Pamoja na mambo mengine mchango wa Mwalimu Julius Nyerere uko kwenye vitabu alivyoandika

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wanaJF, huwa nawaheshimu sana watu wanaopata muda wa kukaa chini na kusoma/kutunga/kuandika vitabu. Kati ya marais wa Tanzania, ni Mwalimu Julius Nyerere tu ndiye aliyekuwa na muda wa kukaa chini/kusoma/kutunga/kuandika vitabu vingi zaidi ukilinganisha na 'successors' wake.

Ametuachia mchango mkubwa sana na leo hii vitabu vyake vinasomwa na watu mbalimbali duniani kwani maktaba nyingi hazikosi vitabu vyake. Hii inatufundisha nini?
 
Usemayo ni kweli kabisa. Nyerere hakuwa na muda wa kuongoza kama inavyopaswa, baada ya miaka 25 katuwacha maskini wa kutupwa. Hatuna hata kandambili. Benki kuu kweupeeee. Alikuwa bize kuandika vitabu tu. Sijui ulitegemea nini kutoka kwa Mwalim wa English literature?
 
Usemayo ni kweli kabisa. Nyerere hakuwa na muda wa kuongoza kama inavyopaswa, baada ya miaka 25 katuwacha maskini wa kutupwa. Hatuna hata kandambili. Benki kuu kweupeeee. Alikuwa bize kuandika vitabu tu.

Na miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete tumekuwa matajiri? Nchi iko gizani, ajira hakuna, rasilimali zetu chungu nzima zinachukuliwa usiku na mchana na wachukuaji wa rasilimali hizo hata kodi hawalipi, malalamiko ya wananchi kuhusu gharama kubwa za maisha yapo kila kona ya nchi yetu. Je, kuna ahueni yoyote tangu Mwalimu ang'atuke miaka 26 iliyopita? Mwalimu alikuwa bora sana kama kiongozi ukilinganisha na hawa wote waliomfuata ambao juhudi zao kubwa ni kuiangamiza nchi na kujitajirisha wao, familia zao na marafiki wao wa karibu.
 
Miaka 24 ya uongozi wake nchi haina barabara,maji,umeme,shule,vyuo,hospitali watz tulitembelea katambuga,tulivaa magunia!HIVI ALIYEANGAMIZA NCHI NANI? WA MIAKA 24?au wa miaka 5?
 
Back
Top Bottom