Pana upendo hapa au ndo kuwa mshika pembe?

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Wanajamvi nimekutwa na swaib moja, xgirlfriend wangu ambae tuliachana kama miaka minne nyuma kipindi hicho tukiwa ndo kwanza tumeanza tu chuo leo anadai bado ananipenda,
nakumbuka tulipomaliza A'level mimi nilipangiwa Udsm, yeye akapata Tumaini,
sasa mwanzoni tu baada ya kuingia chuoni yeye akadai hawezi mapenzi ya mbali so tutengane tuu maana hata weza kuniamini,kwakuwa hatukua na ugomvi na hapo ni baada ya kumsisitiza kuniamini kushindwa nikaridhia kwa moyo mmoja, yeye kule akaanza mahusiano na mimi kwa upande wangu nikapata dem mwingine. Tulikuwa tukiwasiliana kwa nadra sana kama marafiki lakini ikafika kipindi akanikataza nisiwasiliane nae kwani, anampenda sana mtu wake na hataki kumkwaza, wakati mwingine nikawa namfwata mkoani akiwa likizo ili japo nimwone sababu nilimpenda sana, na siku za mwanzo nilifikiri uhusiano wangu mpya ungenifariji kumbe ikawa ngumu maana bado nilimpenda yeye, lakini hakuwa tayari kurudisha moyo nyuma.
Ishu ikaja mwaka jana mwanzoni nikapata mishe iliyoniwezesha kutoka Bongo nakuja state, alichelewa kufahamu kama sipo nchini sasa majuzi kati tukakutana kwenye FaceBook, na tukawasiliana,ishu inakuja anadai ananipenda sana na yuko tayari kubrake na jamaa yake,
Kwakweli kila nikipima naona huyu ni walewale maana nini sasa kinamfanya anipende leo?
Je jamaa yake aliyenae itakuwaje? huu si ubinafsi? wandugu nishaurini.
 
Hmmmmmm! huyu ameweka maslahi mbele zaidi badala ya mapenzi ya kweli. Ulipokuwa bongo hakutaka hata kuwasiliana nawe sasa uko states anataka kuwa nawe! Kama bado unampenda na unataka kuwa naye basi fanya maamuzi muhimu vinginevyo usipoteze muda wako kwa mtu ambaye hana mapenzi ya kweli kwako.
 
Mshirikishe na Mungu pia, maana huwezi kujua yawezekana huyo ndo ubavu wako. Katika safari yoyote kuna kuanguka, kuumia, kukata tamaa lakini cha Mungu huwa kinasimama na kudumu.
 
.....Huyo hana lolote kadata kusikia upo states, yaani kuna baadhi ya wadada wakisikia mtu yupo nje ya nchi huwa wanachanganyikiwa kweli hadi kuacha wapenzi wao kisa kumpata mtu aliye nje ya nchi. Penzi hakuna hapo.......kama kweli alikupenda kwa nini hakukupenda kipindi upo nyumbani?
Si alisema penzi la mbali haliwezi? Kama Dar na Iringa alisema mbali, states leo imekuwa jirani?Iweje leo aseme anakupenda na wakati upo mbali zaidi tena nje ya nchi........mpotezeeeee huyo.
 
.....Huyo hana lolote kadata kusikia upo states, yaani kuna baadhi ya wadada wakisikia mtu yupo nje ya nchi huwa wanachanganyikiwa kweli hadi kuacha wapenzi wao kisa kumpata mtu aliye nje ya nchi. Penzi hakuna hapo.......kama kweli alikupenda kwa nini hakukupenda kipindi upo nyumbani?
Si alisema penzi la mbali haliwezi? Kama Dar na Iringa alisema mbali, states leo imekuwa jirani?Iweje leo aseme anakupenda na wakati upo mbali zaidi tena nje ya nchi........mpotezeeeee huyo.

Mhhhhhh! we kichwa sana. Kachanga hakajambo?

 
Lakini kny mapenzu tunaweza shauri afu ukaenda kumwonyesha watu kny jf walivyoponda uamuzi wako kaka sema na moyo wako nae aseme na moyo wake
 
Hapo hamna mapenzi ndugu yagu,huyo dada yupo kimaslahi zaidi. If i were you wala nisingepoteza muda wangu kumfikiria hata kama nilimpenda kuliko kawaida. Sasa kama mapenzi ya mbali hayawezi kwa sasa atayawezaje? Na je ingekuwa upo nae karibu then ukamuoa bahati mbaya au nzuri ukapata safari ina maana angeshindwa kuwa mvumilivu maana hawezi mapenzi ya mbali.

Usipumbazwe ndugu yangu,japo unampenda ila yy hana penzi la dhati mpotezee tu huyo atakuletea matatizo bureeeee
 
Usidanganyike!Mwenzio kaona mwanya wa kwenda majuu ndio unaomdatisha!!Kwanza ilikua mapenzi ya mbali hayawezi..leo hii umeenda mbali zaidi anakutaka!Then ikawa anampenda sana mpenzi wake wa sasa hataki kumkwaza leo yuko tayari kumuacha!?SHTUKA!
 
Lakini kny mapenzu tunaweza shauri afu ukaenda kumwonyesha watu kny jf walivyoponda uamuzi wako kaka sema na moyo wako nae aseme na moyo wake

Hapo umesema jambo kweli mshauri wa mtu wa mwisho kabisa ni moyo wake mwenyewe.
 
wengi wetu tuna tamaa sana na kushobokea vitu. Mi sijui tuna matatizo gani. Aaagghh.....
Lakini wadada wengi wanapenda kwenda States, sio wa Tz peke yao.. Na kwa sababu hawajawa empowered and they poses no skills, tiketi pekee ya kufika huko ni 'miili' yao.
 
Mmmh nadhani sasa nashawishika kukufahamu, hio stori inafanana na classmate wangu, ngoja nitaki-PM ila kama ni wewe mmh na demu ndo yule hata sikushauri, but kama bado unamhitaji rudi mpwa! ila usijetusemea kuwa tumemponda
 
Km jina lako lilivyo "HUNTER", kuwa mwindaji shujaa na si kutegemea MIZOGA(hahahahahah) maisha lazima yaendelee kaka huyo ni opportunist tu, sie washika dini tuanesema UKIONA HIVYO UJUE MUNGU KAKUEPUSHA NA JAMBO, na jambo lenyewe sasa unaliona, huyo DADA ni mpenda mambo safi aliposikia upo mtoni akajua kabisa life umeishaipatia so anajirudisha kinyemela. Mkuu Hunter piga moyo konde tafuta umpendaye na atayekupenda kwa MOYO wote na si huyo anayeweza kuujeruhi MOYO wako
 
majority ya wasichana/wanawake leo ni maslahi tu, hayo mapenzi ya kuigiza ni ngazi tu ya kupandia kwenye maslahi!
 
lakini wadada wengi wanapenda kwenda states, sio wa tz peke yao.. Na kwa sababu hawajawa empowered and they poses any no skills, tiketi pekee ya kufika huko ni 'miili' yao.

this is so sad!!!! Sijui ni lini ss mabinti tutaacha kujidhalilisha.
 
kwa kifupi,wakati upo dar ulikuwa chini ya jamaa yake mpya wa tumaini.Sasa upo USA umepanda chati kuliko jamaa yake,hivyo ukimrudia akija USA atakutana watu walio juu yako ki uwezo,uelewa etc,so atakuacha na kuhamia kwa jamaa aliye juu yako.
so kaka akili kichwani kwako,kama bado unaisikiliizia K wewe mkubalie ukijua tu iko siku atakuacha.else mpotezee mpe live kuwa hamna mapenzi.
 
kwa kifupi,wakati upo dar ulikuwa chini ya jamaa yake mpya wa tumaini.sasa upo usa umepanda chati kuliko jamaa yake,hivyo ukimrudia akija usa atakutana watu walio juu yako ki uwezo,uelewa etc,so atakuacha na kuhamia kwa jamaa aliye juu yako.
So kaka akili kichwani kwako,kama bado unaisikiliizia k wewe mkubalie ukijua tu iko siku atakuacha.else mpotezee mpe live kuwa hamna mapenzi.

yo very right mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom