Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Pia unaweza kufuga Samaki bwawa la Chumvi. Kuna samaki wa maji chumvi ambao wanafugwa kama vile kambamiti (prawns), koazi (milkfish), perege wa maji chumvi. Hawa ndio kwa sasa wanafuga hapa nchini.

Ila nimefuatilia nchi nyingine wana teknolojia ya kufuga zaidi ya hao kama vile samaki chewa, tuna. Kwa ushauri zaidi nenda wizara ya mifugo na uvuvi kuna idara ya ufugaji samaki.
 
Kambale nao wanafugwa?

Mkuu kambale wanafugwa, japo changamoto ya kambale ni kuwa ukishawafuga hawawezi kuzaliana kwa njia ya kawaida (natural breeding), hivyo unatakiwa uwazalishe (artificial breeding).

Teknolojia yake ni rahisi mno wala haiitaji uwe mtaalamu kinachotakiwa ni mafunzo tu kidogo. Ukiweza watembelee wataalam wa Kingolwira utajifunza mengi hata kwa vitendo.
 
Changamoto kubwa inayoikabili hii sekta hapa Tanzania ni ukosefu wa sehemu za kuzalishia vifaranga (hatcheries) na chakula (feeds). Tuna jamii nyingi za samaki wanaoweza kufugwa kama Chewa (grouper), mwatiko (milkfish), Kambamti (shrimps), Kaa (crabs), Kambale, perege n.k. Kufuga samaki hakuhitaji utaalam sana tena kwa jamii ya wavuvi ambao wanamjua samaki na maji kuliko mtu yeyote inaweza kuwa rahisi sana kwao.

Teknolojia pia ni rahisi mfano mabwawa (ponds), vizimba (cages), matanki n.k. Kwa sasa perege ndio anafugwa sana kwa sababu ya urahisi wa upatikanaji wa vifaranga na chakula. Lakini bado tuna potential kubwa hasa baharini ukizingatia maji ya bahari hayana competition katika matumizi yake.
 
Natanguliza shukrani.mie ninabwawa langu la samaki ambao niliwapanda mwezi wa 12 mwaka jana ambao mpaka sasa watakuwa wametimiza miezi 7 tangu kupandwa,kutokana na maelezo ninayoyapata kwa wadau wa samaki wanasema tangu kupandwa mpaka kuvuna inachukua miezi 6.

Cha kushangaza mie samaki wangu mpaka sasa bado ni wadogo wenye ukubwa wa inch 2, binafsi nadhani tatizo inaweza kuwa chakula ninacho walisha, kwamba pumba pekee haziwezi kutosheleza.

Hizo ni hisia zangu, hivyo naomba mnipe orodha ya vyakula ninavyoweza kuwa nawabadilishia pia na ushauri mwingine ambao unaweza kunifikisha katika malengo ya kupanda na kuvunda ndani ya miezi 6.

Asanteni
 
Bora umegundua mapema kuwa chakula unachowapa hakina virutubisho vinavyohitajika. Ngoja niwaulize wataalamu nitakujuza....
 
naomba niku pm nikuulize maswali
nina interest na kuwa na bwala la kufugia samaki kama wwewe
but sijapata wataalamu
 
hongera kwanza maana ii shughuli nataman sana kuifanya bado cjpata muongoz wa gharama za kufanya haswa kwny kuchimba bwawa la samaki..
mkuu nahitaj kukuuliza maswal mawil matatu ngoja niku pm.
 
Bora umegundua mapema kuwa chakula unachowapa hakina virutubisho vinavyohitajika. Ngoja niwaulize wataalamu nitakujuza....

katavi asante kwa kujitolea kuniulizia kwa wataalam pia nasubiri majibu kwa nguvu zote.
 
The boss na rockll nimekwisha wajibu ktk pm.ila kama hamtoona usumbufu nawaomba m-google neno "bwawa la samaki" google watawaletea link itakayowapeleka moja kwa moja jamiiforums ambapo mtakutana na nondo za wakali wa mambo haya .
 
mkuu,
ulipanda mbegu gani? isijekuwa ulipanda dagaa au wajanja walikuingiza mjini ukifikiri umenunua vifaranga wa sato kumbe dagaa.

Vipi kuhusu pH ya bwawa na aina ya mbegu uliyoipanda, vinaendana? chakula na aina ya samaki vinamatter, pH, space, usafi wa bwawa, hali ya hewa etc samaki wanakula baadhi ya vegetation na si kila aina ya jani by the way kwa maelezo yako inaonekana ulichukulia ufugaji wa samaki kuwa ni rahisi sana [that's biggest mistake you made]
 
mkuu,
ulipanda mbegu gani? isijekuwa ulipanda dagaa au wajanja walikuingiza mjini ukifikiri umenunua vifaranga wa sato kumbe dagaa. Vipi kuhusu pH ya bwawa na aina ya mbegu uliyoipanda, vinaendana? chakula na aina ya samaki vinamatter, pH, space, usafi wa bwawa, hali ya hewa etc samaki wanakula baadhi ya vegetation na si kila aina ya jani by the way kwa maelezo yako inaonekana ulichukulia ufugaji wa samaki kuwa ni rahisi sana [that's biggest mistake you made]

ofcause,lakini ki ukweli katika kulichukulia suala zima la ufugaji,sikupenda kulichukulia wepesi ila pH Pengine liwe nalo ni kosa langu,maana sehem hii nilipo ni sehemu ambayo ina baridi kali,kuhusu kununua dagaa sidhani maana hawa samaki niliwanunua chuoni ambapo wao walinihakikishia,ili nikutoe wasi wasi nikwamba hapo hapo chuoni nao wanamabwawa siku naenda kuchukua hao vifaranga ni siku ambayo vifaranga hawakuwepo,nami kwa kuhofia kupoteza muda niliwaambia wanipe kutoka ktk mabwawa yao ila wao walikataa wakaniambia wale waliopo ktk mabwawa ya watakuwa sio bora.
 
Asanteni sana wadau, mie pia nina bwawa langu la mita kumi kwa kumi,bwawa hiili nilipandikiza vifaranga 200 miezi sita iliyopita bahati mpaya hao samaki mpaka sasa hawajakuwa wakubwa kufikia saizi kubwa,nilikwenda kwa wataalam wa nyegezi walinipa maelekezo mazuri na sasa mambo yanasonga mbele.

Mpaka sasa hawa samaki wametotoa watoto wengi sana kiasi cha kutishia udogo wa bwawa hata hivyo nipo mwishoni namalizia uchimbaji wa bwawa kubwa la mita 35 kwa 30 nadhani mwezi ujao nitapandikiza hao fingerings.

Kwa hivi sasa ninacho hitaji ni vitabu vitakavyo nisaidia kuielewa zaidi hii kazi maana mie sijasomea, kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata vitabu basi anielekeze au kama kuna mtandao wowote ambapo naweza ku downlod hasa vya kiswahili.
 
Asanteni sana wadau, mie pia nina bwawa langu la mita kumi kwa kumi,bwawa hiili nilipandikiza vifaranga 200 miezi sita iliyopita bahati mpaya hao samaki mpaka sasa hawajakuwa wakubwa kufikia saizi kubwa,nilikwenda kwa wataalam wa nyegezi walinipa maelekezo mazuri na sasa mambo yanasonga mbele. Mpaka sasa hawa samaki wametotoa watoto wengi sana kiasi cha kutishia udogo wa bwawa hata hivyo nipo mwishoni namalizia uchimbaji wa bwawa kubwa la mita 35 kwa 30 nadhani mwezi ujao nitapandikiza hao fingerings. Kwa hivi sasa ninacho hitaji ni vitabu vitakavyo nisaidia kuielewa zaidi hii kazi maana mie sijasomea,kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata vitabu basi anielekeze au kama kuna mtandao wowote ambapo naweza ku downlod hasa vya kiswahili.

Toa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.

Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.

Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.

Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.

Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.
 
Mkuu kambale wanafugwa, japo changamoto ya kambale ni kuwa ukishawafuga hawawezi kuzaliana kwa njia ya kawaida (natural breeding), hivyo unatakiwa uwazalishe (artificial breeding). Teknolojia yake ni rahisi mno wala haiitaji uwe mtaalamu kinachotakiwa ni mafunzo tu kidogo. Ukiweza watembelee wataalam wa Kingolwira utajifunza mengi hata kwa vitendo.

Uzuri wa kambale ni rough rider, nilifika Kinguluira na kupata maelezo haya ya kuzalisha hawa samaki.
 
Hizi ndio mada za kusaidia na kukwamua jamii. Hongera mleta mada.

Nawapigia hao Kingurwila sasa hivi. Nna eka moja Kibaha si inatosha sana kwa hii kazi?

Hilo eneo linatosha kabisa kwa kuanzia. Kama hutaona taabu, mtafute Padri mmoja yy anafuga samaki kibiashara njia ya kuelekea Bagamoyo ili ukajionee vitu kwa vitendo.
 
Kambale nao wanafugwa?

wanafugwa mkuu ukienda sua unapata vitoto vya kufuga but kuna complications kambale huwa hawazai sometimes but sua wamegundua mbinu ya kuotolesha kambale hance wao wanauza watoto na mfugaji anawanunua wakikomaa unawavuna na kwenda kununua vingine, ni kama vilanga wa kuku mkuuu!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom