Pasco na waandishi wenzako...

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.
 
Manufaa yapo tumbo zao zipatazo shibe lakini wananchi wanapotoshwa.
OTIS
 
mkuu yani leo ndo nami nilitaka kupenyeza suala kama lako...................kuna wanaSIASA tena vijana pia wamewaweka mfukoni waandishi na wahariri. very sad.
 
Waandishi walipaswa kwanza kusoma na kuwa specilalists kwenye sekta mbalimbali kabla y akuwa waandishi wa habari. Speciality zao zingewapatia kazi zenye heshima na kuacha kuwa ombaomba kiasi cha kuwa wauza taarifa kabla! hivi atoae fedha ili habari yake iandikwe ana uhakika gani mhariri ataikubali au inabidi na mhariri nae apewe bahasha? Jinasueni kwenye uanjanja aliosema JK ili mheshimiwe!!
 
Mimi issue ya akina Pasco imenishangaza sana baada ya rafiki yangu kuambiwa anatakiwa kuandaa bahasha ya khaki ili habari zake zitoke popote.Huyu jamaa analeta suluhisho katika majanga ya moto kwenye hii .Yaani pale maelezo anatakiwa kulipa 60,000 tshs kwa saa moja na ana ambiwa kwa uwazi aandae bahasha kulingana na uzito wa mtu ili habari zile ziandikwe .Hii imenishangaza mno .Hivi hawa waandishi si wako kwa kuandika habari ? Au wewe Pasco na wenzako mko kupata bahasha ndipo muandike na nasikia kama huwezi kumpoza editor unaweza pigwa chini pamoja na bahasha yako kwa mandishi .
Pasco msaada wako tafadhali .
 
Mkuu, kwahiyo na Pasco pia nae ni "mzee wa bahasha za kaki!!?
Kumbeee, ndo maana huwa anatetea MAUOZO!!
Duhh!! Aibu hii Pasco!!
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.
Mkuu Lunyungu, haimhitaji Pasco kujibu kuwa hili halina maslahi ya taifa hata kidogo. Ni tamaa ya hao waandishi kutaka kushibisha matumbo yao tu
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.
Mkuu Lunyungu kwanza pole kwa hii, yote usemayo ni kweli mimi kama mwanahabari, nimeisha vipokea sana hivyo vibahasha na mpaka hapa nilipofika sasa mimi ndio navigawa hivyo vibahasha.

Ila naomba kufuatia msiba mkubwa JF tulionao kwa sasa, Msiba wa Regia Mtema, please lets keep off this topic mpaka baada ya msiba nitakueleza kila kitu na ni kwa nini nasupport hivyo vibahasha, nimevihalalisha na nina vigawa with clear conscious!.
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.

Hapa kweli kuna kazi, hivi tunataka wakati wote habari ziwe za upande mmoja tu? Maanake hapa kuna watu wanataka ziandikwe habari mbaya za upande mmoja tu. Akina fulani wakiguswa inakuwa nongwa! Hakuna mtume wala nabii hapa duniani kwa sasa, tuliopo wote ni binadamu tu. Na binadamu yeyote hawi sahihi wakati wote. Pia hakuna chama cha siasa kilichoshushwa na Mungu, vyote vimeanzishwa na wanadamu. Kwa maana hiyo ikitokea chama chochote kinakwenda mrama ni lazima kiandikwe. Tutakuwa hatutendi haki kwa kutaka ziandikwe habari za upande mmoja tu, ziwe habari mbaya au nzuri. Huo utakuwa si uhuru wa vyombo vya habari. Mbona vyombo hivyo hivyo vya habari, waandishi hao hao tunasema wanakamata bahasha za khaki wakiandika habari nzuri kuwahusu kina fulani hatupigi kelele?
 
Jamani siku hizi hatuna waandishi wa habari, bali tuna waandishi kwaajili ya matumbo yao.

Hivi mwandishi akiandika habari kuhusu fukoto la mgogoro kuhusu chama fulani basi anachukuliwa kama mshika bahasha? Aisee! Kwa hiyo na ninyi wa upande fulani mnachukua bahasha kutoka kule ili mlete hoja za kutetea upande ule wa pili? Acheni watu waandike kile kinachotokea bila kujali kinatoka upande gani.
 
Mkuu Pasco , sasa msiba umepita na Mh.Regia apumzike kwa amani .Naona sasa ni wakati muafaka unipe jibu juu ya wewe na wenzako kupenda bahasha za khaki ili muweze kuandika habari kwa watanzania kujua nini kinaendelea .Karibu tuanzie hapa kwanza maana kwangu nimeshangaa kwamba unahongwa ili uandike habari hata zile ambazo ni za manufaa kwa jamii lakini lazima bahasha ya khaki .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom