BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
Pasipoti, viza sasa kulipiwa benki
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,December 22, 2008 @21:15
Idara ya Uhamiaji nchini imeanzisha utaratibu mpya ambapo kuanzia mwezi ujao, malipo ya huduma mbalimbali kama vile viza, pasipoti na vibali vya kuishi nchini, yatalipwa kupitia matawi ya Benki ya NMB.
Kamishna Mkuu wa Idara hiyo, Kinemo Kihomano alitangaza utaratibu huo mpya jana kwa waandishi wa habari Dar es Salaam katika taarifa yake iliyosomwa na Kamishna wa Pasipoti, Cuthbeth Sambalyegula.
Kihomano alisema utaratibu huo mpya utatumika katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dar es Salaam, ofisi zote za mikoa na wilaya na baadhi ya vituo vya kutoka na kuingia nchini kama vile Namanga, Tarakea na Tunduma.
Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali ili kuhakikisha mapato hayo yanazidi kuongezeka. Alisema ingawa mapato yamekuwa yakiongezeka kila mwaka kwa kati ya asilimia 20 hadi 30, lakini kuna uwezekano wa mapato hayo kuongezeka zaidi.
Alisema lengo lingine ni kuongeza usalama wa fedha hizo kwani zinaweza kuibwa na majambazi wakati wa kusafirisha kama utaratibu huu wa sasa ukiendelea. Alisema utaratibu huo mpya pia utasaidia kupunguza msongamano kwenye ofisi za Idara hiyo kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye ofisi hizo.
Kwa utaratibu huo, wateja wa huduma za uhamiaji tunawasihi kulipia kupitia benki moja kwa moja badala ya utaratibu wa sasa ambapo huwa na adha kadhaa ikiwamo ufinyu wa ofisi zetu, alisema Kamishna Mkuu huyo.
Alisema idara hiyo imeshafanya mazungumzo na kufikia makubaliano na Benki ya NMB na benki hiyo imekubali kutenga dawati maalumu kwa ajili ya wateja wa uhamiaji ili kuepusha adha ya msongamano. Alisema walichagua benki hiyo kwa sababu ina matawi mengi nchini hasa katika mikoa na wilaya ambazo idara hiyo inatoa huduma.
Kwa mujibu wa Mhasibu wa Idara hiyo, David Mbwilo, wafanyakazi wa idara hiyo ambao kazi zao sasa zitafanywa na benki, hawataachishwa kazi kwa kuwa idara hiyo ina uhaba wa wafanyakazi hivyo watahamishiwa vituo vingine vya kazi. Mbwilo alisema makusanyo ya fedha kwa mwaka jana yalifikia Sh bilioni 16.6 na mwaka huu ilikuwa inatarajia kukusanya Sh bilioni 20.4.