Pambano la cheka na kaseba

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,364
Wakuu mwenyekujua matokeo au update za hawa jamaa atawekee hapa!
 
Huwa wanaanza mpambano wao saa 3.30 hivi usiku hadi saa 6 hivi ndio litaisha,kwa sasa bado mapema mapambano ya utangulizi kwenda mbele
 
Huwa wanaanza mpambano wao saa 3.30 hivi usiku hadi saa 6 hivi ndio litaisha,kwa sasa bado mapema mapambano ya utangulizi kwenda mbele

Unajuaje litaisha saa sita au mmeshapanga matokeo, maana akilambwa mtu knockout mapema mapema itakuwaje?
 
Kama Cheka akimpiga tena, bora arudi zake kwenye Mieleka sasa..
 
Kama Cheka akimpiga tena, bora arudi zake kwenye Mieleka sasa..

Atadundwa tu. Hivi unafikiri Cheka anacheka na kima? Muuliza yule Mkurya Madam Maugo, mdomo wote kwisha, ametudhalilisha watu wa mkoa wa Mara kwa kurukia Lori la magereza.

Hivi wakuu, huu uhodo wa kumuona Kaseba akidundwa tutauona live kupitia TV gani?
 
Jamani ma promota wa cheka haya si mashindano ya kumpa, mtafutieni mapambano ya kimataifa km ya wbo, wbc, wba lkn kibongo bongo cheka akikaa 1yr atakuwa amelost
 
Mliopo huko mtupatie update basi wakuu! Afu nilisikia mida fulani wema na wolpa walikua jukuani nani kashinda?
 
Hatimaye ule ubishi kati ya Mabondia wawili waliokuwa wakitambiana kila kukicha Francis Cheka na Japhet Kaseba umemalizwa usiku huu wa 7-7-2012.

Cheka aogopa kichapo kitakatifu toka kwa mbabe Japhet Kaseba na hatimaye Kaseba kutangazwa mshindi wa pambano hilo lililokuwa chini ya TPBO.

Na katika hali ya kusikitisha TAMASHA HILO lilikuwa Very Unorganized kabisa yaani Watazamaji wameliwa pesa zao na sasa inabidi serikali itoe tamko kutokana na Uwizi wa kimacho macho uliofanyika katika tamasha hilo.

Nawasilisha.

Source: Mimi Mwenyewe nilikuwepo Uwanja wa Taifa.
 
Duh! Jamaa kahofia makonde mazito mazito toka kwa mpinzani wake!

Je? Pambano ilikuwa imfanyike mchana ama usiku????
Ama ni mbinu ya washika dau kuwanyang'ang'anya watazamaji pesa zao?

Hebu tufafanulie mambo yalivyokuwa Blood Hurricane kwa mtazamo wako wa kuona na kuvumbua!
 
na lile pambano kati ya wolper na wema sepetu nani ameshinda

WEMA SEPETU, JACQUELINE WOLPER HAKUNA MBABE

Wema akipata mawaidha kutoka kwa mwalimu wake Rashid Matumla.
Waigizaji mahiri wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper wametoka suruhu katika mpambano wao wa raundi 2 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar e Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini
 
Cheka kachomoa kupigana pambano lilitakiwa lianza saa 5:00 za usiku jamaa kachomoa kakimbia. Kafika ulingoni kauza sura kasepa ndio nini sasa! Aibu mbaya.
 
Duh! Jamaa kahofia makonde mazito mazito toka kwa mpinzani wake!

Je? Pambano ilikuwa imfanyike mchana ama usiku????
Ama ni mbinu ya washika dau kuwanyang'ang'anya watazamaji pesa zao?

Hebu tufafanulie mambo yalivyokuwa Blood Hurricane kwa mtazamo wako wa kuona na kuvumbua!

Cheka kachomoa kupigana pambano lilitakiwa lianza saa 5:00 za usiku jamaa kachomoa kakimbia. Kafika ulingoni kauza sura kasepa ndio nini sasa! Aibu mbaya.
 
Hii imenikumbusha pambano la "IRON" MIKE TYSON vs ANDREW GOLOTA...Baada ya round ya pili kuisha GOLOTA akiwa katika corner yake aliinuka na kusema hawezi kuendelea na pambano.
Mashabiki waliolipa pesa zao walianza kumtupia GOLOTA vinjwaji na uchafu mwingine wakati anaondoka ulingoni.

Huku kila mmoja akisema lake, GOLOTA aliomba radhi mashabiki wake na kusema ngumi zilikuwa hazivumiliki 'nzito sana' na baadae iligundulika kuwa GOLOTA alivunjika mfupa kichwani na kama angeendelea basi ungemsababishia madhara katika ubongo.

ie; nakumbuka jamaa alikuwa kama kachanganikiwa alianza kuvutana na watu wa corner yake.
 
Cheka kachomoa kupigana pambano lilitakiwa lianza saa 5:00 za usiku jamaa kachomoa kakimbia. Kafika ulingoni kauza sura kasepa ndio nini sasa! Aibu mbaya.

Huyu kajidhalilisha mwenyewe!

Hana mana ktk mchezo aliouchagua hata kidogo!
 
Tangia awali kaseba alishasema cheka akishaenda kijijini kwao akirudi huwa anakataa ama kukubali pambano basi kutakuwa na ukweli ndani yake! Aibu kwake cheka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom