Paprika: Paprika: Paprika: Paprika

rollingstone

Member
Apr 1, 2012
29
1
Jamani wanajamiiforums, naomba msaada wa soko la paprika. Nina tani kati ya 50 hadi 70 kuanzia mwezi july. Kama kuna mtu anahitaji naomba msaada.
 
Rollingstone,
Miaka michache iliyopita niliwahi kukutana na Kampuni iliyoitwa Spices Tz Ltd. Hawa walikuwa Wa-Dutch walioshughulika na utoaji wa mbegu za kilimo hai cha Paprika, ukuzaji wa zao na ununuzi nyanda za juu kusini. Walikuwa na mikataba na wakulima maeneo ya Kilolo-Iringa na walikuwa wanauza moja kwa moja kwenye Kampuni yao Mama huko Uholanzi. Kwa taarifa niliyopata ni kwamba hii Kampuni haikupata ikipata mzigo wa kutosha katika misimu na hivyo kuamua kufunga biashara Tz. Wapo sasa Malawi na Msumbiji wanafanya kazi na Cheetah Co. Jaribu kusearch Cheetah Paprica na uwasiliane nao. Ukikosa mawasiliano, ni-PM J3 nikutumie.
 
Rollingstone,

Miaka michache iliyopita niliwahi kukutana na Kampuni iliyoitwa Spices Tz Ltd. Hawa walikuwa Wa-Dutch walioshughulika na utoaji wa mbegu za kilimo hai cha Paprika, ukuzaji wa zao na ununuzi nyanda za juu kusini.

Walikuwa na mikataba na wakulima maeneo ya Kilolo-Iringa na walikuwa wanauza moja kwa moja kwenye Kampuni yao Mama huko Uholanzi. Kwa taarifa niliyopata ni kwamba hii Kampuni haikuwahi kupata mzigo wa kutosha katika msimu na hivyo kuamua kufunga biashara Tz.

Wapo sasa Malawi na Msumbiji wanafanya kazi na Cheetah Co. Jaribu kusearch Cheetah Paprica na uwasiliane nao. Ukikosa mawasiliano, ni-PM J3 nikutumie.
 
Mkuu uko Mkoa gani? Kama uko Arusha itafute kampuni moja inaitwa FaidaMali, au Faida Market Linkage company, wameisha fanya sana linkage katika hiyo kitu, Ila mkuu wakati mwingine usilime kitu bila kujua utamzuia nani, make hata kama utapata soko mnunuzi ndo atakae kupangia bei na si wewe,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom