Passport: Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mimi nilipata passport kwa siku mbili tu bila hata rushwa, unatakiwa uwe na barua ya wito kama unaenda nje pia na barua ya utambulisho kama ni mfanyakazi. hii ni hatua ya mwisho baada ya kujaza form. Gharama ya passport ni sh 50,000/=,
ukitaka kupata kwa urahisi bila mawazo unaenda na 50 nyingine unamkonyeza jamaa pale mnapeana namba za simu unaondoka kwenda mjini kuendelea na shughuli zako zingine halafu jamaa anapiga simu unafuata mzigo wako
 
na kama nataka ku-renew, maana yangu imeexpire utaratibu ukoje na gharama zikoje
 
Ni kweli uyasemayo ni rahisi saana kupata hata mimi nilifanya hivyo
 
kwanza unataka passport ipi,ile ya muda ya karatas,ya East Africa or international?

ya karatas ni dakika chache,eas africa na international ni ndani ya wik moja unapata, mkuu eac au ya muda ya kalatas c nitaka wik 2
 
Ukitoa laki na hamsini na picha ndogo nane,we unakaa nyumbani tu,watakupigia simu kwenda kuchukuliwa alama za vidole na ni kitendo cha dakika kadhaa tu,siku ya pili unaletewa pasi yako ofisini,bar au hata nyumbani.
 
Naombeni msaada nawezaje kupata pasport ya Tanzania sababu mimi ni mtanzania ninayetegemea kuanza kufanya biashara fulani katika nchi za Sadec na EAC na swala la short permit lina usumbufu naomba kujua naanzia wapi.
 
Hilo neno la mwisho litakuchukua mda mrefu mpaka unaipata
By eze wey nakutakia kila la kheri na biashara njema
 
Naombeni msaada nawezaje kupata pasport ya Tanzania sababu mimi ni mtanzania ninayetegemea kuanza kufanya biashara fulani katika nchi za Sadec na EAC na swala la short permit lina usumbufu naomba kujua naanzia wapi.

Kupata passport (Hati ya Kusafiria) hakuna usumbufu wowote, ikiwa tu viambatisho vyote muhimu unavyo! Nenda office ya uhamiaji iliyo karibu nawe na ulipie form (ilikuwa ni elf 10, sina uhakika kama bei bado ni ile ile), then ijaze hiyo form kikamilifu, then irudishe ofc ya uhamiaji na utalipia sh elf 40, taaratibu za kiofisi zitafuata kama vile kuchukuliwa finger prints etc, then baada kama ya wiki moja passport yako itakuwa tayari!

KAma nilivyoeleza hapo juu, kikubwa ni kuwa na viambatisho vyote muhimu vinavyotakiwa na form ijazwe kikamilifu na Kwa usahihi! Kwa kuwa wewe ni mfanyabiashara, sababu ya kuomba passport itakuwa ni safari za kiibiashara, na itabd uambatishe nakala ya leseni yako ya biashara!
 
je kama ninamatarajio ya kusafiri nje ya nchi badae so kibiashara lakini taratibu zikoje
 
Naombeni msaada nawezaje kupata pasport ya Tanzania sababu mimi ni mtanzania ninayetegemea kuanza kufanya biashara fulani katika nchi za Sadec na EAC na swala la short permit lina usumbufu naomba kujua naanzia wapi.
Hapo unamanisha nini mkuu, maana uhamiaji wanatoa hati ya kusafiria ya muda mfupi au ile ya muda mrefu 10yrs, permit za kuingia au kuishi zinatolewa na nchi husika, au labda kama sio mtz ndio utapewa hiyo permit ya kuishi humu nchini na uhamiaji ya kwetu
 
Heshima kwenu wakuu,

Naomba kufahamishwa ni hatua gani ambazo naweza kufanya ili kupata passport ya kusafiria kwa ajili ya kwenda kusoma.

Naomba kujulishwa ni process gani natakiwa kufuata na itachukua muda gani kuipata,nipo Mwanza naweza nikaipatia huku huku au ni lazima niende Dar?

Thanks in advance

=============
passport-ya-tanzania.jpg


Yapo mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia mtu ndipo huhisi jambo ambalo alikuwa halijui kuwa ni jepesi. Lakini kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu. Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa au ufahari tena isipokuwa ni jambo ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya kila siku ya walio wengi. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho husababisha watu kutoka nchi moja hadi nyingine.

Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. Yumkini usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana na pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi lakini moja ni kuwa pasipoti ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti.


1. PASIPOTI HUOMBWA NA MWOMBAJI LAKINI HUBAKI MALI YA SERIKALI.

Hakuna mtu mwenye umiliki wa kudumu wa pasipoti. Kwa mujibu wa sheria licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo ya mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali. Hii ndio sababu serikali huweza kumnyanganya mtu pasipoti panapo jambo fulani. Ni kwakuwa pasipoti ni mali yake. Wewe mwombaji uliyepewa pasipoti unayo haki ya matumizi na uhifadhi wake lakini mmiliki mkuu ni serikali.

2.ILI KUPATA PASIPOTI UNAHITAJI KUWA NA VITU HIVI.

( a ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha mwombaji.Cheti cha kuzaliwa ni hivi vyeti vya kawaida ambavyo hutolewa mahospitalini au mamlaka nyingine baada ya kuzaliwa kwa mtu. Katika kipindi hiki wapo wengine wamekwisapata vyeti vya uraia. Cheti cha uraia chaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa. Pia tumesema hati ya kiapo. Hii hutolewa kwenye ofisi za wanasheria. Mwombaji huwa anaapa pamoja na mambo mengine kuthibitisha kuwa taarifa anazozitoa ni za kweli kwa dhati yake. Pia tukasema vyeti vya uraia wa kuandikishwa. Hivi wanavyo raia wa Tanzania ambao si wa kuzaliwa. Katika kuomba kupata pasipoti nao hutakiwa kuwa navyo.

( b ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha
mzazi au wazazi wa mwombaji. Hapo juu tumeona vitu kama hivihivi lakini ilikuwa ni kwa mwombaji wa pasipoti mwenyewe. Hivi hapa sasa ni kwa ajili ya mzazi wa mwombaji. Vile vitu vyote alivyowasilisha mwombaji pale juu ndio vilevile anavyopaswa kuwasilisha mzazi wa mwombaji. Si kwamba mzazi mwenyewe ndio anapeleka vitu hivyo hapana, wewe mwombaji ndio unabeba vitu hivi kwa niaba ya mzazi. Hapa mzazi ni yeyote anaweza kuwa baba au mama.Lengo lake ni kutaka kujua historia fupi ya nasaba ya mzazi wa mwombaji.

( c ) Inahitajika picha ya hivi karibuni ya pasipoti size. Sharti kubwa waliloweka hapa ni kuwa picha hiyo isiwe katika fremu. Fremu hapa si tu ile fremu ya kawaida tuliyoizoea bali pia hata pasipoti kuwa na maringo au mapambo ya kuzungushia pembeni nayo ni fremu kwa maana hii. Pasipoti iwe mnyooko(plain) isiwe na mbwembwe zozote.

( d ) Iwapo mwombaji ana umri wa chini ya miaka kumi na nane (18), wazazi walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi. Nyaraka hii ya ridhaa ya maandishi huandaliwa na mwanasheria.Hii ni kusema kuwa utaratibu wa mtu mzima aliyevuka miaka kumi na nane ni tofauti na mtu aliye chini ya miaka hiyo katika kupata pasipoti. Baada ya kukamilisha vitu hivi kama nilivyoeleza basi hatua inayofuata ni kufuata utaratibu huu chini.

3.FOMU ZA MAOMBI HUPATIKANA WAPI.

Ofisi za uhamiaji ndipo zilipo fomu za maombi ya pasipoti. Hii ni popote Dar es salaam au mikoani. Suala la msingi ni kuwa ofisi hiyo iwe ya uhamiaji utapata fomu hizo. Utachukua fomu hiyo utaijaza na baada ya kuijaza itawasilishwa kwa mkurugenzi wa uhamiaji. Aidha suala jingine la msingi ni kuwa fomu hii itawasilishwa sambamba na nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

4.BEI YA PASIPOTI NI KIASI GANI.

Ada rasmi ya kupata pasipoti ni fedha za Kitanzania kiasi cha shilingi 50,000/=( Elfu hamsini tu). Aidha kwakuwa wanasheria ndio hushughulika na kutafuta pasipoti basi bei yao haiingizwi katika ada rasmi ya serikali kama nilivyoieleza hapo juu.

5.UNAWEZA KUOMBWA VIAMBATANISHO VYA ZIADA.

Jambo jingine ni kuwa safari zimeainishwa kwa namna mbalimbali.Ukisoma nyuma ya fomu ya maombi utaliona hili. Kutokana na hilo wakati mwingine waweza kuombwa viambatanisho vya ziada. Hii ni kutokana na utofauti wa safari. Hii ni kusema kuwa yawezekana mwombaji akaombwa viambatanisho viitwavyo viambatanisho "maalum". Hivyo basi mtu asishangae kukutana na kitu cha namna hiyo.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
 
nenda ofisi ya uhamiaji iliyo jirani na wewe manake uhamiaji wana ofisi katika kila mikoa na baadhi ya wilaya kwa msaada zaidi NI-PM!!!
 
kuipata fasta inategemeana na wewe utaandika unaanza lini masomo yako kwenye form utakayopewa uhamiaji.
 
Wakuu kwa wenye uzoefu na hili, utaratibu ukoje? Je wanataka viambatanishi vipi na gharama zikoje?? Je inachukua muda gani toka kufanya application mpaka kuipata? Na mwisho kuna tofauti gani kati ya VISA na PASSPORT?

Natanguliza shukrani!!
 
ki kawaida ni Wiki ila i know some people ambao watakufanya umiliki passport kwa siku 2 tu
sema dau lako liwe kubwa
na dau lako likiwa kubwa zaidi kuanzia saa kumi na moja asubuhi mpaka kesho asubuhi saa kumi na moja una passport tayari

karibu Dar Es Salaam
 
Wakuu kwa wenye uzoefu na hili, utaratibu ukoje? Je wanataka viambatanishi vipi na gharama zikoje?? Je inachukua muda gani toka kufanya application mpaka kuipata? Na mwisho kuna tofauti gani kati ya VISA na PASSPORT?

Natanguliza shukrani!!

Passport (Hati ya kusafiria)uombwa kwenye nchi yako na idara ya uhamiaji ndio wenye mamlaka ya kukupatia,jaza fomu,cheti cha kuzaliwa na picha ndogo (passport size)kuhusu mda inawezachukua one week lakini kama upo ''connected'' utaipata chini ya saa moja...Visa ni kibari cha kuingia kwenye nchi nyingine iwe ni kufanya kazi,kutembea nk wenye uwezo wa kukupa visa ni idara ya uhamiaji wa nchi unayokwenda...visa na passport ni watoto mapacha ambao uenda pamoja
 
ki kawaida ni Wiki ila i know some people ambao watakufanya umiliki passport kwa siku 2 tu
sema dau lako liwe kubwa
na dau lako likiwa kubwa zaidi kuanzia saa kumi na moja asubuhi mpaka kesho asubuhi saa kumi na moja una passport tayari

karibu Dar Es Salaam

dau kubwa ni lipi mkuu? Kifupi sihihitaji kwa uharaka sana...ila nitajie hilo dau incase of emergence!!
 
Passport (Hati ya kusafiria)uombwa kwenye nchi yako na idara ya uhamiaji ndio wenye mamlaka ya kukupatia,jaza fomu,cheti cha kuzaliwa na picha ndogo (passport size)kuhusu mda inawezachukua one week lakini kama upo ''connected'' utaipata chini ya saa moja...Visa ni kibari cha kuingia kwenye nchi nyingine iwe ni kufanya kazi,kutembea nk wenye uwezo wa kukupa visa ni idara ya uhamiaji wa nchi unayokwenda...visa na passport ni watoto mapacha ambao uenda pamoja

nashukuru kwa maelezo yako mkuu!!
 
ki kawaida ni Wiki ila i know some people ambao watakufanya umiliki passport kwa siku 2 tu
sema dau lako liwe kubwa
na dau lako likiwa kubwa zaidi kuanzia saa kumi na moja asubuhi mpaka kesho asubuhi saa kumi na moja una passport tayari

karibu Dar Es Salaam

mkuu me yangu ime-expire ita cost sh ngapi ku-renew kwa haraka maana huo muda wa week unaweza kuwa hata mwezi nenda rudi sitaweza
 
Back
Top Bottom