Pappy Kocha na Nguza Vicking

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,457
154,323
Mko wapi wapenzi wa Nguza Vicking na mwanae Pappy Kocha?
Mlikuwa mnasimamisha magari yenu mkiwaona wakipita, mlipeana mikono na kuwanunulia bia. Yap, mlifanya vyema sana. Sasa shilingi imepinduka, kama mlikuwa mnaona sura zao sasa oneni na visogo vyao.
Mwende mkawatembelee kwenye shida zao. Bia ni bei kubwa kuliko sabuni, wapelekeeni rafiki zenu sabuni ili waoge na kufua. Kawaangalieni rafiki zenu ili wafarijike.
Leo unapeta uraini, kesho itakuwa zamu yako kuwa mfungwa, jifunze kuwa rafiki wa kweli.
ACHA UNAFIKI NA UZANDIKI
 
Umesema kweli ila issue kama ile ya babu seya unaweza usitembelewe hata na mwanao.hebu fikiri ingekuwa mwanao ndo kaliwa masaburi ungemtembelea?tunajua jela hakuna mwenyewe ila hili la babu seya linatisha sana na sio kidogo wala uzandiki.
 
Nakuunga mkono Ndoano...laiti ungewaona wale watoto 7 waliofanyiwa vile vitendo (mimi niliwaona kwa sababu nilikuwa nafanya kazi wadi ya watoto Muhimbili wakati ule), na sina huruma yeyote kwa babu Seya na wanae, na ingekuwa mmojawapo ni mwanangu...ningekuwa nishanyongwa tayari!
 
Hivi wanae walioachiwa wako wapi mbona hatuwasikii?
 
Swala la babu seya gumu sana. Matendo aliyofanya haitaji msaada wowote.
 
ni juma lililopita tu nilipodhiirisha fikira zangu za siku nyingi kuwa zaidi ya asilimia sabini (+70%) ya watu walioko magerezani hawatakiwi kuwa huko.
Mfumo wetu wa sheria umefikia wakati mbaya kabisa katika historia ya nchi hii iliyo na utata!
Ni bora tungerudi kwenye mfumo wa kutafuta haki (kama Rwanda walivyofanya kwenye 'Gachacha') badala ya sheria ilipofikia kwa sasa!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom