Pamba imetangaza bei ni 650/= kwa Kilo Wabunge waliosema bila Buku hakuna pamba watajiuzulu?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Napenda kufahamu kwa wabunge hasa wale wa kanda wanazolima Pamba kwa kauli yao Bila buku (1,000/=) hakuna kilo ya Pamba.

Sasa nauliza hawa wabunge kwa kushindwa kwa kauli mbiu yao watakubali kuwajibika kwa kutowatendea wapiga kura wao haki????
 
Nasikia Zambia, wakulima wengine walichoma moto sokoni pamba yao sababu ya kushuka sana kwa bei. Ulaya normally wakulima wanakuwa subsized.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma akina mzee lupondije akiwa mbunge na pia mwenyekiti wa chama cha ushirika cha mwanza(NYANZA);walisababisha CCM kuchukiwa mwanza kwa kusababisha wakulima wa pamba kukopwa na kutokulipwa kabisa.Baada ya mzee kufa , CCM ilipata taabu sana kurudisha kiti cha ubunge , ndo mze mapesa akashindwa,maana wananchi waliamua kukiadhibu chama kwa msingi huo.Hili ni somo tosha, nakumbuka chanzo cha nyanza kufa mwanza ni wabunge haohao wa ccm, kama mheshimiwa dalali ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa nyanza.Amefaulu kuuza na kusababisha mali nyingi kuuzwa kihorela.nachela kusema, pamba kwa kanda ya ziwa ndo dhahabu.najua mbunge wangu ndo mwenyekiti wa bodi ya pamba ambayo ambayo si chombo cha kutetea zao la pamba .Bodi ya pamba ndo tanuru la kuua zao la pamba.namjua mbunge wangu , hata ubunge kapata kinyemela.hawezi jiuzulu sababu yeye ndo chanzo cha tatizo hili.Ni ukweli usiopingika kuwa bila kutafuta mbinu za makusudi wasipohangaikia kurudisha khali wengi watapoteza ubunge hata kama hawatajiuzulu.kanda ya ziwa wananchi wameamka.
 
Tatizo la wabunge wanatafuta umaarufu wa wapiga kura, Hivi mtu km cheyo ambaye inaaminika ni msomi wa kirusi( textile Technologist) kama anavyojiita iweje autangazie umma kuwa no buku no cotton hali anajua kabisa soko la kimataifa limeanguka. Huu ni upuuzi mtupu, tunawadanganya wananchi kwa kutumia udhaifu wao wa kuwa mashambani. sasa msimu umetangazwa tuone sasa km hiyo buku itatoka, na huu ndio mwanzo wenu wa kufa kisiasa nyie wabunge wa kanda ya ziwa, mtakoma mimi kwangu sawa tu sina hasara mkikosa ubunge kwa kauli zenu km hizi.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma akina mzee lupondije akiwa mbunge na pia mwenyekiti wa chama cha ushirika cha mwanza(NYANZA);walisababisha CCM kuchukiwa mwanza kwa kusababisha wakulima wa pamba kukopwa na kutokulipwa kabisa.Baada ya mzee kufa , CCM ilipata taabu sana kurudisha kiti cha ubunge , ndo mze mapesa akashindwa,maana wananchi waliamua kukiadhibu chama kwa msingi huo.Hili ni somo tosha, nakumbuka chanzo cha nyanza kufa mwanza ni wabunge haohao wa ccm, kama mheshimiwa dalali ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa nyanza.Amefaulu kuuza na kusababisha mali nyingi kuuzwa kihorela.nachela kusema, pamba kwa kanda ya ziwa ndo dhahabu.najua mbunge wangu ndo mwenyekiti wa bodi ya pamba ambayo ambayo si chombo cha kutetea zao la pamba .Bodi ya pamba ndo tanuru la kuua zao la pamba.namjua mbunge wangu , hata ubunge kapata kinyemela.hawezi jiuzulu sababu yeye ndo chanzo cha tatizo hili.Ni ukweli usiopingika kuwa bila kutafuta mbinu za makusudi wasipohangaikia kurudisha khali wengi watapoteza ubunge hata kama hawatajiuzulu.kanda ya ziwa wananchi wameamka.

Funguka vzr, Mbunge wako ni nani? mie tatizo lipo kwa wabunge na watendaji wengine katika hio mikoa ya Pamba na maeneo mengine ambayo wanadhani kutegemea zao moja "kama dhahabu", wananchi wanatakiwa kupewa kila alternative (opportunities) ili wasiweze kunyanyaswa na kuongopewa kuwa bila 1,000 hakuna kitu?je wanadhani wakulima watapata wapi fedha ya kujikimu? kwa nini wasishauri serikali (bodi ya pamba) inunue hiyo pamba kwa bei hio 1,000/= ili wamalizane na wakulima na wao (bodi serikali) wabanane kusubiri bei ya dunia kupanda? wabunge, serikali na bodi ya pamba hawapo kwa ajili ya wakulima ila wanatafuta umaarufu tu.
 
Back
Top Bottom