SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Hata miezi miwili haijapita tangu kuhamishwa kwa askofu Methodius Kilaini kwenda kuwa askofu msaidizi wa Bukoba, Papa Benedict XVI amewateua mapadri wawili kuwa maaskofu wasaidizi wa jimbo kuu la DSalaam. Wawili hao ni Padri Salutaris Libena na Padri Eusebius Nzigilwa.
Wakati askofu Kilaini alikuwa na Phd. Sasa jimbo limempata professa kwani mmoja wa hao watakaokuwa maaskofu wasaidizi ni Professa (Padri) Salutaris Libena ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa na ni mhadhiri kwenye seminari kuu ya Kipalapala iliyoko nje ya mji wa Tabora. Vilevile alikuwa mkurugenzi wa kiroho au spiritual director wa seminari hiyo. Yeye (Libena) alikuwa ni padri wa jimbo la Mahenge kule kwa askofu Ndorobho nadhani na nimzaliwa wa Itete.
Mwenzake Padri Eusebius Nzigilwa ni padri wa jimbo la DSalaam na ni mzaliwa wa Mwanza na amewahi kuwa rector wa seminary ndogo ya Visiga iliyoko mkoa wa Pwani karibu na Kongowe.
Hivyo jimbo kuu la DSalaam sasa linakuwa na maaskofu watatu yaani Kadinali Polycarp Pengo na hawa wasaidizi wake wawili. Aliondoka mmoja yaani Kilaini sasa wameletwa wawili kwa mpigo.
Chanzo: RADIO TUMAINI