Papa Awaomba Radhi Watoto Waliolawitiwa na Wachungaji

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Papa Awaomba Radhi Watoto Waliolawitiwa na Wachungaji
4251242.jpg

Papa Benedict XVI Saturday, March 20, 2010 3:52 PM
Papa Benedict XVI ametoa tamko rasmi la kuwaomba radhi wahanga wa skendo la wachungaji kuwalawiti na kuwanyanyasa kijinsia watoto waliokuwa wakienda kanisani. Skendo hilo limeyakumba makanisa ya kanisa katoliki katika nchi mbali mbali duniani lakini Ireland ndio iliyotajwa zaidi kwa idadi kubwa ya watoto walionyanyaswa kijinsia na wachungaji huku kanisa katoliki nchini Ireland likifunika maovu ya wachungaji wake ili kanisa lisiharibiwe sifa yake.

"Najua mmenyanyasika sana na kufanyiwa ukatili na nawaomba radhi sana wote waliokumbwa na maovu haya", alisema Papa katika taarifa yake kwa makanisa ya Ireland.

"Najua hakuna kitu kinachoweza kuuondosha uovu mliofanyiwa, Imani zenu kwa kanisa zimesalitiwa".

"Sote tumekumbwa na skendo linalotokana madhambi ya baadhi ya wadau wa kanisa".

"Madhambi makubwa yamefanyika dhidi ya watoto wasio na utetezi wowote".

"Najua baadhi yenu mnaona ni vigumu hata kuingia tena kwenye milango ya kanisa baada ya yote haya yaliyotokea", aliendelea kusema Papa Benedict.

Kwa miaka zaidi ya 10 wachungaji na viongozi wa kanisa wameharibu imani za watu ndani ya kanisa, alisema Papa katika taarifa yake ambayo itasomwa kwenye makanisa karibia yote nchini Ireland wakati wa misa ya jumapili.

Maskendo ya ngono yanayowahusisha wachungaji na watoto wa kiume yamekuwa yakiripotiwa katika nchi mbali mbali duniani huku nchi zilizokumbwa zaidi na maskendo hayo zikitajwa kuwa ni Austria, Uswizi, Uholanzi, Brazil, Mexico na hata dayosisi ya kanisa la zamani la Papa nchini Ujerumani imo kwenye skendo hilo.

Papa alisema kuwa miaka ya kuficha maovu ya wachungaji waovu imeisha na ametaka wachungaji watakaogundulika kuendeleza maovu yao waripotiwe polisi.

Papa aliongeza kuwa katika miaka iliyopita ameishakutana na baadhi ya wahanga wa skendo hilo kutoka nchi mbalimbali duniani na anatarajia kufanya hivyo tena baadae.
 
Back
Top Bottom