Panya Road: Uhalisia au Nadharia?

Cardinal06

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
963
326
Niko huku wanakopaita mkoani (nje ya Dar) na nimeckia kilichotokea huko jijini Dar cku chache zilizopita, wengi wa viongoz wanaolizungumzia suala hili wanasema kwamba hiki kikundi HAKIPO na ni vijana wachache tu wenye lengo la kufanya uporaji. Naomba kwa wenye kufaham suala hili wanipe ufafanuz juu ya uhalisia wa tukio hili!! Je hili kundi lipo?? Mazoez au mafunzo yao wanayafanya wapi??
 
Dar kuna makundi mengi kuna Waghana, Wamarekani weusi, Panya road, Mbwa mwitu hawa mbwa mwitu hupatikana zaidi kiwalani....hawana mazoezi maalumu na sehemu maalamu ya kufanya mazodzi ni makundi ya watoto watukutu, mateja na wale wa mitaani. Sio nadharia...wapo!
 
Asante mkuu.
 
Hakuna cha panya road wala nini, wananchi wamekalia woga tu, hii habari imebaki ni ya kusadikika tu, hakuna ushahidi wa moja kwa moja zaidi ya kutuonyesha picha za madogo wakiwa kwenye pozi kabisa na nyingine za wananchi wakitimua mbio bila kufukuzwa na mtu yeyote!
 
Dar kuna makundi mengi kuna Waghana, Wamarekani weusi, Panya road, Mbwa mwitu hawa mbwa mwitu hupatikana zaidi kiwalani....hawana mazoezi maalumu na sehemu maalamu ya kufanya mazodzi ni makundi ya watoto watukutu, mateja na wale wa mitaani. Sio nadharia...wapo!

Lakini hayana impact kubwa kama inavyokuzwa...hayana uwezo wa kuteka jiji zima na kufanya watu walale SAA mbili...wanadhibitika kirahisi tuu...

Tatizo wanakuzwa sanaaa...
 
Haya makundi yalikuwa yanajulikana kama Camps, siku za sikukuu utawakuta wamekodi magari, nyuma wamefunga matambara yaliyochorwa wanaenda zao beach ( wanapendelea sana dege beach sijui kwa nini)
Huku magari yakiwa katika mwendo kasi, wengine wanachungulia dirishani....

Ni organization za vijana wa mtaani, na Mara nyingi unaweza kukuta kuna bifu kati ya kundi moja na lingine....si ajabu kukuta wamefunga mtaa na wanazichapa kisa wanagombea msichana au kisa matokeo ya Mpira.

Ni vikundi vinavyodhibitika, hawana ubavu wa kutingisha hata mtaa, sembuse jiji zima....

Wanasiasa wanayatumia sana haya makundi wakati wa kampeni, huwafungia kigodoro wacheze, kuwaandalia kombe LA mchangani (utasikia kombe LA diwani, LA mbunge) kuwanunulia pombe na kuwapa ahadi hewa....Ndo maana haya makundi hayafi, yanajua ulaji wao uko wakati wa uchaguzi!

Hii panya road iliyokuzwa ni muendelezo tu wa episodes za Director wa ulimboka Saga ili kuzima Escrow....na tushasahau.

Halafu niulize hivi yule alowekwa kiporo kashachacha au ndo kapashwa moto analika kama kawa?
 
Back
Top Bottom