Paschal Mayalla: Acheni kulalamika, kubalini mafanikio ya Serikali

Nimemsikia vilivyo na anastahili pongezi kwa kuzidi kuinadi JF live ,alichosema ni kawaida kuwa hapa JF wale madhaifu wa CDM wanaona wale makobe waliomo bungeni wanaonewa ,jambo ambalo sio kweli ,makobe mnasema mpaka mnatolewa nje ,yaani huwa mnashika kasi mpaka mnashindwa kueleweka.
 
mafanikio anayoyasema mayala ni kama yale ya kuwa Tanzania inaongoza katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara kwa kuuza ardhi yake zaidi ya hekta milioni moja kwa wageni nafikiri hayo ndio mafanikio ya serikali anayotaka tuyaone.
 
Katika kukiri JF inawafanya wengi wasilale speaker hii paschal mayala imetumika ku amplifayi kuwa JF wamejaa walalamishi msipinge tu. Katika mtazamo huu anaingia kundi moja la yule mama wa mikocheni kuponda JF


Aje hapa ili aweke mafanikio yoyote kuanzia 2005 hadi sasa ndani ya hii Serikali DHAIFU ambayo yanahitaji kupigiwa makofi na vigelegele
 
Pascal Mayalla naona anaangalia mambo nusu nusu. Sasa hivi kila mtu analalamika, kuanzia waziri mkuu (Jairo gate) hadi wabunge. Arejee hansard ndio ataona ni jinsi gani wawakilishi wa wananchi wanalalamika, na wengi wao wanatoka chama kinachounda serikali. Kwa kifupi, mambo yanaenda kinyume na matarajio ya wananchi na ndio sababu watu wanalalamika.
 
Aje hapa ili aweke mafanikio yoyote kuanzia 2005 hadi sasa ndani ya hii Serikali DHAIFU ambayo yanahitaji kupigiwa makofi na vigelegele

Naanza kabla pasco hajaja:

Mkoloni + Nyerere + Mwinyi + Mkapa = 6,000Km of paved roads.

Kikwete = 11,154 KM of paved roads.

Source: Magufuli bungeni na hansard zipo na hakuna Mbunge aliyepinga kwa kuomba muongozo wala utaratibu.
 
Pasco katoa thread hapo juu kabisa na inachangiwa kila siku halafu mnataka kumkosoa, acheni hizo kwani katika member 82'858 wa leo wa JF siwaoni wengi huenda wameamua kuwa wasomaji tu, kuliko kuwa wabishanaji wa mambo ya kisiasa.
ni sawa kabisa kuna majukwaa mengine yana Amani lakini baadhi kila saa ni ulalamishi wa kitoto tu kwa vile mtu ana laptop, mabile au modem basi atazusha la kuzusha amalize hasira zake
JF mnaliharibu jukwaa
 
Back
Top Bottom