Parking Dar: Kingunge na familia yake ni wasanii?

Sounds like Kinje's Son
Tatizo wengi hujitia kujua vitu, kumbe hawajui chochote...

Mheshimiwa Kibaunango unasikika ni mtu anayekana reality...huoni kuwa zile fedha hazisaidii chochote jiji..hebu angalia mfano Kariakoo kulivyo na traffic jam god forbid kukitokea fire hakuna hata njia ya firebrigade kupita...i believe kama zile pesa zingetumika vyema kungekuwepo mabadiliko.
Awali ya mimi sio msemaji wa JIJI, ila kwa ufahamu wangu mapato yote ya JIJI hutumika kwa mjibu ya bajeti yao. Aidha ni JIJI(watendaji na madiwani) ambao hupanga jinsi ya kuondoa kero mbalimbali katika JIJI. Nafasi ya mwananchi wa kawaida katika kuona matumizi ya Mapato ya JIJI ni yeye mwenyewe kushiriki katika vikao kuanzia ngazi ya wadi hadi kwenye Baraza Kuu la JIJI.

yaani mapato na Kingunge na mkewe na watoto wake unasema iende kujenga Kariakoo ama mimi sijakuelewa ?
Kamanda naona sasa umehamishia majungu na fitna kwenye vidole... Kazi unayo..
 
Hii kampuni ya parking inakusanya karibu shs milioni tano kila siku.Nadhani City council wanatakiwa kulipwa kitu kama milioni.Lakini sasa hao City wenyewe hawalipwi.JK alitaka kumnyang'anya huyo mama hio tenda na kumpa nani sijui.Lakini huyo Mama Kingunge alikwenda kulia kwa JK kuwa wao wamechukua mikopo kwa ajili ya kuweka mitambo ya kisasa kwa ajili ya hio shughuli ya parking.Sasa tunasikia kuwa waliongezewa mkataba kiholela.Pale Ubungo bus terminal,wanakusanya kama milioni kila siku,lakini hakuna maendeleo yeyote pale toka pamejengwa.Yule mama kanunua nyumba nyingi sana masaki,regent estate,maana wanajua kuwa hii dili itakufa anytime.Na habari za ndani ni kwamba hata Kingunge mwenyewe hayuko too keen on the deal,sasa sijui kwa sababu mwenye dili ni mkewe au kwa sababu ya balaa litakalolozuka baada ya kugundulika kuwa kampuni ni ya wakina kingunge.Lakini yule anayesema kuwa Kinje sio mtoto wa Kingunge,hio sio kweli...na wamefanana,tena sana tu
 
Sumae hana 10% ktk huu mradi?

Mie sioni umuhim wa hizi kampuni zinazopewa tender na Jiji kuanzia parking systems, kuzoa taka etc na Malaji kwenda Mbele.
Jiji Wanashindwa nini kufanya wao wenyewe na watu waombe ajira huko. Maana kuweko kwa Hizi kampuni Uchwara ni kula pesa.
Pia Wafanyakazi wa hizi kampuni hawalipwi cha maana, sijui kama wana NSSF.
Hizi ziliwekwa na akina sumae kumpa ndugu yake keenja kula.
Madiwani wetu hawana say. pia wengi elimu zao DUNI so uwezo wa kutetea hoja sijui kama wanao.

Please TUNAHITAJI Clean people. Mlioko UK, London na kwingineko tuambieni kwanini miji hio misafi..mipango mizuri...
 
Hivi nina hasa anayemiliki Tanzania Parking System(TPS)?Kwasababu hapa Dar es salaam hawa jamaa wemekuwa ni watu wenye bugudha na karaha kwa watu wanaomiliki magari. Unakuta barabara,jengo limejengwa na mamlaka nyingine kabisa kukiwa na sehemu ya maegesho ya magari.
Halafu unakuta mamlaka husika haina mkataba wowote na TPS kufanya kazi ya makusanyo ya fedha kwaajili ya hizo
parking(maegesho).
Kwa kifupi TPS haina sehemu ya maegesho kwaajili ya magari ndani ya hili jiji.Hivyo basi,wanachofanya ni wizi;wakitaka kufanya biashara halali wajenge sehemu zao kwaajili ya maegesho ya magari.
Na waliyoipatia TPS kibali cha kufanya hiyo kazi ni wezi na wanastahili kushitakiwa kama wahalifu wengine.
Ninaomba halmashauri ya jiji la Dar es salaam isimamishe mara moja wizi huu wa mchana kweupeeee!
Kwasababu sioni jipya katika kuboresha miundombinu ya maeneo husika pamoja na kutuchukulia fedha zetu.
Wana-JF wenzangu ninaomba tuzungumzie hili kwa jinsi mnavyowaona hawa TPS.
 
Mkuu umenena lakini hivi nikiasi gani kinaenda katika halmashauri baada ya makusanyo?Hii kampuni inahusishwa na familia ya Kingunge kama sikosea ndo kapewa tender ya kukusanya sasa sijui anapeleka kiasi gani kwenye halmashauri na halmashauri inafanyia nini hizi pesa maana wameshindwa hata kufukua tu mifeleji tunapata taabu sana kamvua kadogo kakinyesha chemba zote unakuta zimeziba uchafu ndo usiseme hili bila shaka ni dili la wanene kula pesa za wajinga kweli wajinga ndio waliwao.
 
Kwa nini hawafikirii kujenga parking..........hata moja tu? ndio kusema hawajapata pesa za kutosha toka wameanza kukusanya parking fees?
 
Watajenga wapi?
Wataweza kununua kiwanja mil 900 hao?
Jibu lililo wazi hawawezi zile zinaishia kwenye kamati na wajanja wachache tu.
 
Watajenga wapi?
Wataweza kununua kiwanja mil 900 hao?
Jibu lililo wazi hawawezi zile zinaishia kwenye kamati na wajanja wachache tu.


By the way huhitaji maelfu ya ekari kujenga parking!Pale makao makuu ya

TPS mbona kuna ile sehemu iko wazi, hawawezi kujenga parking ya kisasa pale?

Wangeweza hata kuwashawishi wanaojenga majengo mapya kuwa na parking hata ya magari 100 tu! Utatizo wa tatizo la parking hapo downtown sio zito kihiiiiiivyo.
 
Unategemea jipya au ufanisi wowote kwa Kingunge Ngombale Mwiru na Kinjekitile???!!!! Mtoto wa mama wa mjini anaweza kazi gani???!!! Mliosoma na Kinje you have it all!!!!

Kule Ubungo Bus Terminal ilipoanza walikuwa walipa manispaa like 8m per month (habari za kuambiwa not researched) but kwa siku wanakusanya over 10 million Ubungo pekee!!! Achilia mbali kodi za vibanda pale na kulaza magari!!!! So you can imagine of the healthiest earning there but kiduchu jiji/manispaa inapata. Wakati mwingine nafikiri wanfanya deal na big shots nao wanapata mgao na mgao kidogo kwa manispaa husika. Kwa hivyo basi, kazi za kifisadi huwa siyo fanisi. Halafu kinachosikitisha hawa vibarua wa parking (wanakusanya fedha kwenye points) wanashirikiana na vibaka kuiba car accessories. Ni watu hatari sana. Be aware of them. Tena kama umepaki afadhali mtafute hata mshona viatu jirani na gari yako kama atakuwepo mpe kitu kidogo cha asante ili akulindie gari yako. Wananikera.
 
Maane, tukubali yaishe? huko TPS na Ubungo bus terminal mtoto wa mjini aendelee kupeteshwa?
 
Kwa nini hawafikirii kujenga parking..........hata moja tu? ndio kusema hawajapata pesa za kutosha toka wameanza kukusanya parking fees?

Mama, hawa tps wamekuwa kero na kidonda ndugu kwa muda mrefu sasa. Hawana lolote wanalofikiria zaidi ya kutuibia mchana kweupe. Sijaona eneo lolote katikati ya jijini ambalo wamelitengeneza maalum kwa ajili ya maegesho ya magari zaidi ya kuchuma wasipopanda!
 
Mama, hawa tps wamekuwa kero na kidonda ndugu kwa muda mrefu sasa. Hawana lolote wanalofikiria zaidi ya kutuibia mchana kweupe. Sijaona eneo lolote katikati ya jijini ambalo wamelitengeneza maalum kwa ajili ya maegesho ya magari zaidi ya kuchuma wasipopanda!

Okay, kwa nini wanaDar wameamua kunyamaza juu ya hiyo kero ? Wanadumisha amani na utulivu na kuamua kuishi na maumivu ya kidonda ndugu ?

Je kuna yeyote amewahi kuhoji kwa nini parking hazijaendelezwa miaka yote hiyo ya TPS ?
 
Hii sasa ni wake up call kwa tunaotumia na hata wale wasiotumia hii huduma fake ya hawa jamaa.
 
Tatizo la kuegesha magari ni sugu sio tu Dar e salaam bali hata majiji megine kote ulimwenguni. Njia mbalimbali zinachukuliwa kwa maksudi ili kuweza kuboresha huduma wa mijini.
1. Kila anayejenga jengo jipya refu basi atenge parking ya wakazi/watumiaji wa jengo Anaweza kuweka basement na ground floor.
2. wawekezaji mahsusi wanaweza kuwekeza katika kujenga majengo ya kuegesha magari
3. mamlaka husika ni lazima itenge sehemu kadhaa wa kadhaa ambazo watu wataegesha magari kwa malipo.
4. ili kuzuia msongamano wa magari katikati ya jiji barabara zipanuliwe

KITENDAWILI NI UOZO NA KUTOJALI KWA MIPANGO MIJI!!!!
 
Pinda aumbua familia ya Kingunge

2009-03-13 14:17:27
Na Restuta James​

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshuhudia mkataba mbovu unaonukia ufisadi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT), jijini Dar es Salaam.

Ufisadi huo unafanywa kupitia mkataba uliofikiwa kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Mkandarasi, kampuni binafsi ya Smart Holdings, inayomilikiwa na familia ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Kingunge Ngombale-Mwiru.

Mkandarasi huyo alipewa zabuni ya kukusanya mapato kituoni hapo na amekuwa akifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Kwa mujibu wa Meneja wa UBT, Fadhili Izumbe, katika mkataba huo, mkandarasi huyo hulipa Sh. milioni 1.5 kwa Halmashauri ya Jiji hata kama atakusanya mapato ya Sh. bilioni 1 kituoni hapo kwa siku.

Waziri Mkuu alishuhudia ufisadi huo alipotembelea kituo hicho jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika Jiji la Dar es Salaam, iliyoanza juzi.

Pinda alishangazwa na kushtushwa na utendaji mbovu wa uongozi wa UBT, mkataba huo na namna mkandarasi huyo alivyopatikana.

Alifikia hali hiyo, baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Abubakari Kingobi, kuhusu hali ya utendaji wa uongozi wa UBT, ukusanyaji wa mapato, mkataba wa mkandarasi na maendeleo ya kituo hicho.

``Kituo hiki ni kikubwa sana, kuna maswali mengi ninawauliza hamna majibu. Hizi hela mnazopata ni kwa manufaa yenu au wananchi? Mmempataje huyu mkandarasi? Mikataba ikoje? Naomba kujua,`` alisema Pinda.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Kingobi hakuweza kujibu lolote, badala yake akamwita Meneja wa UBT, Izumbe ambaye naye hakutoa majibu, badala yake aliishia kusema: ``Aah!``

Katika taarifa yake, Izumbe alisema kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi huyo hutoa Sh. milioni 1.5 kwa Halmashauri ya Jiji kwa siku, taarifa iliyomshangaza Pinda na kumfanya ahoji: ``Hata kama anakusanya Sh. bilioni 1 anatoa Sh. milioni 1.5? Na kwa nini mkataba utamke shilingi badala ya asilimia?``


Kutokana na hali hiyo, Pinda aliiagiza Halmashauri ya Jiji na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuupitia upya mkataba huo ili kuondoa maswali yasiyokuwa na majibu.

Kwa siku mabasi zaidi 400 husafirisha abiria kutoka UBT, teksi 100 na watu zaidi ya 2,000 huingia. Pia kuna maduka ya vinywaji (Baa na Grosari), maduka ya kawaida, hoteli, `vioski`, gereji, ambavyo vyote hulipa ada za viwango mbalimbali.

Naye Katibu wa Kamati ya Ulinzi UBT, Kibakuli Ngonyani, alimweleza Pinda kuwa askari mgambo wamekuwa wakishirikiana na wezi na ndio maana wimbi la wizi limeongezeka kituoni hapo. Pinda aliagiza tatizo hilo lifanyiwe kazi mara moja.

Akiwa katika soko la Tandale, Pinda aliiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuweka uongozi mpya ili mapato yanayokusanywa sokoni hapo yaongezeke.

Pinda aligiza suala hilo baada ya kutoridhishwa na uongozi uliopo, ambao umekuwa ukikusanya Sh. milioni 1 kwa mwezi, huku soko likikabiliwa na ukosefu wa umeme, maji, vyoo na miundombinu mbingine.

``Hela zinazokusanywa ni nyingi, lakini zinawanufaisha wachache,`` alisema Pinda.

Kuhusu maji yanayojaa katika eneo la Msasani Bonde la Mpunga, Pinda alisema tatizo hilo liko ndani ya uwezo wa serikali na akaahidi kulifanyia kazi.

Hata hivyo, aliiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kwamba wanapotoa vibali wahakikishe wawekezaji wanafanya tathmini ya mazingira katika eneo hilo.

Mkazi wa eneo hilo, Godfrey Bagenda, alimweleza Pinda kuwa wananchi wenye asili ya Kiasia wamekuwa wakiwanyanyasa na kusema kuwa kuna siku watadai haki zao kwa nguvu.

Katika ziara ya jana, Waziri Mkuu alitembelea eneo la Kigogo, ambako wakazi wake walionyesha kukerwa na dampo lililoko katika eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo, Pinda aliagiza dampo hilo liwe limehama ifikapo Septemba, mwaka huu.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom