Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Malila Malia, shusha shusha vitu. Huwa nikiona tu jina lako, basi huwa lazima nipekue hata kama kitu hakinihusu.

Ila ufugaji wa SAMAKI huwa unanikuna sana. ONE DAY nitakutafuta kwa hili. Asante sana kwa nondo zako.

Tunafaidi mengi sana na usisite kuweka zaidi na zaidi busara zako. Watakaomeza watameza, watakaotema wateme.
 
kwa aliye karibu na ziwa ,unaweza kufugia samaki kando ya ziwa badala ya kuchimba bwawa la samaki.nilishawahi kuona program ktk tv. Discover Africa ,kuna kaburu yupo zimbabwe anafuga samaki ktk ziwa,na anawalisha soya na nafaka zinginezo.

musoma kuna kituo kikubwa cha utafiti wa samaki,nina rafiki yangu alikuwa stationed huko miaka ya nyuma
 
Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.
ni kweli angemPM lakini hata sisi tunahitaji kupata huo ujuzi kupitia kwenye hii sred. hivyo ni vema wakaendelea kuhojiana hapahapa ili tupateelimu nzuri. wakiingia kwenye issue za PM itakula kwetu.
 
Wakuu natamani kufuga samaki lakini sijui wapi nitapata wajenzi wa bwawa, kuna mtu ana habari zozote kuhusu hili jambo??? msaada tafadhali

Bwawa linahitaji inlet na outlet ili ufuge vizuri,lakini wakati mwingine static water ponds unaweza kutumia, hapa inabidi uangalie kama hilo bonde lako linaweza kukupa sifa hizo vinginevyo unaweza kupata shida kama ziwa likarudi na level ya maji ikazidi sana, samaki wote watasombwa, au ukitumia maji yaliyotuama kama ulivyosema, level ikipungua chini ya mita 1.2 samaki wanaweza wasifanye vizuri.

Hizi zote ni changamoto, lazima upambane nazo na uzishinde. Mimi nilianza pilot kwa kutumia static water, samaki wanakuwa vizuri, ila mimi maji yanatoka chini, kwa hiyo evaporation hainiathiri, kuna wakati dalili za kukosekana oxygen huwa naziona. Kama unaweza kupata mahali ambapo unaweza kuwa na mfereji wa kuingiza maji, ungefanikiwa sana.
 
what is the comperative cost advantage?

hivi ukifuga samaki kwenye bwawa lako, je gharama za ufugaji mpaka kuuza zinaweza kuwa better than samaki wanaotoka kwnye maziwa kama victoria etc, bei zikoje, je ukiweza kufuga sato dar au karibu na dar unaweza kuuza kwa bei ya sato katika soko la kawaida na kupata faida? hivi samaki wa kufugwa mwenye wastani wa nusu kilo anaweza kutunzwa kwa muda gani mpaka kuwa tayari kuuzwa?

and what is yielding rate

is fish farming in Tz worth the value of investment and time?

just out of curiousity

someone should revert back to my queries please
 
Kwa Tz ufugaji wa samaki haikuwa biashara kubwa huko nyuma, lakini sasa hivi biashara hii inakuwa kwa kasi nzuri na inalipa. Samaki hawatoshelezi soko, samaki hawafiki kwa walaji ktk ubora unaotakiwa. Ukija ktk suala la afya, samaki wa kufugwa wanapendwa sana. Jiulize swali, iweje samaki atoke Japan na aje auzwe Dsm?

Market size ya tilapia hufikiwa baada ya miezi sita, tilapia huzaliana sana na wana growth rate kubwa ukizingatia utalaam. African cat fish huchelewa kidogo kufikia market size, lakini ni samaki anayeweza kuvumilia mazingira. Siku nilipofika FAO Kinguluira na kukosa vifaranga ndio nikajua kumekucha. Wafugaji wanaongezeka.

Igowole, kuna kabwawa kadogo, lakini kanatema samaki ile mbaya na kameajiri watu kibao, na mji wa Igowole sasa wana kitoweo cha uhakika. Ni suala la planning na kufuata utalaam.
 
Bwawa linahitaji inlet na outlet ili ufuge vizuri,lakini wakati mwingine static water ponds unaweza kutumia, hapa inabidi uangalie kama hilo bonde lako linaweza kukupa sifa hizo vinginevyo unaweza kupata shida kama ziwa likarudi na level ya maji ikazidi sana, samaki wote watasombwa, au ukitumia maji yaliyotuama kama ulivyosema, level ikipungua chini ya mita 1.2 samaki wanaweza wasifanye vizuri.

Hizi zote ni changamoto, lazima upambane nazo na uzishinde. Mimi nilianza pilot kwa kutumia static water, samaki wanakuwa vizuri, ila mimi maji yanatoka chini, kwa hiyo evaporation hainiathiri, kuna wakati dalili za kukosekana oxygen huwa naziona. Kama unaweza kupata mahali ambapo unaweza kuwa na mfereji wa kuingiza maji, ungefanikiwa sana.

Mkuu nakushukuru sana kwa uelemishaji wa hali ya juu unaoendelea kuutoa pamoja na wana jamvi wote mnaoendelea kutoa michango yenu.
kuhusu bwawa, heka 10 zipo kama km 3 kutoka ziwani, mpango wangu ni kuchimba kisima ambacho ndo kitakuwa chanzo cha maji ya bwawani, nitaweka drainage (outlet) kuelekea ziwani.

Maji ya ziwa hayaweza kufika bwawani isipokuwa wakati wa mvua za nguvu kama el nino ambazo ni adimu. Jambo ambalo sijui nitafanyaje ni kuzuia maji ya mvua yasifurikie bwawani, nimesoma kwenye mtandao wanasema ikitokea hivyo basi silt itajaa ndani ya bwawa na kuaribu.

kwa uelewa wangu nadhani silt wanamaanisha tope
 
ni kweli angemPM lakini hata sisi tunahitaji kupata huo ujuzi kupitia kwenye hii sred. hivyo ni vema wakaendelea kuhojiana hapahapa ili tupateelimu nzuri. wakiingia kwenye issue za PM itakula kwetu.

Malila ana uelewa mpana juu ya hili jambo, naona ni vyema tuendelee hivi hivi ili wenye interest kama yangu pia wafaidi ila nita m PM kwa maongezi ya faragha
 
these are real great thinkers who can even overthrow the world,thanx very much indeed my people i'm closely walking with you to reach my dreams
 
Niko hapa Mbezi kwa Msuguri DSM, nataka kuanza kufuga samaki, udongo ni wa mchanganyiko wa mfinyanzi na mchanga...naomba ushauri kama udongo huu utafaa kwenye kutengeneza bwawa na kama haufai mbadala wake ni nini, na ni aina gani ya samaki naweza kuwafuga kwa eneo hili?
 
Mkuu mimi nimefaidika sana na michango iliyotolewa hapa JF, mwanzoni nilidhani hapa JF ni mizaha mizaha tu lakini sasa nimekubali hapa ni mahala pa great thinkers, nilikuwa bado najipanga kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanaJF wooooteeee!

Baada ya kuyasema hayo ngoja nikumegee kidogo namna ya kupata jibu unalolifatufa. Kwa ufupi wasiliana na Kajitunus Osewe, Assistant director, Aquaculture Development Division, Ministry of Livestock development and Fisheries mobile: 0755166226 au 0787469801Email yake ni kajitanus@gmail.com ukiwa na bahati kama ya kwangu atakukabidhi kwa afisa anayeshughulikia ufugaji wa samaki kwenye eneo lako Oh! ni watu wazuri sana, very friendly, bless them.
Good luck
 
Dar kuna watu kadhaa wanafanya hiyo biashara. Barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Palm Beach Hotel kuna jamaa anafanya hiyo biashara, kwa Gold Fish nafikiri anauza kwenye shs 20,000 kwa mmoja, wengine ni kuanzia elfu 5 mpaka 25 kutegemea na aina.

Anauza vyakula pia, kuanzia 3,000 mpaka 10,000 kutegemea na aina. Huuza aquariums pia. Ana wateja wa kutosha hapa mjini.
 
How profitable is this business. Sijasikia yeyote akielezea. Baada ya miezi sita, samaki moja utamuuza kiasi gani.
 
How profitable is this business. Sijasikia yeyote akielezea. Baada ya miezi sita, samaki moja utamuuza kiasi gani.

Kwa Tanzania biashara hii ndio kwanza inaanza,hakuna wakulima wakubwa wa samaki kama wenzetu Uganda/Kenya ambao wanaweza kutoa takwimu vizuri, ila samaki ni biashara ya kimya kimya,wale jamaa wa Iringa wanaoleta samaki Dar toka Iringa wanajua kinachoendelea ndio maana hawaachi.

Kama WAFICO wa Uganda, wanafanya vizuri na wanazidiwa na mahitaji.
 
Dah hiyo ya kenge imenishtua maana bwawa ninalotaka kufugia ni eneeo lenye kenge...dawa ya hawa kenge ni nini wakuu?

Dawa inayojulikana kule Uswahilini kwetu ni kuchemsha mayai mengi,halafu yachukue kayaweke pale kando ya bwawa lako.

Kenge anakawaida ya kumeza yai na analivunjia shingoni kama halijachemshwa, sasa likichemshwa haliwezi kuvunjika, basi linamkaba na ndio kifo chake. Sasa kama ataweza kumeza, si ajabu akamaliza mayai yote na asife!
 
Dawa inayojulikana kule Uswahilini kwetu ni kuchemsha mayai mengi,halafu yachukue kayaweke pale kando ya bwawa lako. Kenge anakawaida ya kumeza yai na analivunjia shingoni kama halijachemshwa, sasa likichemshwa haliwezi kuvunjika,basi linamkaba na ndio kifo chake. Sasa kama ataweza kumeza, si ajabu akamaliza mayai yote na asife!!!!!!!!!!!!!

Teh teh teh...hapo kazi kwl kwl mkuu Malila! Hii nilishaisikia ila sijapata ushuhuda wa mtu aliyefanikiwa kutumia huu mtego na ninaogopa isjie kula kwangu maana hata nguchiro na mbwa nao wanazagaa zagaa hilo eneo!
 
kingolwira wanauza na kukuchimbia bwawa bei ni laki tano tu. Ni kituo cha mafunzo ya wakulima juu ya ufugaji wa samaki, kipo Morogoro kabla hujafika Morogoro jr seminary kama watokea Dsm upande wa kulia. Ukishamaliza mashamba ya mkonge, kunja kulia kama 1km basi utawaona jamaa pale wamejaa tele.

Si warasimu, wala hawana njoo kesho. Ili kuondoa longo longo piga 0757891761 moja kwa moja ili upate majibu ya maswali yako yote.
 
Back
Top Bottom