Paradox: Mgomo wa MDs unawadhuru Wangonjwa; Kufutia Usajili MDs kunasaidia wagonjwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Hoja kubwa ambayo imekuwa ikitolewa na wale wanaopinga mgomo wa madaktari ni kuwa mgomo una madhara ya moja kwa moja kwa wagonjwa na hasa upatikanaji wa huduma ya afya. Wanaopinga mgomo wa madaktari wanasema "madaktari hawana uzalendo" na wanafanya hivyo kwa kuendekeza "pesa" na siyo "wito wao". Wanatuambia - ndugu zetu hawa - kuwa mgomo wa madaktari una madhara ya moja kwa moja kwa wagonjwa na kuwa "madaktari wanawatoa kafara wagonjwa" kwa kuamua kugoma. Hoja zao tunazielewa hata kama hatuzikubali baadhi yetu sisi.

Hoja yao hiyo ingekuwa na nguvu na kuonesha ukweli kama ndugu zetu hawa hawa wangekuwa wa kwanza kulaani kitendo cha serikali kuanza kuwafutia usajiri madaktari na hata kuwaondoa kazini. Mtu mwenye hekima anajiuliza kuna tofauti gani basi kati ya mgomo wa hiari wa madaktari na amri ya nguvu ya kuwaondoa madaktari kazini? Kuna tofauti gati ya kimatokeo (consequential difference) kati ya daktari kugoma kutokwenda kazini na daktari kufutwa usajili wake na asiende kazini? Mgonjwa anaona tofauti gani?

Utaona hoja inayotolewa ni ya kuwakomoa madaktari. Kwamba "kwa vile serikali ilitaka mrudi kazini katika mazingira yale yale na kwa masharti yale yale nanyi mkakataa basi tunawakomoa ili tuone mtatumia elimu yenu wapi!". Sasa hili ni zuri kwenye kulipiza kisasi lakini kiakili halina mantiki, ni woga, na matumizi ya ubabe wa serikali (the tyranny of the government). Lengo ni kutaka kupigiwa magoti, kubembelezwa na hatimaye kuwafanya madaktari hawa - wengi vijana - wawe katika hali ya kukata tamaa (desperation) ili hatimaye mmoja mmoja waje kuomba msamaha na wakubali kurudishiwa usajili kwa masharti makubwa zaidi! Ni mbinu hii hii kwa wale waliosoma Boarding school wanaikumbuka hutumiwa na shule kuwarudisha wanafunzi walioleta vurugu; pale ambapo shule inawafukuza halafu ili warudi basi wanatakiwa kuweka sahihi makaratasi ya kutojihusisha na vurugu au masharti mengine magumu. Wanafunzi wanaokubali masharti hayo kimsingi wanajifunga utumwa; hawawezi kulalamika - bila kujikuta wanakumbushiwa walichotia saini!

Hivyo basi tunaweza kuona pia tofauti nyingine kubwa; madhara ya kuwafutia madaktari usajili au kuwatimua kazini ni makubwa zaidi kuliko madhara ya mgomo wa madaktari. Nitarudia sentensi hiyo na ninatumaini watu itawafikirisha kidogo: madhara ya kuwafutia madaktari usajili au kuwatimua kazini ni makubwa zaidi kuliko madhara ya mgomo wa madaktari. Madhara haya kwanza ni kwa wagonjwa na pili yanaingiza mchakato mwingine kabisa. Lakini zaidi ni madhara ya hatari kwa sababu kama madaktari wakiwa majasiri na kuamua kujiuzulu na kutojali usajili waliokataliwa na wakaamua bora warudi kulima kuliko kulazimishwa kufanya kazi kwenye mazingira magumu serikali haitokuwa na jinsi isipokuwa kurudi nyuma na kuwa itakuwa imepoteza hazina kubwa na kwa hakika itaingia gharama kubwa zaidi kuwa-replace hawa kuliko kama ingekaa na kukubali madai yao ya msingi!

Hoja ya kwamba madaktari wangeendelea kurudi kazini wakati "serikali inashughulikia matatizo yao" ni hoja yenye kuvutia dhaifu wa fikara. Matatizo ya madaktari siyo sawa na kero za muungano ambazo kwa miaka hamsini zimekuwa zikishughulikiwa kwa uvivu. Matatizo ya madaktari na hasa changamoto ya sekta ya afya ni wazi sana - maslahi, vitendea kasi na mazingira ya kazi. Kimsingi hayo matatu tu yanahitaji sera inayoeleweka na ambayo inazingatia unyeti wa sekta hii. Kufikiria sekta ya afya na fani ya udaktari kama fani nyingine ni kukosa kabisa kuelewa vitu vinavyoitwa "vipaumbele".

Binafsi ninaamini mgogoro mkubwa wa sekta yetu ya afya unasababishwa kwa sababu serikali imeng'ang'ania kujihusisha na utoaji wa huduma ya afya na hasa uajiri wa madaktari. Sielewi kwanini bado serikali inataka kuendessha hospitali nyingi hata za chini. Binafsi naamini mojawapo ya vitu ambavyo serikali ingeweza kuvifanya vizuri ni kuendesha hospitali za rufaa tu na vituo vya afya ya msingi na kuachilia huduma zote za katikati na mahsusi kufanywa na sekta binafsi. Serikali ingeweza kabisa kutengeneza mazingira mazuri kwenye afya ya msingi na mazingira mazuri kabisa kwenye rufaa. Madaktari na taasisi bbinafsi zingeweza kutoa huduma ya afya nyingine - isiyohusisha rufaa (na hata rufaa) lakini ikipunguza mzigo mkubwa wa serikali.

Leo serikali inapata mzigo mkubwa kwa sababu inajaribu kuendesha mambo mengi kutoka serikali kuu; halmashauri, polisi, magereza, maji, elimu, ulinzi, tawala za mikoa vyote vinaendeshwa toka serikali kuu. Matokeo yake serikali kwa kweli haiwezi kuhudumia sekta nyeti kama ya afya kwa uzuri zaidi. Na kuamua kuwafuta usajili madaktari hakusaidii kabisa kuondoa tatizo lilipo bali kunalichochea kwani kunajengwa katika hoja kuwa - madaktari watasalimu amri na kuja kuomba radhi. Sasa kama madaktari hawaombi radhi na baada ya kuona serikali inaamua kuwafutia wenzao usajili wakaamua kujiuzulu ili kulinda haki zao serikali itafanya nini?

Ikumbukwe kuwa punda hubeba mizigo kwa muda mrefu na huweza kwenda umbali mrefu na mizigo mingi tu. Lakini punda naye ambaye husifiwa kuwa ni "mnyama wa kazi" naye huchoka. Na kuna wakati - kwa wale waliowahi kufuga punda wanajua hili - punda hugoma. Haendi kwa fimbo, upinde au ulimbo! Sasa punda akigoma hata umtukane vipi au umshawishi kwa fimbo haendi! na akitaka kukuudhi zaidi - na sijui wanawajuaje - punda hukaa chini kukuonesha tu kuwa haendi unakoktaka aende hadi umpunguzi mizigo.

Madaktari wetu wamekuwa kama punda; wameenda na kwenda na kubebana na kubeba na sasa nina wasiwasi kuwa wanaweza kukaa chini na kusema "screw this!". Na wakifanya hivyo, siyo usajili wala udahili utakaoweza kubadilisha na kimsingi kulazimisha serikali kuanza upya.

Vyovyote vile ilivyo, uamuzi wa kuwafutia madaktari usajili ili kuwalazimisha kurudi kazini ni uamuzi wa kiwoga, wa kibabe na ambao umejaa kushindwa ndani yake. NI uamuzi unaoonesha upeo wa uwezo wa watawala wetu kutatua matatizo yetu. NI uamuzi ambao unahitaji kupingwa na kulaaniwa kwani unakwepesha matatizo. Kwani, hata madaktari wakiamua kurudi na kufanya kazi kwa kuhofia usajili wao kufutwa bado matatizo ya msingi yatakuwepo pale pale na bado yataendelea kuchemka chini kwa chini (simmer).

Na kwa kadiri matatizo bado yanafurukuta basi bado migogoro itatukuta.

Na. MMM
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi


Bilashaka hapa umechanganya uwelewa. Madaktari na wanaharakati ni makundi mawili tofauti. Bado hatujasikia kama kuna wanaharakati wamejiuzulu kutokana na mgogoro huu.
 
Bora wa-Resign watakuja wengine hao wanaotaka 7.7m wa nini jamani?
Walijiuzulu Mawaziri wakaja wengine sembuse hao MaDr wasio wazalendo!
Kwa nini humu ndani mnawatetea wakati mambo yalishaisha, na waliambiwa kuwa atakayeona anaonewa na kupewa ujira mdogo NI BORA AJIONDOE mwenyewe na sio kuanza kuleta chokochoko na Serikali yenu. Serikali yenu haina uwezo wa kuwalipa wanavyotaka wao

una matatizo wewe! unadhani daktari ni sawa na Waziri..sio kila mtu anaweza kuwa daktari wewe!! na wenye upeo mdogo kama wako wanadhani hapa ni kutetea, hakuna ushabiki ..lete facts kama great thinker..
 
Wewe inaelekea humtakii mema huyu mkweree, kwani ushauri unaompa unamfaa tu kiongozi asiyekuwa na hekima na busara na kiongozi kama huyo mwisho wake ni mbaya!!!!
Bulesi usihangaike na KIMOLO kwani haumjui vema? sema tukuwekee CV yake hapa uone alivyo mtupu
 
Vyombo vya Habari na mitandao ya habari kuna Habri yenye kichwa Taarifa kwa UMMA kuwa madaktari zaidi ya 300 wamefukuzwa na kufutiwa usajiri
Inanipa taabu sana kwanza kuletewa au kutangaziwa habari hii sisi umma wa Watanzania . unatupa hii taarifa hili iwe nini ? hilo ndilo swali kubwa , Serikali mnatuletea hii taarifa hili tufurahi kuwa mmeshinda game hii, kwamba baada ya kufukuza hawa watu mia tatu sasa mambo ni shwali tutatibiwa sasa vizuri zaidi na je hawa watu 300 walikuwa hawana umuhimu wowote kwa hiyo hata kama hawapo mambo ni safi tu. Nchi ya ajabu sana kama watu wawili tu eti viongozi wantengewa mabilioni ya shilingi ya kwenda kutibiwa nje na utitiri wa watu wanakufa bila tiba kwa kukosa vifaa ! laana hii mtaitoaje ? ndio maana nchi ya utajiri kama Tanzania imelaaniwa watu wakee wananuka umaskini , watu wamekuwa maskini hata mawazo ? mtu anadai umlipe mil 3, analala wodini na kushika vinyeshi na damu zenu hammwonei huruma mnasema wapi tutapata pesa za kumlipa ? mwekezaji nakuja anachukua mali yako kwa asilimia 97 wewe anakupa 3 unasema ahasante anakuacha na ubwege wako unasema huna pesa za kulipa.
Hospital ndogo tu ina vifaa na vitendea kazi kibao , sisi hospital ya taifa watu wanalala chini mnaona akili tunayo ?
Mimi nadhani viongozi wetu wana ubia na hospital za Private ndio maana hawajali watu watatibiwa wapi, Kwa ni i Aghakan iwe na vifaa vyote na Muhimbli ikose ? Kwa nini huduma za Aghakhan ziwe ghali sana na serikali isiitoze kodi kwa nini ? Mimi naona kuna mshiko kwa viongozi na ndio maana wanapenda kutoboresha huduma za afya hili wakatibiwe nje na humo kuna percentage yao
Nini Kifanyike ? Chonde Chonde wananchi , hasa wabongo ni kwa nini tusifanye Harambee tukachangie vitanda katika hospital zetu hasa Muhimbili ? kwa nini watu walale chini ? kwanini watoto walale mchongoma
?
Safari moja ya Rais nje inatosha kununua vitanda vyote katika hospital za Dar es salaam
tutafakari na kuchukua hatua mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuchangia vitanda 2 kama kuna mtu anaweza kuratibu hii kitu. Jamani Tuondokane na Aibu hii
 
Uongo mtupu. Mnatamani mabalaa lakini sisi huwa tuna duwaa hii:

Qur'an 113

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU


1. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko,


2. Na shari ya alivyo viumba,


3. Na shari ya giza la usiku liingiapo,


4. Na shari ya wanao pulizia mafundoni,


5. Na shari ya hasidi anapo husudu.
Ficha dua zako za kuku, onyesha uzalendo wako!
 
Kwa hiyo hii movement ilikuwa kuondoa utawala? au ni kwa ajili gani. Nisaidie

Kama ni kweli busara ni kuweka koti begani, stethescope mkononi nenda kijiweni. Muulize Dr Kibassa alishagoma tangu mwaka 2005 na aliamua kuwahudumia waTZ kutokea private, hakuna tatizo, kwani lazima public?
Nasikitika sana nikikumbuka chanzo cha mgogoro huu, pale inteni walipocheleweshewa mishahara yao wakagoma kushinikiza walipwe, baada ya kulipwa eti wakasimamishwa na kazi!!!!!!.........kuwasimamisha kazi sijui selikali walimaanisha nini? kuwakomoa? mgogoro huu selikali iliumisimeneji tangu mwanzo lakusikitisha zaidi sioni mwenye hekima hata mmoja aliyebaki selikalini naona wooote wana mtazamo wa kushindana nakukomeshana komeshana tu wamepungukiwa na hekima kabisa!!!!!!
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi

Kuna tofauti kati ya daktari( anatibu, kushauri kuhusu masuala ya afya, kutoa elimu) na mwanaharakati(anayetetea haki za wanyonge, anayesimamia haki) ..unaposema wanatumia wagonjwa kama bomu, unapaswa kuelewa wewe hukumwajiri daktari..
1.uliwachagua viongozi wasimamie afya na mambo mengine ktk nchi
2.kwa kulipa kodi unapaswa kupata huduma ya afya
3.serikali iliajiri madaktari
4.Kama kuna mgogoro unapaswa kuwadai serikali( ulioingia nao mkataba kwa kulipa kodi na kuwachagua katika uongozi)
5. ukija ktk suala la madaktari ni bora kujua madai ya madaktari na si kusikiliza madai potofu kutoka kwa serikali)
 
jk kiboko kweli. eti madaktari wanajiuzulu au wanaacha kazi? kwenda kwenda hatutaki upuuzi wao,
 
Mtaongea mengiii........! Mwenzenu yuko UK anafundishwa namna ya kuvaa Kondom!
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi
Madaktari hawapiganii vitanda vya kutosha maodini ili wavilalie wao!, hawatafuti dawa za kutosha ili watibiane wao na familia zao!, ni lini mtaacha kuwekeza india na kujenga kwenu? vilivyoko India vilijengwa havijadondoka kutoka juu jengeni kwenu bwana!.
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi

duh!toka lini Dr. Akawa mwana harakati???
 
Akirudi nyuma ataonekana dhaifu! Hivi lengo ni kuonyesha ushupavu au kutatua tatizo? Kwa nini kung'ang'ania ushupavu wakati ukweli unaonyesha ni dhaifu. Serikali au raisi akaonekana sio tukio moja ni mtazamo wa mambo mengi hivyo sio rahisi akajionyesha ushupavu kwa jambo moja la leo tu. Sanasan ataonekana kituko zaidi
 
na wengine wanaenda kazini lakini hawatoi huduma. Wanazunguka corridor hadi muda wa kutoka kazini. Mwingine anasimulia hospitali ya mkoa haina chumba cha upasuaji, kazi yake kuandika rufaa, amekata tamaa ya kazi,
 
Back
Top Bottom