Stahmy Junior
Member
- Mar 11, 2011
- 82
- 16
Inachukua siku ngapi toka kulipia mpaka kuipata?
Wadau kwa mwenye upeo naomba mnisaidie..Gharama ya kupata hati ya kusafiria au paspoti kwa hapa kwetu Tanzania ni shilingi ngapi?
Kuna taratibu za kufata, ila hiyo fifty ndo kila kitu, nimechukua mwaka jana, na hawajatangaza kubadili gharama. hakuna gharama za pembeni ukiondoa wewe kuwa picha 6, kuna wakati utahitaji muhuri wa wakili (utamlipa ghrama huyu), serikali ya mtaa.
Kama uko karibu na ofisi za uhamiaji ni bora ukaenda kuwaona, hawana shida. Kuipata inategemea lakini haizidi mwezi tangu umeclear yanayohitajika.
All the best
Wana jf naomba msaada.ninarafiki yangu anatarajia kupata mualiko kutoka kwa rafiki yake ambae anaishi Turkey.sasa hajui jinsi yakuomba visa hadi kuipata,nakupata passport maana hajawai kusafiri.ss anaomba msaada kwa mwenye uzoefu na haya mambo.je?visa na passport anaweza kupata kwa mda gani?je akipata anaruhusiwa kusafiri mara 2 apatapo au inakuwaje?2naomba msaada kwa ilo wanajf.pamoja na mahali unapofatilia na gharama.asante
Mkuu passport inapatikana ofisi za uhamiaji kila mkoa japo mikoani ni maajenti tu maana lazima itoke Dar es Salaam. Kwa kawaida inachukua majuma mawili kuipata na gharama yake ni Tshs. 50,000 (kama hawajapandisha au kushusha). Baada ya kupata passport basi aende ubalozi wa Uturuki uliopo Dar es Salaam akiwa na barua ya mwaliko kutoka kwa huyo mwenyeji wake akaombe visa. Maelezo mengine atayapata hukohuko ubalozini.

Nina pasport niliokuwa naitumia ila imeisha kurasa mkuu je kunahaja ya barua ya kijiji?
mbona ni issue ndogo sana,passport kwa njia ya kawaida unaipata ndani ya wik moja,kwa rushwa siku 2 adi 3
hiyo ya pili bei gan nataka kwenda kampala kushehekea my birth day na shemeji yako.mkuu