Papaa Musofe mbaroni kwa mauaji!

Hata kama atatoka kwa pesa, lakini muda atakaokaa huko utamfanya kutafakari kuwa kumbe wakati mwingine pesa sio kila kitu vinginevyo angenunua mtu wa kukaa lumande kwa niaba yake wakati kesi inangojea kupelekwa mahakama kuu!
Umeona mkuu eee, hii inshu imemkalia vibaya lazima somo lieleweke safari hii. Akifanikiwa kuchomoka lazima mtu mzima abadilike lakini pia kiburi cha aina hiyo huwa wanaishia kufa vibaya. Utoto wake wa mjini utamjutisha.
 
Umeona mkuu eee, hii inshu imemkalia vibaya lazima somo lieleweke safari hii. Akifanikiwa kuchomoka lazima mtu mzima abadilike lakini pia kiburi cha aina hiyo huwa wanaishia kufa vibaya. Utoto wake wa mjini utamjutisha.
ile kauli ya 'ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga' ina maana pana kweli ila ukiangalia hapo on red&bold ni kuwa maisha yana misingi yake na ukiifuata daima utakuwa awarded hivyo hivyo bila kujali kama una pesa au huna lakini uki tress pass na kufanya mambo mengi chini ya kapeti mara nyingi unakuwa revealed kabla hujamaliza muda wako katika dunia hii!
Naanza kuiamini hii kauli kutokana na matukio mengi niliyoshuhudia na huyu 'mkuu' ndiko anako elekea huko kama sio kufika!

 
wala usijali hawa ni kawaida sana kuwa na makesi mengi mahakamani na polisi,siku zote wanaishi kwa pesa za kutapeli wengine na wako tayari kukuua kupunguza kero maana hawako tayari hata kurudisha......pia wako wale wa uchwara wao wanatapeli mpaka laki 5 na kudhulumu watu km kina Shomari kimbau anavyodhulumu mabondia anaowapiganisha bila kuwalipa na wngine wengi tu.....na huwa wanatumia gharama kubwa tu kujifisha na kuhonga polis
 
Sana tu mkuu, huwezi kuwajuwa hawa kama wewe si mutoto ya mujini,kwanza utawaona wapi? Kariakoo kwenye vumbi kamwe huwezi kukutana nao hawa.

Hahaaaa....kamwe huwezi kumjua Msofe kama ww si mtoto wa mjini!
 
ooooh brother kamdedisha nani tena aaah sa ntapata wapi ugali wa kilasiku ngoja nikamcheki umwerani migomigo
duu kweli malipo ni hapahapa kawaumiza watu weeeeeeeeee sas zam yake.le grand mupao mutu ya pakee duh
rest in peaces brother

na kumuua umeamua kumuua kabisaa duh kweli mopao amekwisha
 
Kutokana na hukumu iliyotolewa, je mahakama imetenda haki? manake hii iliwahi kujadiliwa humu wakuu.
 
Kutokana na hukumu iliyotolewa, je mahakama imetenda haki? manake hii iliwahi kujadiliwa humu wakuu.
Hukumu imetoka imekuwaje? Last time mahakama ilikuwa ikimsubiri shahidi wa muhimu ambaye ni Alex Massawe.
Inamaana Carlos alishatimba bongo na kusimama kizimbani.
Kah! Haya mambo vipi jamani?
Haki ya mama Yule iko wapi???

Cc: @Matola @king kong 11 @lukindo
 
Da!chuma ya reli haipati kutu papaa musofe...jamaa kawaumiza sana watz wanyonge yeye na Alex Masawe

halafu cha kushangaza badala ya watu humu kuguswa na ukatili au upuuzi aliowafanyia watanzania na hao wageni kuna watu humu humu tena katika huu huu uzi wanamsifu kana kwamba vitendo vyake vya kiuhalifu wamevihalalisha. kweli watanzania tuna safari ndefu katika kujitambua na kujua kutimiza wajibu wetu. mhalifu anasifiwa kushinda hata yesu kristo anavyotuhangaikia kutuombea na kutusamehe dhambi zetu! nimesikitika sana na nyie mnaomsifia na kumpamba laiti mngeyajua ya kiundani ya huyo jamaa mngeenda tu mapema kutubu kwa Mwenyezi Mungu.
 
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar, mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mwaka 2011.

Kesi hiyo iliyounguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa kumiliki nyumba hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.

“Pia mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.

Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu ambacho hakuwa akikitarajia.

“Yaani siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba, nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.

Msofe na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba 288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni 30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom