Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Mkuu Pasco.Heshima mbele.

Nimeamua kuanzisha thread hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umeufanya hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge. Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.

Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema. Kuongeza ni suala la kawaida sana. Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali. Hansard ikitoka nitaweka hapa.

Naomba uiondoe thread yako. Ili usipotoshe na wengine pia.

Kutoka Mjengoni
Aluta Continua.
 
Mkuu,
sawa kabisa,,,
ameropoka huyu, na hatuwezi kukaa kimya TUKIIACHA kauli yake yenye sumu ipite bila kupigwa !
 
Inawezekana amemuelewa vibaya au ana lake jambo. Ila ukisoma katikati ya mstari utagundua kuwa anamambo yake binafsi na Mbowe. Kama wanamambo yao binafsi wadili kivyao, wasikiingize chama chetu.
 
Asante sana mama. Huyu jamaa alishapotosha watu hivyo KANUSHO kama hili lilikuwa muhimu sana. Mimi mwenyewe nilishangaa imekuwaje Mwenyekiti atoe tamko kama hilo tena ghafla namna hiyo. Pasco atuombe radhi wana CDM.
 
Mie nilijua tu kachanganya habari, maana alivyoiweka kishabiki shabiki tu!
 
Sikutegemea ile thread itoke kwa Pasco! kwani imekaa kishakunaku sana.. nahisi wamemwibia password:coffee:
 
Mkuu Pasco.Heshima mbele.

Nimeamua kuanzisha thread hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umeufanya hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge.Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema.Kuongeza ni suala la kawaida sana.Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali.Hansard ikitoka nitaweka hapa.

Naomba uiondoe thread yako.Ili usipotoshe na wengine pia.

Kutoka Mjengoni
Aluta Continua.

Asante dada Regia kwa correction
 
Sema mama, tunawahitaji watu kama wewe, siku hizi hadanganywi mtu na wala propaganda haiwezekani kamwe.

Ndio sababu naipenda jamii forum ukilinganisha na mitando mingine, Ukweli bila chenga.

Safi saana.

Peoples power.
 
Tunashkuru Mh. Regia kwa kutoa ufafanuzi huu maana kama ulivyosema waatu wengi hatujapata bahati ya kusikiliza bunge na hapa JF ndo tunapopategea haswa kwa taarifa muhimu kama hizi. Ombi langu ni kuwa hata kama mpo bize na shughuli za bunge, mkipata wasaa muwe mnapita pita huku kutupa kinachoendelea huko.
 
kweli mimi nimeangalia.mbowe kampongeza jk kwa kutekeleza jambo lisilokuwa ktk ilani yao.ningekuwa mimi hiyo ilikuwa kejeli.na amewaomba wasione aibu kukopa mengine mazuri.sasa huyo pasco vipi tena?
 
Karibu sana Sister... Tunashukuru kuwa hata ukiwa mjengoni wakati wabunge wa CCM wanasifia umaskini wa taifa hili kana kwamba tuna laana ya kuishi gizani wewe unaboreka na kuamua kujumuika na sisi wana jukwaa wenzako huku bunge linaendelea. Big up mheshimiwa mpe vidonge huyo Pasko, nahisi katumiwa na Tambwe Hiza.
 
Huyu Pasco ana lake jambo, nilimsikiliza mbunge wangu wa Hai kwa makini sana, alimpongeza kikwete kwa hatua ya kuanza mchakato wa katiba.
 
tunashukuru kwa marekebisho but huyu Pasco yupo kishabiki zaidi tunamfahamu na tumemzoea!
 
Mkuu Pasco.Heshima mbele.

Nimeamua kuanzisha thread hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umeufanya hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge.Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema.Kuongeza ni suala la kawaida sana.Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali.Hansard ikitoka nitaweka hapa.

Naomba uiondoe thread yako.Ili usipotoshe na wengine pia.

Kutoka Mjengoni
Aluta Continua.

hapo red&bold.

inaruhusiwa kuweka jamvini?
 
Karibu sana Sister... Tunashukuru kuwa hata ukiwa mjengoni wakati wabunge wa CCM wanasifia umaskini wa taifa hili kana kwamba tuna laana ya kuishi gizani wewe unaboreka na kuamua kujumuika na sisi wana jukwaa wenzako huku bunge linaendelea. Big up mheshimiwa mpe vidonge huyo Pasko, nahisi katumiwa na Tambwe Hiza.

Ki ukweli Bunge limeniboa hasa..Yaani kipindi cha maswali kikiisha sijisikii tena kusikiliza mipasho na vijembe vyao.Jumatatu ifike haraka tumalize kuchangia hii hotuba ya Rais inayotupa nafasi ya kuogeleoa popte unapotaka.
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom