Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ndugu soko lipo juuu sana sio kwa dar tu..nilipata order ya kg300 ya samki ila.akashindkana mtu wa kua nao..ss kama kg moj.dukan ni sh.7000 ad 8000..jumla utapatana na mnunuzi and utaona.how much itaingiza

naomba unipe no yako ya simu pm....samaki wangu wakikua nikutafute...
 
Habari.

Kupitia jukwaa hili tumekua tukijifunza vitu tofouti juu ya namna ya kujiendeleza kiuchumi ili kujikwamua kutoka katika hali tulizonazo. shukrani kwa wale walionitafuta na wakapata ushauri, nadhani bado tupo pamoja na mtafanikiwa.

Bado nasisitiza uchaguaji wa eneo na uchimbaji wa bwawa unahitajika umakini kwani ndipo ambapo utakua unafanya mladi hivo ikiwa kama initial stage ,inabidi umakini,hivo ujumuisha, uwepo wa maji safi kwa kiasi kikubwa, na uwezekeno wa kupata chakula cha samaki wako.

Mahitaji ni makubwa kulinganisha na wataalamu tuliopo, ivo tuendelee kuwasiliana kwa ajili ya kupeana ujuzi na ushauri, fuga samaki mana ni biashara inayolipa sana. kwa maelezo zaid wasiliana nami 0717451771.

kaka nitakutafuta chemba
 
Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wanaolalamika kuwa samaki wao hawakui hasa tilapia.

Zifuatazo ni sababu zilizobainika kuwa ndio chanzo cha tatizo hilo:

1. Mfugaji kapata wapi hiyo elimu ya ufugaji

2. Idadi ya samaki wanaopandikizwa kwa mita ya mraba kwa mabwawa ya ardhini na kujengea kwa cement. Kiwango halisi ni vifaranga 5-7 kwa mita ya mraba kwa aina ya monosex na 1-3 kwa mixed sex na sio 10-20 kama inavyoelekezwa na baadhi ya watoa elimu.

3. Chakula feki kinachouzwa mitaani. Watu wanatumia tu pumba na kuwadanganya wakulima kuwa ni chakula special. Nunueni chakula kilichokuwa na label inayoonesha ingredients na percentage yake ikiwemo chapa ya tbs.

4. Ulishaji wa chakula. Wakulima wanalisha chakula kiasi kidogo. Kopo dogo la uhai sio kipimo jamani. Samaki anakula 1/3 ya uzito wakee au lisha mpaka uone hakuna samaki anahangaikia chakula ktk bwawa.

5. Uzito wa samaki mmoja ndani ya miezi 6 ni 200-400 g tena hiyo 400 uwe umefanya management ya nguvu. Hii ni kwa bwawa la ardhini na kujengea. Sio kilo moja kama mnavyoamonishwa.

Hitimisho: Kabla ya kuanza kazi za ujenzi na ufugaji tembelea wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanapatikana Temeke vetenari
 
kaka nimekupata vizuri kabisa. Mimi ni mmojawapo wa wanaotaka kujiingiza katika kilimo hiki, naomba pia kama una info za gharama ya ujenzi wa bwawa la ardhini nipatie tafadhali
 
Kama ungependa kujua ni jinsi gani unaweza kutengeneza bwa la samaki yaani FishPond.
Fuata steps zifuatazo.

  1. Chimba bwawa lako kwa ukubwa utakao kulinga na eneo lako linavyo kuruhusu
  2. Funika na Mfuko mgumu wa plastic ili kuzuia maji yasipotee sana
  3. Zungusia matofali Bwawa lako
  4. jaza maji
  5. weka samaki wako
NB: Hakikisha hakuna wanyama waaaribifu kama kuku na mifugo mingine.
Chini hapa nimeeambatanisha na kitabu kidogo kitakachokupa mwongozo halisi zikiwemo na picha
View attachment Fishpond-Book.pdf
 
Mkuu nakushukuru sana kwa kutupatia maarifa na utaalam mzuri wa kutengeneza bwawa la kufugia samaki. Ndoto yangu ya kufuga samaki nyumbani itatimia sasa!

Vipi kuhusu maji, kutakuwa na haja ya kuyabadili baada ya muda au ni hayo hayo?
 
Asante mkuu,nimepata elimu hapa kwani nina ndoto ya kufuga samaki..

Ahsante kwa mwitikio wako. Fanikiwa katika ndoto yako.

ahsante mkuu,wewe unafaa kuwa rafiki yangu,maana una ideas za maendeleo kama mm.

Karibu rafiki,
usisite pia kuniandikia info@chapisha.com

Nashukru kwa maarifa haya mkuu

Karibu, tembelea mara kwa mara chapisha.com kwa maarifa zaidi.

Nimenufaika. Asante sana.

Karibu

Barikiwa sana ..... tupo pamoja

Amina. na wewe pia.
 
Back
Top Bottom