata naomba tupeane elimu ili tuweze kufuga kisasa kwa ajili ya kutengeneza kipato.
===============
Kama kuna mtu ana utaalam wowote wa ufugaji wa bata naomba tupeane elimu ili tuweze kufuga kisasa kwa ajili ya kutengeneza kipato.
Naombwa kujuzwa wana jamvi na kupewa darasa kuhusu elimu ya ufugaji bata
1. Wapo aina ngapi?
2. Wanaatamia mayai kwa mwaka mara ngapi?
3. Soko halisi likoje kwa mfano kama naishi DSM
4. Vyakula wanavyokula kama nikitaka kuwafuga kibiashara
5. Je, naweza kutotoleshea mayai yao kwa kutumia incubator?
Kama kuna mtu anawafuga naomba anipe mawasiliano yake niweze kupata ujuzi kwa vitendo kwake. Nashukuruni na nawatakia mwisho mwema wa mwaka.
Wenu katika ujenzi wa taifa.
Kifuniko
===============
Bata ni kama walivyo jamii nyingine ya ndege yaani poultry mfano kuku,kanga,Bata mzinga,njiwa,kwereakwerea, nk,.Mahihitaji yao yanafanana kabisa na yale ya jamii nyingine ya ndege.Chakula ambacho kuku anakula hata bata anakula. Bata wakilishwa vyakula vya kuku wa kisasa wanakua haraka na uzito wao huu mkubwa kwa muda mfupi .
Utagaji wa bata utakuwa mzuri kama utakuwa aidha na bwawa au mto uliopitishwa shambani kwani Bata anahitaji maji kwa asilimia 90.
Magonjwa yote anayopata kuku au jamii nyingine ya ndege pia bata hupata. Lakini ugonjwa unaowasumbua zaidi ni Mafua na kipindupindu.B ata ni wastahimilivu wa kupata magonjwa lakini wakipata ugonjwa uwezo wa kustahimili kwao huwa ni mdogo sana, mara nyingi huwa wanakufa hovyo hivyo umakini unahitajika.
Masoko ya Bata yako ya kutosha hasa kwenye mahoteli makubwa ya mijini. Wageni wengi sana wanahitaji nyama ya bata na kutokana uzalishaji wake kuwa mdogo ndio maana unakuta bei ya bata haikamatiki.
Ukijuhusisha na ufugaji wa bata, ndani ya muda mfupi, uwezekano wa kuwa tajiri ni mkubwa sana. Hebu tazama Tanzania sijasikia kampuni yoyote inayojihusisha na utotoreshaji na uuzaji wa vifaranga wa bata.
Asikudanganye mtu nyama ya bata ni tamu sana. Tatizo letu watanzania ni mazoea mazoea. Tumezoea zaidi nyama ya Ng'ombe, mbuzi na kuku. Lakini nyama ya Kondoo, bata na kanga si maarufu sana.
Kama mtu ukaaanzisha miradi ya ufugaji wa wanyama kama kondoo, bata na kanga wakapewa promo nadhani biashara itafanyika. Ebu fikiria hoteli zinaagiza bata kutoka magereza bwawani na unakuta mahitaji yanakuwa makubwa kuliko uzalishaji.