'Papa wa Kanisa Katoliki Atakayefuatia Atatoka Afrika'

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Tuesday, October 13, 2009

Mmoja wa makardinal wanaoheshimika barani Afrika toka Ghana amesema kwamba hakuna shaka kuwa Papa wa kanisa katoliki atakayefuatia atatoka barani Afrika.

Baada ya kuchaguliwa kwa Barack Obama kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani, kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson toka Ghana ambaye amepewa jukumu la kuongoza vikao vya kanisa katoliki vinavyoendelea mjini Vatican amesema kwamba hakuna sababu yoyote itakayozuia Papa wa kanisa katoliki atakayemfuatia Papa Benedict kutoka barani Afrika.

Akiongea na waandishi wa habari jumatatu, Turkson alisema kwamba wakati umefika wa kuwa na Papa mweusi toka Afrika.

Akitolea mfano wa aliyekuwa katibu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ambaye naye anatoka nchini Ghana, Turkson alisema kwamba Annan alikabiliwa na matatizo mbali mbali lakini alifanikiwa kumaliza muda wake kwa mafanikio.

"Kwa kuwa makanisa ni ya Mungu, kama Mungu atataka tuwe na Papa mweusi, tutamshukuru sana".

Suala la kuwa na Papa kutoka barani Afrika limekuwa likizungumziwa kwa miaka mingi sasa na sababu kubwa ni kwamba Afrika ndiko ambako kanisa katoliki linapoonyesha uhai.

Kati ya mwaka 1978 na mwaka 2007, idadi ya wakatoliki iliongezeka barani Afrika kutoka milioni 55 hadi milioni 146.

Kinyume chake idadi ya waumini wa kanisa katoliki barani ulaya imekuwa ikizidi kupungua siku hadi siku.

Mwaka 1978, Papa John Paul aliyezaliwa nchini Poland, ndiye aliyekuwa papa wa kwanza kutoka nje ya Italia baada ya miaka 455.

Alipofariki, mwaka 2005 makardinal walimchagua Papa Benedict XVI aliyezaliwa nchini Ujerumani kuwa Papa.

Pamoja na Afrika kuwa na waumini wengi wa kanisa katoliki, makardinal wengi wanatoka barani ulaya na haijulikani kama kweli wataweza kufumbua macho yao na kulipa nafasi bara la Afrika.

Hata hivyo Papa Benedict mwenye umri wa miaka 82 anaoneka ni mwenye afya njema hivyo itabidi waafrika wasubirie kidogo kuanzisha mjadala wa ujio wa Papa toka Afrika.

Papa mpya huchaguliwa baada ya Papa aliyepo kufariki dunia.

Source:
NIFAHAMISHE.com
 
sijui kama kuna ukweli wowote kwenye hii, kwa uelewa wangu mdogo huwa najua papa huwa hakuna uchaguzi au kupiga kura kama rais anavyopatikana
 
Source: NIFAHAMISHE.com
I believe this cardinal went in the conclave during which Pope Benedict was elected.Sio rahisi kiasi hicho kuchagua papa. Historia inaonyesha mara nyingi wanaochaguliwa si watu wenye majina makubwa. Inasemekana Pope John Paul II aliwahi kutamka kuwa ni ngumu kupata papa kutoka afrika kwa sababu ibada zitageuzwa sehemu za kucheza dansi na utamadunisho ulioanzishwa.
Huwa kuna kazi kubwa sana kupata papa maana inataka ushawishi mkubwa kwa wale wote watakaoingia ndani ya conclave, na ni lazima uwe mtu ambaye makadinali hawatakuwa na mashaka mashaka ya nini kitatokea mbele ya safari.Labda ameshapiga mahesabu ya yale yatakayotokea. Ila mhhh.!!
 
Yeyote anayefaa atachaguliwa kutoka bara lolote, na wala huwa hakuna kinyongo. Si lazima upapa utolewe kwa zamu, inategemea na majibu ya maombi wafanyayo makadinali.
 
Hili ulilosema ni jambo la maana sana
 
Pamoja na Afrika kuwa na waumini wengi wa kanisa katoliki, makardinal wengi wanatoka barani ulaya na haijulikani kama kweli wataweza kufumbua macho yao na kulipa nafasi bara la Afrika.

Yote hayo ni maneno. Papa kutoka Africa labda baada ya karne moja.
 
jamani papa si huwa hawastaafu ni mpaka wafe? mbona nyinyi mnaongelea habari za papa mpya wakati huyu baba wa watu hajafa? mmemchoka kihivyo? au mnamuombea kifo?
 
Inawezekana kwani kanisa katoliki i kama ccm kazi yao kufisadi vitu.wanagombania kunywa wiski,kiongozi wa dini anakunywa pombe wamefulia kidini.

Na mtachonga gega mpaka midomo iende upande mwaka huu..Yanaonekana Kanisa Katoliki lawachoma sana eehh?
 
Back
Top Bottom