Midavudavu
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 287
- 59
Jamaa mmoja mkazi wa Kihonda Kwa Mkomola aliwavunja wenzie Mbavu katika daladala. Akiwa ndani ya daladala alipigiwa simu na mgeni wake ambae alikuwa anafika Morogoro kwa mara ya kwanza. Mgeni alitaka kujua jamaa anakaa wapi ili amtembelee. Basi yeye akamjibu " kwangu huwezi kupotea, wewe panda daladala za kihondo ukisikia harufu mbaya tu utakuwa umefika kwangu mwambie konda akushushe". kazi kwenu Viongozi wa Manispaa ya Morogoro; harufu kali ya viwanda imekuwa kituo cha daladala kwa wageni.