Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

ImageUploadedByJamiiForums1449417454.486731.jpg
 
Niko mbioni kuanza jambo hili, kwa sasa nafukuzia kijipesa flani cha loan toka NMB ili nikalipe Ardhi kisha naanza mchakato. Tusitupane humu ndani, tuwe tunapeana feedback. Asanteni nyote kwa mawazo yenu mazuri na ya kujenga
 
Niko mbioni kuanza jambo hili, kwa sasa nafukuzia kijipesa flani cha loan toka NMB ili nikalipe Ardhi kisha naanza mchakato. Tusitupane humu ndani, tuwe tunapeana feedback. Asanteni nyote kwa mawazo yenu mazuri na ya kujenga

Tutaendelea kufahamishana-
 
Kwenye thread mwanzoni nimeelezea rasilimali zinazohitajika
1.Ardhi
2.Nguvu kazi
3.Maji
4.Fedha

Sasa nashindwa kuweka monetary value ya hizo rasilimali sababu zinabadilika badilika kulingana na eneo husika.kwa mfano maeneo ya arusha ardhi iko juu kwa ekari moja unaweza gharamia 14m na hapo ni kijijini.

Uchimbaji nao pia inategemea unachimba na mashine au watu,ila uchimbaji na mashine ndio mzuri lakini gharama zake ziko juu kidogo kama nilivosema nimekodisha mashine kuchimba 43m*15m kwa 700,000 kina cha meter 3.

Maji nayo nategemea maji ya mferejeni nimejiunga na wana kijiji,ila haya maji sio reliable nikipata hela ntachimba kisima changu mwenyewe.

Vibarua wa kufanya kazi hawa ndio hawana gharama ni maelewano tu.

Asante sana kwa Elimu nzuri. Mungu akubariki sana.
Je kina kinatakiwa kiwe mita 3?
 
Jamani mimi nipo Lindi nina bwawa heka moja natamani kufuga samaki aina ya kambare , perege na kamba wa maji baridi sasa mtaji sina nahitaji mwekezaji tushirikiane
 
Sure naona wengi tumeangalia uwekezaji upande mmoja tuu..;)

[Hello JF members yeyote atakayehitaji chakula cha samaki aina ya cassava chips au casssava cripts tunaomba aweze ku tu PM, tunazo aina zoote ya cassava chips na mapumba yake ambayo hutumika kwa ajili kutegeneza chakula cha kukuQUOTE=Malila;816346]Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

--------------------------

Uvuvi%2Bbusega%2B4.jpg



-----------------------------






*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments
[/QUOTE]
 
Uchimbaji wa bwana unategemea na ukubwa wa bwawa,ukitaka kazi na bwawa likae vizuri inakuhitaji uwe na excavators ila pia wapo watu wanachimba ila wanachukua mda mrefu sana. Kwa mfano nimechimba na excavator size ya 43mx15m kwa shilling 700,000 arusha.

Mkuu naomba number yako nipo Arusha nahitaji kuchimba pia
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom